Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Hakika nimesikitishwa sana na ajali ya Mv Nyerere.
Masikitiko zaidi ni katika utendejai wa zoezi zima la uokoaji, unawezaje kusitisha zoezi kisa giza , as if kuna namna hao watu wanakungoja.
Let say Familia yake au yeye binafsi angelikuwamo ni mmoja wa wahusika wale aliowaacha usiku na kuwaambia atarudi asubuhi kuendelea na kuwanusuru.
John jitafakari kwenye hilo, umeteleza tena umeteleza pabaya sana.
 
13:20 - WAZIRI ISACK KAMWELWE: ZOEZI LA KUOPOA MIILI ILIYOKWAMA LITAKAMILIKA SAA 12 JIONI LEO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Zoezi haliwezi kukamilika muda huo, Huu ni Uongo
Ukweli ni Kwamba Giza litakua limeingia hivyo hawawezi kuendelea na Zoezi..
 
[http://img2]

Mbunge wa Ukerewe (Chadema), Joseph Mkundi Katika moja ya swali alilouliza bungeni hivi karibuni, Mkundi alitaka kupata kauli ya Serikali jinsi itakavyoshughulikia kivuko hicho ili kisije kusababisha maafa.

“Naomba kupata kauli ya Serikali, ni suala ambalo tumekuwa tunalishughulikia mara kwa mara, tuna kivuko kinachounganisha Ukerewe na kisiwa cha Ukara, kivuko hiki kinahudumia watu zaidi ya 50,000,” amesema Mkundi.

“Kimekuwa kinaleta shida mara kwa mara na nimekuwa nawasiliana na wizara, sipendi siku moja tuje hapa kuomba rambirambi kwa sababu ya wananchi waliozama katika kivuko kile” Ameongeza.
 
Zoezi haliwezi kukamilika muda huo, Huu ni Uongo
Ukweli ni Kwamba Giza litakua limeingia hivyo hawawezi kuendelea na Zoezi..
Waziri muongo.
Yani jamaa anaona watanzania wote ni viazi na yeye tu ndio kasoma na ana upeo wa kika kitu.
Pumbavu zake
 
12:49 "... Litafunguliwa Jalada maalum la kuchunguza tukio la kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere"
Maneno hayo tumesha yazoea sana kila kitu kikitokea utasikia litafunguliwa jalada lakini hakuna matokeo yanayoonekana. Majalada kila siku hata Lissu tuliambiwa wamefungua jalada lakini hakuna lolote linalofanyika. Jalada la MV Bukoba liliishia wapi? Kama mnafungua majalada halafu hakuna mrejesho yafungeni tu mnapoteza makaratasi na kututia hasara bure!
 

Hiyo mifumo inatumika tayari nchi zilizoendelea, ID yako ukiswap mahali inasoma details zako zote. Wakati mwingine mkono wako ukiuweka mahali unasoma details zako zote na hii inawezekana maana wao kila kiumbe kinachozaliwa wanasajili DNA kwa hiyo kwao maisha ni rahisi sana, VITU HIVI UNAWEZA TU KUFANYA KAMA UTAKUWA NA WATU WENYE KUWAZA LEO, KESHO NA MIAKA 1000 MBELE. Kwa sasa tunaweza kutoa kwa haraka National ID na iwe lazima kila mtu kutembea nayo (tukiweza tunaweza kuilink na mifumo ya bima), Kila mtu anapoingia mahali manifest ya kurejista lazima iwepo kwa ajili ya details za mhusika.
 
Mkuu
Hakuna rekodi ya watu walioingia. Naskia ni kupanga tu mstari unaingia chomboni.
Ukisikia statistics za 400 (yaani takwimu za sufuri mbele) huwa ni makadirio ya siyo na uhalisia.
Pathetic agencies!

Hii ni basic ambayo inatushinda sasa kwanini tunakimbilia mambo makubwa wakati kumbe hata msingi wa vitu vidogo hatuuwezi, Hata hivyo vikubwa vitatushinda sasa.
 
Msiba wa Taifa uliotokea katika visiwa Vya Ukerewe sI pigo TU KWA N YETU NA FAMILIA ZILIZOPOTEZA WAPENDWA WAO bali pia ni AIBU kwa TAIFA letu.

HATUJIFUNZI ama hatutaki KUJIFUNZA maksudi kutokana na majanga yaliyowahi kutokea huko nyuma
ikiwemo utayari wa UOKOAJI.
Janga hili lingeweza KUZUILIKA ila basi tu....!!!

i
Kwa kifupi. hii NEGLIGENCE/UZEMBE wa hali ya juu sana ambao mtu ama watu wanahitaji KUWAJIBISHWA!!

Uzembe huu si tu kwa nahodha wa chombo hicho au waliokuwa wakikata tikikti bali ni UZEMBE
wa WIZARA na Tassis zake HUSIKA.

