Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Hee.., mbona unatutisha wa huku Kigamboni? ,ndio maana nasema pajengwe daraja pale, hamsikii..
Huwezi jenga daraja apo ww, uchumi Wa inchi utakufa, kama unaogopa pantoni LA pale pita darajani kule shimo LA udongo
 
Wakijiuzulu watoto wao utawalipia karo na kuwapa chakula?

Mkuu Tanzania Uongozi ni biashara kama biashara nyinginezo. Uwajibikaji ni sifuri. Ndo maana wakiteuliwa wanafanya sherehe na kuiba. Hakuna kitu kama kuhudumia wananchi.

The sad part of it, hao hao viongozi kesho watakuja kuomba kura kwa kutumia hicho kivuko kama mtaji. NA wananchi walivyo na akili nyingi watawachagua kwa kishindo!

Africa bado tuna safari ndefu sana!
 
Hakuna kujiuzulu Bashite kashindwa kujiuzulu itakuwa wa Uchukuzi mtakuwa mnamwonea jamani
 
Mbona bendera hazipepei nusu mlingoti.Kuna nini kinaendelea Tanzania.
 
Mkuu,
Hii chain inahusisha mlolongo mamlaka nyingi na hazifanyi kazi kama system.
Vitambulisho tu vya Taifa kupata ni mwaka mzima unasubiri.
Haya, hawa nao hata daftari la majina tu hawana au mpaka tumpe tenda mzungu ya kuturekodia majina ya wasafiri...?
Bado nchi hii inasafari ndefu.
 
Waziri anasema moaka sa 12jioni zoezi la uokoaji litakuwa limeshakamilika.
Maana yake kivuko kilikuwa kimemeba watu 400
Waliookolewa wakiwa hai 37
Baki
363
Maiti zilizoopolewa ni 135.

Haya 363-150=228.
Mpaka leo jioni sa 12 waziri ana uhakika wa kupata miili ya watu 228?

Ninachoona waziri kwanza angejiuzulu kwa kuleta maneno ya kipumbavu mbele ya hisia na majonzi ya watanzania
 
Jamani mlitaka sfanye nini wakati hakuna vifaa vya kuokolea muda huo?? Na sio kwamba atakuwa alijiamulia tu mwenyewe, hao wazamiaji hawana vifaa vya kufanyia kazi kwenye mwanga itakuwa gizani?? Ni aibu kwa nchi, hatuko tayari kwenye majanga!! Ya nchi kavu tu yanatushinda itakuwa ya majini??
 
Hivi, unafahamu kwamba kuna vyanzo vya uhakika vinasema kwamba abiria walokuwamo humo kwenye kivuko ni zaidi ya 200?

Na pia hakuna anaefahamu zaidi ikwamba inawezekena abiria wakawa zaidi ya 400 na wengi walokuwa wakienda gulioni?

Sasa waziri wa uchukuzi anaingiaje hapo?

Cha msingi ni kwamba kivuko ni kizima na hakikuwa na kasoro yoyote ile kwani hivi karibuni kilipata injiini mbili mpya.

Suala linaanzia kwenye msimaizi wa hicho kivuko ambae anasimamia kwamba ni tiketi ngapi ziuzwe na abiria wangapi waruhusiwe kuingia kwenye kivuko.

Hivyo usimamizi kwamba kivuko kinabeba uzito upi, namba ya abiria, mizigo na korokoro zingine si jukumu la waziri.

Hilo ni jukumu la wasimamizi wa kivuko ambao ndo wanapaswa kuwajibishwa.
 
haiwezekani kwa sababu hatuna mitizamo ya mbele. hatuna mikakati ya miaka ijayo 10, 25, 50 n.k . yaani ile tunasema vision. halafu pia tunashindana na nchi maskini tu kama kenya na uganda.
 
Mkuu,
Unaweza kuwaza hii nchi hadi jioni unywe panadol kwa kuumwa kichwa.
Uzembe tu ndo matokeo ya haya yote.
 
Hata spika wa Bunge...

Mambo yanaulizwa bungeni anaruhusu mawaziri wajibu kipumbavu, matokeo yake tuna poteza uhai wa watu wetu bure tu!
 
Waizir ajizulu Kwa kosa gan alilofanya ndivyo mnavyojidanganya mkiwa na mzee wakubadilisha gia angani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…