tinkanyarwele
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 2,016
- 1,946
H
Hakuna anayemchukia RC wa Mwanza wala hakuna atakaye furahia au kufaidika na kuadhibiwa kwa mkuu Huyo. Unachopaswa kujua huwa kuna kitu kinaitwa HEKIMA au BUSARA, hata kama pasingekuwepo na njia yoyote ya kutoa msaada unapaswa kiongozi usome nyakati na hali ikoje.Taifa lote lilikuumbwa na Taharuki kila sikio LA Mtanzania mwenye wasaa wakati huo nahisi lilikuwa huko, ni bora kabisa angekaa kimya akawaondoa watu wake kimya kimya bila hata kuujulisha umma. Hapa kilichotakiwa ni busara tu na hekima ndugu yangu. Zaidi hata angeufumba umma kuwa hali ya HEWA ni mbaya kuliko kutumia kigezo cha GIZA.Nafikiri tusimlaumu mkuu wa mkoa pasi kujua vizuri sababu.kwanza tatizo limeanzia kwa wafanyakazi wa kivuko yamkini kupakia watu wengi kuzidi kiwango cha kivuko,shughuli ya uokozi inawatazama wataalamu wa majanga hayo na mkuu wa mkoa utakuta yeye hana taaluma hiyo,inawezekana giza lilipoingia wataalamu walimuomba kusitisha zoezi labda hata kwa kuepusha vifo vingine ambavyo ni vya waokozi wenyewe kwa uhaba wa vifaa yamkini vya kumulikia eneo husika na chini ya maji.zaweza kuwepo sababu nyingi hata wao na mkuu ni watu hawawezi kusitisha tu zoezi bila sababu na mle ndani kuna watu.sasa tukianza kumlazimisha Rais na kuweka uchochezi hapa wa kutamani kuona mkuu wa mkoa kafukuzwa kazi sioni kama ni sawa sana.