Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

[emoji818][emoji818][emoji818]
 
Nimesikitika sana kusoma kwamba sababu ya kivuko kupinduka ni abiria kukimbilia upande mmoja ili wawahi kushuka kivuko kikitia nanga, hivyo kupelekea kivuko kuzama. Abiria wanatakiwa kupewa elimu ya jinsi uwiano wa uzito ulivyo muhimu kwa kivuko kuelea majini.Nashauri kwenye vivuko kuwe na "vessel attendants" kama ilivyo kwa "flight attendants" kwenye ndege ambao kazi yao ni kuelekeza abiria nini cha kufanya waingiapo kivukoni, wakati gani wa kuanza kujiandaa kushuka, kuonyesha jinsi ya kuvaa boya(maybe thru a tv screen)n.k. Hii ajali insingetokea iwapo kungekuwa na watu wa kuwazuia/elekeza abiria kusubiri walipo hadi kivuko kitie nanga.
Anyway, yameshatokea. Nawapa pole wote walioguswa kwa karibu na maafa haya.
RIP marehemu wote.
 
Dalili zimeanza kuonesha, baadhi ya Wanasiasa kudai watu flani wawajibike,wajiudhuru, mawazo ambayo yako kisiasa zaidi, ni kweli ipo sababu iliyopelekea kutokea ajali hiyo mbaya, sababu zinaweza kuwa ni za uzembe wa kibinadamu,au za kitaalamu(mechanical problems), hivyo kwenda moja kwa moja kwenye(human error) tutakuwa hatuwatendei haki wataokumbwa na sakata.

Itakuwa kisiasa zaidi, hivyo kabla ya yote Mashauri uchunguzi wakina ufanyike, isije kutokea kama ile ya Muhimbili kupasua kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa, maamzi ambayo yalipelekea kuwapoteza !adakitari bingwa wa mifupa na wenye uwezo mkubwa, ambao Mara moja Botswana iliwachukua hadi leo wanafanya maajabu huko.

Ikumbukwe mfano Prof. Kinasha alieleza kwamba alikuwa ameshafanya upasuaji wa kichwa kwa watu 1,008 na wote walipona, na huyu ambaye ni bahati mbaya alikuwa wa 1,009. Sasa akahukumiwa kwa kosa moja tu !!!!

Hii ilikuwa kisiasa zaidi ikiongozwa na Prof. Mwakyusa, Sikatai kuwa uzembe ni mbaya na unaweza kugharimu maisha ya watu, jambo ambalo kamwe halikubaliki wala kuvumilika.

Lakini pia sikubaliani kuona kuwa watu wanaadhibiwa kwa mintarafu ya kisiasa, watu kutafuta kiki za kuonekana na jamii kwamba wamechukua hatua. Ajali hutokea kokote kule hata Ulaya na marekani, mfano Nyambizi ilizama, je nani aliwajibishwa?

Ndege aina ya Conctord iliua watu kibao je nani alifukuzwa kazi? Tusilione limetokea hapa kwetu, sasa ukawa muda wa wanasiasa kuishutumu Serikali nakuitaka kufukuza watumishi wake kwa madai kwamba wamefanya uzembe.

Kikubwa hapa ili Wanasiasa waoneshe kukomaa kwao wanatakiwa kuitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya sababu zilizopelekea ajali hii mbaya. Huu ni Ushauri tu na si vinginevyo.
 
Bajeti ya kununua hivo vivuko inapitishwa na wanasiasa.
Matengenezo yanategemea msukumo wa wanasiasa.
Usimamizi unategemea wataalamu na wanasiasa.
Hilo eneo lilihitaji zaidi ya kivuko kilichozama, pia ilihitaji wanasiasa wafanye maamuzi,
Vifaaa vya uokozi kwa jeshi la polisi na majeshi mengine yanahitaji wanasiasa wapitishe bajeti

Unatenganisha vipi siasa na matukio ya kizembe kama haya iwapo kina watu wanapaswa kuwajibika?

Mkuu wa Mkoa awajibike
Waziri wa uchukuzi awajibike
Polisi wawajibike kwa uzembe
SUMATRA wawajibike
 


..una uhakika gani kama hizo "injini mpya" hazikuwa na matatizo?

..na pia kivuko kuwa na "injini mpya" haimaanishi kwamba hakina matatizo ktk maeneo mengine.

..kwa maoni yangu it is too early kujua chanzo cha ajali hiyo ni nini.

..Uchunguzi huru wa kitaalamu unatakiwa kufanyika kubaini kivuko kilipatwa na matatizo gani na kupelekea kizame/kupinduka.
 
Waambie hawa hayo mawazo yako UVCCM KUSHIRIKI UOKOAJI ZIWA VICTORIA - JamiiForums
 
Kudos!
Yaani nadhani hata adui akitushambulia usiku kupitia ziwa Victoria tutasema hatuna taa ya kumlika kufanya mashambulizi.
Ina maana Mwanza hatuna Navy force yenye boti na vifaa vya uokozi?
Jeshi letu la wanamaji hawawezi ku respond kwa catastrophe kama hii, sasa tutakuwa tayari lini?
Tunasubiri South Africa watuletee wanamaji kuokoa kama walivyofanya miaka 22 iliyopita??
Yaani hatupo tayari kwa disaster yeyote.
 
Ulitaka waokoaji nao wafe kwa kukosa vifaa vya kuokolea usiku hyo ndipo ujue walikuwa na uchungu wa watu waliozama, Na wewe jitafajari umeteleza [emoji102] [emoji102]
Bwana Panzi na Jongoo, acha kubwabwaja bwabwaja kama hayawani.

Wavuvi huvua usiku.Kwa umri wako hujawahi kuona taa inayoitwa KARABAI?



Nenda kwa wavuvi waombe wakuoneshe karabai ikiwashwa usiku inakuwaje halafu rudi uje kubwabwaja.

 
Siasa ni nini? Tuanzie hapo. Nchi inaongozwa na wanasiasa, bajeti inapangwa na kupitishwa na wanasiasa, maamuzi yanafanywa na wanasiasa, utekelezaji unasimamiwa na wanasiasa. Basi kama sio siasa itumike kilimo. Hata kilimo utaambiwa ni siasa ndio maana kuna siasa ni kilimo. Wewe unatetea kitu usicho kijua!
 
..mimi nadhani tumlaumu Mbunge wa Ukerewe anayetokea chama cha Chadema.

..kwanza, alipiga kura kukataa bajeti ya wizara ya uchukuzi.

..Mbunge alitegemea serekali itatoa wapi fedha za kununua au kukarabati vivuko?

..Pili Mbunge anapata milion 58 kila mwaka kwa ajili ya mfuko wa maendeleo. Angetumia fedha hizo kukarabati kivuko huenda ajali hii isingetokea.

Cc tindo
 
Ha ha ha....
Wazee wa kugharamia mazishi.
So sad[emoji24] [emoji24]
 
"Every person is wise until when he speak or act"

Unajua umuhimu wa "priorities" if possible change your ID name to oldmind, to reflect your thoughts.
 
Mtu anasemwa live na mkuu wake lakini kagoma kujiuzulu; sasa itakuwa hili ambalo halimhusu mtu directly.

Kujiuzulu ni utamaduni wa watu waliostarabika; sisi bora kumekucha.!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…