Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

yaani serikali nzima ya jiwe na inapaswa kujiuzulu na siyo waziri peke yake, mbunge alikwisha ona kuna shida kwenye hicho kivuko na akatoa ushauri bungeni lakini serikali ya jiwe ikapuuza, leo hii roho za watanzania zimetekea! ila ma-CCM kiama chao kitafikaa tuu!
 
Natumaini atatoa agizo hakuna kivuko kuondoka bila kujua Idadi ya waliokuwamo

Hebu tujitafakari kidogo
 
Naomba Wana Ukerewe wafanye ya Uganda kilichowapata askari kule makaburini
ccm mmekuwa mkishinda mkihubiri hamuwezi kupeleka maendeleo kwenye majimbo ya upinzani leo mnaenda kufanya nini?
Atulize makalio yake aache wenye nao walie nao waomboleze nao
ccm mmelitoa siasa za wale na sisi amini Misa mini hizi kauli zitawatafuna wote kwanguru nyie!
Mnastahili hukumu ya hasira ya Mungu!
 
Ndio imetoka hiyo..Ndugu zetu wanazikwa then tunasubiri tukio jingine...and life goes on as usual
 
Habari mbaya hizi jamani. Napiga picha pale Ukara, karibia kila familia wanamsiba, hakuna wa kwenda kumliwaza mwenzie!!!
Hasa kijiji cha Bwisya na Nyang'ombe hali ni tete. Kuna familia wamepoteza maisha watu 5 kijiji cha Nyang'ombe
 
Matukio kama haya kamwe huwezi kumuona Magufuli kwenda kuona waanga. Sijui tumepata rais wa aina gani awamu hii tsk......
 
Kuna taahira kichwa kimebonyea hataemda na akiemda anaishia kuwatusi kuwa serikali haijaleta maafa.
Alaaniwe
 
Ni aibu kwa Watanzania.
1.Eti idadi ya watu waliongia ktk kivuko hawaijui.
2.Uzito halisi wahusika hawaujui.
3.Kivuko cha watu 150 wanaingia takriban watu 400 na mizigo zaidi.
4.Vivuko vingi vina screen tvs ila zote zinapiga miziki na bongo muvi tu badala ya kutoa elimu ya usalama na jinsi ya kujiokoa.
5.Ukosefu wa vifaa vya kujiokolea km life jackets nk.
6.Vifaa duni vya kuokolea....ajabu wamepeleka mitumbwi ya kasia hata kukigeuza kivuko wameshindwa.
7.Uokoaji ulisitishwa sababu ya giza....Hivi kweli hatuna teknolojia ya kupata hata mwanga tu, watu wakapiga kazi 24hrs.
HIVI WATANZANIA TUTAJIFUNZA KWA LIPI??
 
Yani Tanzania tupo nyuma katika kila kitu.
Picha hiyo ya wanajeshi wakiokoa sio picha ya tukio la jana,lakini kwa upopoma na uvivu wa baadhi ya vyombo vyetu vya habari wameipakua mitandaoni na kuitumia kama ya jana.


Ukifuatilia Media za Kenya ndio utagundua ni jinsi gani Tanzania hakuna vyombo vya habari.
Mkuu
Picture Ile Jana Imezagaa Baadhi Yetu Tukasema JW Wapo Kazini Kumbe Hakuna Siyo Ya Tukio


Mungu Awape Pumziko La Milele
 
Jamani mlitaka sfanye nini wakati hakuna vifaa vya kuokolea muda huo?? Na sio kwamba atakuwa alijiamulia tu mwenyewe, hao wazamiaji hawana vifaa vya kufanyia kazi kwenye mwanga itakuwa gizani?? Ni aibu kwa nchi, hatuko tayari kwenye majanga!! Ya nchi kavu tu yanatushinda itakuwa ya majini??
Wangewasha hata mishumaa basi.
by the way, mita 100 toka nchi kavu siyo mbali kihivyo pale wangeweza hata kuita kivuko kingine kiende pale kikiwa kimebeba gari zenye taa za mwanga mkali au wangewahi kunyofoa hata zile taa za mwanga mkali unaosafiri mbali angani mida ya usiku kuashiria sehemu ilipo taa hiyo pana Club...
Just kwa kuunga unga tu tungefanikiwa kitu fulani
 
Back
Top Bottom