Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

W
Ww ulitaka wafanyeje acheni malalamishi....
Kiongozi kumbuka tukio Kama hili lilitokea miaka nadhani 20 iliyopita, unaweza kutuambia ni hatua au tahadhari zipi zilichukuliwa kudhibiti au hata kuokoa watu kwenye janga Kama hili?!
 
Dah hii nchi ni ngumu sana.
"Et mkata tiketi alizama kwenye maji pamoja ma mashine aliyokatia tiketi kwahio hatuwezi kujua idadi kamili iliyokuwemo kwenye kivuko"
Carcinoma, Ndio wamesema hivyo !!??. taarifa za abiria wanaosafiri zinapaswa kubakia ofisini na sio kuenda nazo kwenye Kivuko/Meli, imekuwa hiace hiyo ya mlalahoi, hii si ni serikali kabisa ambayo mimi nilidhani inajielewa, ambayo kimsingi inapaswa kuwa na ofisi stationary, kwa hiyo na mapato yote yamezama kwenye ziwa ?.
 
Hapa mkuu nimekuelewa kwa herufi kubwa
 
Mkuu paschal Mayalla leo umeandika kwa mzuka wa Baba yako.
Keep it up this spirit.
 
May the love and mercy of our Lord be bestowed upon to you people of Ukerewe and your family during this unfortunate time. May God rest (dead one) their heart in eternal repose. My most sincere condolences.
 
Hilo la kukimbilia mbele ni kweli linasababisha Inbalance but lazima kuna sababu nyingine kubwa, taarifa zilizopo (japokuwa sijui kama ni za kweli) ni kwamba kulikuwa na abiria kiasi cha 400 na uwezo wa kivuko ni abiria 100, Serikali hii ambayo jeshi lake la polisi huwa linatumia Intelligensia ya hali ya juu kufanya maamuzi ya kuzuia mikutano ya wapinzani inashindwaje kuona udhaifu huu ?, hii ni serikali mzigo, wadau wanuliza hivi angekuwemo mama yake na JPM wangesitisha uokoaji jana ?
 
Nimesoma kwa kina andiko lako Pascal Mayalla, naamini mtu yeyote aliyesoma shule na hiyo elimu ikamstaarabisha hawezi kukubaliana na hoja yako kwamba eti watu hawawajibiki kwa makosa ambayo ama ni moja kwa moja wamehusika au ni kwa migongo ya wsnawaongoza, Tumeshuhudia, akina Tibaijuka. Muhongo, Kitwanga. Nape, Nchemba, Je hao walipowajibika ilikuwa enzi ya Baba wa Taifa hili? Hasira yako hakika inatokana na ndugu yako kuwajibika ? Au inatokana na chuki yako binafsi? Binafsi nakufahamu sana pengine kuliko hata unavyojifahamu wewe. Kila Mara mandiko yako huwa ni ant system, lakini unasahau kuwa Taifa hili limekusomesha , linakupa fursa ya kujivinjari mitandaoni kwa gharama nafuu kabisa, kuwa na shukrani kwa Serikali yako. Siyo kila siku kuibeza.
 
Majeneza tayari
Majeneza ya kiwango,
Majeneza yapo ya ziada.
Kauli nyingine ukizisikia uafiwa upya.
 
Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama jana mchana Septemba 20, 2018 imefikia 126 huku uokoaji ukiendelea.


Akizungumza wakati akihojiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) leo saa 10:30 jioni, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issack Kamwelwe amesema miili 36 tayari imetambuliwa na ndugu na jamaa wakati kazi ya kuitambua iliyosalia ikiendelea.



Amesema hadi leo mchana waokoaji walikuwa wameipata miili 76 na waliporejea tena kuanzia saa 10 jioni walifanikiwa kupata mingine na kufanya idadi yake ifikie 126.
Soma Zaidi: Lowassa, CUF wawalilia waliofariki dunia kuzama kwa MV Nyerere



Leo saa 5 asubuhi, ilielezwa kuwa miili iliyokuwa imepatikana hadi muda huo ilikuwa 42, jana ilipatikana 44 na kufanya idadi yake kufikia 86, baadaye mchana kuongezeka hadi 94.
Waziri huyo ameahidi kutoa taarifa nyingine saa 12 jioni ambayo itatoa mwelekeo halisi kama kazi ya kuopoa miili mingine itaendelea au kuahirishwa hadi kesho.



“Bado kazi ya kusaka miili zaidi inaendelea. Nitazungumza tena baadaye jioni na tutaeleza kama tunaweza kuendelea na kazi hii au itatubidi kuahirisha hadi kesho,” amesema.



Soma Zaidi: VIDEO: Mbatia: Ajali ya MV Nyerere ni ya kujitakia



Hata hivyo, leo mchana Kamwelwe wakati akihojiwa na TBC amesema uokoaji utasitishwa saa 12 jioni.
Kuhusu uokoaji, amesema wazamiaji hawajakumbana na ugumu wowote zaidi ya kukuta mizigo ambayo hulazimika kuitoa kwanza ili waweze kutoa miili.



Kamwelwe amesema kila wakati wamekuwa wakiwasiliana na na Rais John Magufuli ambaye amekuwa akifuatilia tukio hilo kwa ukaribu mkubwa.
“Mheshimiwa Rais macho yake yote yako huku na kila mara nimekuwa nikiwasiliana naye,” amesema.
 
Hivi yule aliyesema kwamba zoezi la uokoaji limesimama na "wanakwenda zao kulala kwa kuwa kuna giza tororo" bado yupo ofisini? I am sure kama baba, mama au mke wake angekuwa ndani ya hiyo ferry, asingetamka huo utumbo. Shithole indeed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…