Kwani hii ndio ajali ya kwanza ya uzembe hadi watu wawajibike?!. MV Bukoba aliwajibika nani?. MV Spice Island amewajibika nani?.
Kifo cha Daudi Mwangosi, amewajibika nani?!. .
Kifo cha Akwiline amewajibika nani?!
Mpaka watu wangapi wafe ndipo watu wawajibike?.
Utamaduni wa kuwajibika, umekufa na Nyerere!,
Mimi ni muhanga wa uwajibikaji, wakati wa Nyerere, baba yangu, Mzee Andrew Mayalla, ndiye alikuwa RSO wa Mwanza, kuna mahabusu wawili, Masanja Makulla Mazengenuka na Issack Mwanamkoboku, walikufa mikonani mwa polisi katika mahojiano baada ya kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya vikogwe.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hasssan Mwinyi alijiuzulu!,
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Mzena, alijiuzulu!,
Mkuu wa jeshi la Polisi, IGP, Pundugu alijiuzulu!.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Peter Kisumo, alijiuzulu!
RSO wa Mwanza, RPC, RSO na OCD kwanza walistaafishwa kwa manufaa ya umma, kisha wakafunguliwa mashitaka ya Kesi ya Mauaji Mwanza!.
Uwajibikaji ni enzi za Nyerere!.
Ingekuwa Nyerere yupo, hata mtu aliyeuza Nyumba za serikali kwa kuwagawia hata vimada wake, hadi kuuza nyumba za line police!, asingethubutu hata kuwaza kuchukua fomu!. Mtu amelitia taifa hasara ya kulipishwa fudia kibao kwa maamuzi tuu ya papara!.Mtu amenunua kivuko mtumba kwa mabilioni ya shilingi, halafu hakikufanya kazi!.
Kuwajibika kumekwenda na Nyerere, sasa ni zama za kupeana pole tuu!.
Poleni kwa yote!.
P.