Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Yule bwege alosema wasitishe uokoaji bado kakalia kiti chake tu?
Haki ya nani hii Serikali hii basi tu
Wacha ninyamaze
 
Dah hii nchi ni ngumu sana.
"Et mkata tiketi alizama kwenye maji pamoja ma mashine aliyokatia tiketi kwahio hatuwezi kujua idadi kamili iliyokuwemo kwenye kivuko"
 
Kuna tatizo gani kuandika hicho kilichoonwa na mashuhuda hapa?
 
Dah hii nchi ni ngumu sana.
"Et mkata tiketi alizama kwenye maji pamoja ma mashine aliyokatia tiketi kwahio hatuwezi kujua idadi kamili iliyokuwemo kwenye kivuko"
Basi linapoondoka kituoni huwa wanasaini kwa polisi bila shaka ni muda pamoja na idadi ya watu sasa hawa ndg zetu bado wako analogy kama CCM
 
Yale maboya yanatakiwa yawe free ili emergency inapotokea yawe yanaelea tu majini na watu waweze kujiokolea
ni kweli kiongozi , ila ni wakati sasa hao temesa waulizwe nini maana ya maboya kufungiwa vile?mbona wezetu baadhi wananinginia pembeni tu kuzunguka ata boti au kwanini abiria wasiwe wanayavaa kabisa kwa hivi vivuko vifupi kanda ya ziwa??ni sheria gani inayosema yafungiwe mule?
 
Ile ilikuwa ni planning 1 thinking kwanini uokoaji usitishwe hadi asubuhi walikuwa wanataka idadi ya watu walio kuwa wanawataka... cc Mshana Jr
 
Someni vitabu vitakatifu mataifa yanaondesha dhulma Mungu hayaachi salama. Ishara ya mwanzo-warning shot tujirekebishe.God's justice is restorative.
 
ySi useme tu kilichoonwa unaogopa nini?.... Ajali imeshatokea hakuna siri tena
 
Ni ktu gan kinachowez kudisturb stability? Sio mpngo wa mzigo?
So manya factors mkuu. Kuzitaja chache, Moja kupanga mzigo vibaya mfano uzito zaidi kuwa upande wa juu kiasi cha kuhamisha center of gravity kuelekea juu na kupunguza kina kati ya metercenter na center of gravity, au kupakia mzigo zaidi upande mmoja au pia kutoudhibiti mzigo sawasawa(lashing) kiasi kukitokea nguvu yeyote mzigo unahama yaani cargo shifting mfano meli ikiyumba sababu ya wimbi au kukata kona kali. Sababu zipo nyingi wakati mwingine hata uundaji wa meli yenyewe unaweza kuwa usiokidhi viwango
 
Mkuu umeongea ukweli kabisa,kunakipindi pale dsm feri kunawatu walizama pale mida ya saa 12 lkn hakuna juhudi zozote zilizofanywa hadi kesho ake mida ya saa sita ndo wanakuja na matumbo yao ufukweni na bado kazi na vifaa wakakabiziwa wavuvi ndo wakaingia kwenda kuokoa.Kitu nachojiuliza hiyo taaluma walisomea au waliwekwa tuu cuz ambao hawana(wavuvi) ndio walijitahidi siku ya tukio kuokoa baadh yao na ilipoingia usiku wakatimuliwa kesho ake tena haohao ndo wakahitajika.

"Yajayo yanafurahisha,mpo tayarii".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…