mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
[emoji112][emoji112]Unafikiri angekuwemo mama yake kichaa huo uokoaji ungeghairiswa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji112][emoji112]Unafikiri angekuwemo mama yake kichaa huo uokoaji ungeghairiswa?
Kuna tatizo gani kuandika hicho kilichoonwa na mashuhuda hapa?Engine mbili zilizokuwa mbovu zishabadilishwa. Na hawana hata mwezi toka kivuko kimeanza fanya kazi. Ndo maana nakwambia shida sio kivuko. Nisingependa andika mtandaoni kilichoonwa na mashuhuda wa ajari, lakini shortly ni human actions. Uzuri captains wa3 wa kivuko wamepona, hivyo wataeleza baadae nini kilisababisha. Ila jua tu kivuko kilikuwa full fit.
Basi linapoondoka kituoni huwa wanasaini kwa polisi bila shaka ni muda pamoja na idadi ya watu sasa hawa ndg zetu bado wako analogy kama CCMDah hii nchi ni ngumu sana.
"Et mkata tiketi alizama kwenye maji pamoja ma mashine aliyokatia tiketi kwahio hatuwezi kujua idadi kamili iliyokuwemo kwenye kivuko"
ni kweli kiongozi , ila ni wakati sasa hao temesa waulizwe nini maana ya maboya kufungiwa vile?mbona wezetu baadhi wananinginia pembeni tu kuzunguka ata boti au kwanini abiria wasiwe wanayavaa kabisa kwa hivi vivuko vifupi kanda ya ziwa??ni sheria gani inayosema yafungiwe mule?Yale maboya yanatakiwa yawe free ili emergency inapotokea yawe yanaelea tu majini na watu waweze kujiokolea
Ile ilikuwa ni planning 1 thinking kwanini uokoaji usitishwe hadi asubuhi walikuwa wanataka idadi ya watu walio kuwa wanawataka... cc Mshana JrEngine mbili zilizokuwa mbovu zishabadilishwa. Na hawana hata mwezi toka kivuko kimeanza fanya kazi. Ndo maana nakwambia shida sio kivuko. Nisingependa andika mtandaoni kilichoonwa na mashuhuda wa ajari, lakini shortly ni human actions. Uzuri captains wa3 wa kivuko wamepona, hivyo wataeleza baadae nini kilisababisha. Ila jua tu kivuko kilikuwa full fit.
ySi useme tu kilichoonwa unaogopa nini?.... Ajali imeshatokea hakuna siri tenaEngine mbili zilizokuwa mbovu zishabadilishwa. Na hawana hata mwezi toka kivuko kimeanza fanya kazi. Ndo maana nakwambia shida sio kivuko. Nisingependa andika mtandaoni kilichoonwa na mashuhuda wa ajari, lakini shortly ni human actions. Uzuri captains wa3 wa kivuko wamepona, hivyo wataeleza baadae nini kilisababisha. Ila jua tu kivuko kilikuwa full fit.
So manya factors mkuu. Kuzitaja chache, Moja kupanga mzigo vibaya mfano uzito zaidi kuwa upande wa juu kiasi cha kuhamisha center of gravity kuelekea juu na kupunguza kina kati ya metercenter na center of gravity, au kupakia mzigo zaidi upande mmoja au pia kutoudhibiti mzigo sawasawa(lashing) kiasi kukitokea nguvu yeyote mzigo unahama yaani cargo shifting mfano meli ikiyumba sababu ya wimbi au kukata kona kali. Sababu zipo nyingi wakati mwingine hata uundaji wa meli yenyewe unaweza kuwa usiokidhi viwangoNi ktu gan kinachowez kudisturb stability? Sio mpngo wa mzigo?
Mkuu umeongea ukweli kabisa,kunakipindi pale dsm feri kunawatu walizama pale mida ya saa 12 lkn hakuna juhudi zozote zilizofanywa hadi kesho ake mida ya saa sita ndo wanakuja na matumbo yao ufukweni na bado kazi na vifaa wakakabiziwa wavuvi ndo wakaingia kwenda kuokoa.Kitu nachojiuliza hiyo taaluma walisomea au waliwekwa tuu cuz ambao hawana(wavuvi) ndio walijitahidi siku ya tukio kuokoa baadh yao na ilipoingia usiku wakatimuliwa kesho ake tena haohao ndo wakahitajika.NIMEUMIA SANA
Anaandika Kijana Msomi
Rashid Chilumba
Nimesikia zoezi la uokoaji kwenye ajali ya kivuko Mwanza limesitishwa hadi kesho kutokana na kiza, sasa kesho mtakwenda kuokoa au kuokota Maiti?
Hapo Mwanza kuna kikosi cha Jeshi, boti za doria za polisi, helikopta na vivuko vingine? Hivi kweli vyote hivyo havina taa kubwa za kuwezesha zoezi la uokozi kuendelea usiku kucha? Kama havina tulivinunua vya kazi gani?
Ni aibu kwa viongozi kusema tunaenda kulala eti kuna giza ziwani wakati kuna dazani ya watanzania wenzetu tunaowahudumia wamezama ziwani tena siyo kwa uzembe wao bali kwa ujuba na tabia ya kutokujali maisha ya watu na kutosimamia usalama wao.
Mkuu wa mkoa, RPC, mkuu wa kamandi ya Jeshi la Wananchi, Mkuu wa Bandari Mwanza mnapata wapi ujasiri wa kwenda kulala na kuna watu watoto wao, baba zao, Mama zao wamo majini na hawajui kama watawapata wakiwa hai? Hivi ingelikuwa ni jamaa zenu wa karibu mngepata ujasiri wa kusimamisha zoezi kwa sababu ya kiza?
Katika dunia ya leo seriously kabisa mnasema kiza kinawazuia kuokoa watu? Aiseee.... Kwa hiyo hao waliozama ikiwa kwa bahati bado wapo hai hadi sasa mnategemea Israeli atawangoja ninyi hadi kesho jua litapochomoza? Huu ni uzembe wa hali ya juu mno.
Kweli kabisa mnashindwa kufunga tochi kubwa kama zile za bandari kwenye helikopta moja ya polisi hapo na boti nne tano mkaingia kuwaokoa watanzania wenzetu? Hata ikiwa ni wafu lakini faraja ni kupata japo miili yao hadi kesho samaki, mawimbi ya ziwa nk inaweza kuwa imewapoteza zaidi.
Leo nimeumia sana, makosa yale yake ya Mv Bukoba, Spice Islander, Skagit yamejirudia Mv. Nyerere na watu wanaenda kulala usiku umeingia na vyombo vya habari vinaonesha shilawadu na kutoa dakika kiduchu kwa habari muhimu na msiba mkubwa huo wa taifa.
Na tena mlionywa mara kadhaa kuwa chombo ni kibovu. Mkuu wa bandari ya mwanza bado yupo na wadhifa wake na msimamizi wa Sumatra kanda ya ziwa kesho ataenda pia ofisini.
Mungu awapumzishe waliotangulia na atawalipa waliowasababishia kuzama kwenu kwa uzembe wao.
Cc
Dotto Bulendu
Malisa GJ
Kheri James
Tusaidiane kusema Ndugu zangu. Tunawezaje kwenda kulala na watanzania wenzetu wako majini sasa hivi?