Katika nchi zilizoendelea janga kubwa kama hili likitokea ambalo LINGEWEZA KUZUILIKA lakini likaachwa lijishughulikie lenyewe basi
WAZIRI huwa anachukuwa jukumu la KUJIUZULU.
Si kwa sababu YEYE ALIHUSIKA DIRECTLY bali kama kuchukuwa POLITICAL RESPONSIBILITY la uzembe WOWOTE uliotokea wizarani mwake.

Je hili linaweza kutokea Tanzania?
Jibu ni ndiyo ikiwa mioyo yetu itajielewa.
Picha hii ya kujiuzulu huonyesha nchi kuwa hata mkuu wa nchi huwa naye AMEKERWA.

Nawaachia WAHUSIKA wajihoji NAFSI zao!!
Wakiamua kuwa "HAMNA" na ni business as usual basi bado ni sawa tu hata hivyo I have given out my mind!/Nimetoa maoni yangu.
 
Sasa kwenye swali alilouliza mbunge na ajali uhusiano upo wapi yeye alitaka usafiri wa uhakika sio leo upo mara kesho haupo kutokana na ubovu wa engen,aya engen mbili zimenunuliwa na kufungwa abiria wamepata usafiri wa uhakika,na ajali ya jana taarifa za awali ni kutokana na kujaza kupita uwezo wake lawama kwa serikali inatoka wapi kuwa haikununua kipya mpaka kimeleta maafa? muda mwingine jaribu kuuficha ujinga ulionao hata kama ni mkazi wa ufipa.
 
Meli ilibeba watu 400.
Waliookolewa wakiwa hai ni 37.
Haya
400-37=363.

Watajigawanyaje kwenye kuzika watanzania 363?
Una weza kujibu hapo?
 
Hii ni basic ambayo inatushinda sasa kwanini tunakimbilia mambo makubwa wakati kumbe hata msingi wa vitu vidogo hatuuwezi, Hata hivyo vikubwa vitatushinda sasa.
Aisee,
Tutalalamika lakini agency husika kama SUMATRA hawana cha kutuambia.
Kazi yao nauli tu kupanga na kupokea pesa zetu.
Inauma sana!
 

Naona juhudi za kujiondoshea lawama za uzembe zinafanywa kwa juhudi kubwa sana.
Wafanyakazi kwa nini waruhusu watu wengi kiasi hicho???

Mbunge wao alisema mapema lakini ile kauli ya watoto wa kambo wanakula makombo ndio unatimia.

Kamaa jiwe alifikiri Wanaukerewe wanatakiwa waadhibiwe kwa kunyimwa maendeleo sababu tuu wamechagua upinzani basi kamwe hayuko sahihi.
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema mazishi ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya Mv.Nyerere iliyotokea Septamba 20 huko kisiwani Ukara, Ukerewe mkoani Mwanza yatakuwa ya kitaifa ambapo viongozi wakuu wa kitaifa wanatarajia kushiriki mazishi hayo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe.
Akiongea na ITV Mhandisi Kamwelwe amesema shughuli za mazishi hayo zitagharamiwa na Serikali na kwamba utaratibu kamili wa eneo yatakapofanyika mazishi hayo utatolewa baadaye.

Hata hivyo Mpaka sasa zoezi la uokoaji na uopoaji wa miili ya watu waliokuwa kwenye kivuko cha MV.Nyerere linaendelea ambapo miili 94 ya watu imeopolewa na waliookolewa wakiwa hai wanazidi 40.

Vikosi vya uokoaji mkoa wa Mwanza vimeongezewa nguvu na vikosi vya mkoa wa Mara katika eneo la tukio ili kuongeza kasi ya kuopoa miili ya watu waliopinduka na kivuko hicho.

Aidha uongozi wa wakala wa meli mkoa wa Mwanza umetambua wafanyakazi wa kivuko watano ambao wamepoteza maisha akiwemo nahodha, fundi, Karani, mlinzi na mkuu wa kivuko, Kivuko hicho kilikuwa na wafanyakazi wanane.

Mamia ya wakazi wa Ukerewe wamekusanyika nje ya kituo cha afya cha Bwisya kutambua miili iliyoopolewa kwenye ajali ya kivuko cha MV.Nyerere iliyotokea wakati wakisafiri kutoka kisiwa cha Bugorora kwenda Ukara kwenye gulio.

Mwandishi wetu aliyepiga kambi katika eneo hilo ametueleza kuwa wengi wa walioopolewa hadi sasa ni wanawake.
 
Hoja ya pili hapo chini ni yenye uzito, usikurupuke kusima paragraph moja tu
 
Very sad, kuna haja ya kuwa na imegency boats kwa ajili kusindikiza vivuko , hiii ni aibu sana, very sad once again, Mungu aweke mahali pema Roho za watz wenzetu
 
Kwa hiyo kivuko kikizama, Watanzania wakafa, serikali ya jiwe ikasitisha uokoaji na mwenyekiti wa uvccm akienda kuopoa maiti za Watanzania chama pendwa CCM kinapata credit dhidi ya CHADEMA?
Hujaelewa!

Tuishie hapo, kwasababu hujaelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…