Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kwa iyo umeridhika na kauli kua uokoaji hauendelei sababu ya giza ??? Mungu uyu [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
wapate pumziko la milele wote waliokufa
 
Pole Sana kwa familia zote na ndugu was marehemu...!! Wapumzike kwa Amani... Lakini pia Toka muda kivuko kimepata Ajali mpaka muda wanaahirisha Zoezi la uokoaji hakika Kama mtu hakuonekama kuomba msaada kuokolewa muda huo hakuna uwezekano Kama alikuwa yupo hai bado... Labda waopoe miili iliyonasaa kwenye hicho kivuko Kama wangefanya hiyo kazi Usiku wa Janaa....!! Tusiwe wepesi wa kulaumu Sana bila kuangalia mazingira ya kuarisha zoezi lenyewee hapo ya kualaumiwaa ni SERIKALI na sio mkuu wa mkoaa... Kama rais alisikia na kukaa kimyaa bilaa kutoa Order means yeye ndo wa Kwanza kualumiwa maana hili ni jangaa la kitaifaaa....
 
Hizo bombadia za kubebea waccm kumuunga mkono rahisi
 
Tunaongelea mambo ya uokoaji wa wenzetu waliopata ajali we unaingiza mambo. Ya reli na flyover uko timamu kweli !
 
Sisi uwa mara nyingi tunaopoa siyo kuokoa hasa linapokuja suala la ajali za majini. Nakumbuka kwenye ajali ya MV Bukoba, vifaa na wapiga mbizi ilibidi watoke S.a na bahati mbaya wakakuta jamaa aliyekuwa anajiita Engineer ashawashauri waitoboe meli ili kuokoa watu, huku mvuvi asiye hata na certificate ya physics aliwabishia kuwa waakiitoboa itazama kabisa chini.
 
mkuu sio hivyo na hayajakukuta, si tunalo jeshi la majini, kweli jeshi la majini linashindwa kuwa na vifaa vya kuokolea usiku, hata kama wameshakufa, hii ni aibu, na jeshi la majini lipo, achana na wale wavuvi waliokuwa wanasaidia kutoa miili wakiwa hawana zana zozote zaidi ya mikono yao, imenisikitisha sana
 
Kwa mujibu wa mwananchi mida ya saa nne asubuhi mkuu wa mkoa amesema ni miili 86 imeopolewa..Ukijumlisha na wale hai waliookolewa inaonyesha kivuko kilikuwa na watu wengi kuliko idadi inayostahili ya watu 101.
Mimi nimesikiliza kwenye radio muda siyo mrefu wamesema wamefika 94 waliolala usingizi wa mauti na miili yao kupatikana
 
Kuna hatari ya watu kutmbuliwa.
Mnashindwa kkuleta taa mkaendelea na uokoaji, huku mkuu wa kikosi cha uokoaji yupo, mkuu wa mkoa upo, mkuu wa majeshi upo, boat na meli zipo.
We cannot entertain this. Lazima watu wachukuliwe hatua
natengua............................
 
Nanukuu " Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja."
Swali langu je ndani ya kivuko cha MV nyerere kulikuwepo na hayo magari matatu na watu mia.
Je na kama magari hayakua matatu kuna uwezekano wa kuongeza abiria iki kufika lengo la tani 25?
Maana naona idadi ya waliopo hai na waliokufa imevuka mia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…