Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

John alikuwa huku juzi juzi kuhitimisha kafara hii.Mkono wa John huu sio mtu mwingine. Hii yote ni ili aweze kufuata nyayo za Paulo na Kaguta kushikiria kiti kwa miaka mingi.
 
Kuna taa zinaitwa spotlight, kwa taa moja inaweza ika cover mita 200 mwanga kwa hiyo zingepatikana taa 3 kazi ingeendelea, ninauzoefu na hivi vitu msitetee madudu, kweru mto na kweru mkungu taa kama hizo haziwezi kukosekana, Nina uhakika kila kambi ya uvuvi hiyo taa ipo
 
Fernando Jr, Mimi sielewi ni kitu gani kiliwashinda hawa serikali kuagiza Vivuko hata vitatu ambavyo viko jirani hapo mwanza kuja kusaidia uokoaji tangu saa nane mchana Mv Nyerere ilipozama, halafu usiku sa mbili tunaambiwa zoezi la uokoaji limesimsmishwa sababu ya giza, uzuri ni kwamba pale mahali ni karibu kabisa na nci kavu )tumeambiwa si zaidi ya mita 100, Mkuu wa mkoa na timu yake wanaamua kwenda kulala ili waje kesho yake asubuhi kuendelea na uokoaji, huo hauwezi kuitwa uokoaji bali uopoaji wa miili ya marehemu, kwani nina uhakika wengi watakuwa wameendelea kufa usiku
 
Idadi ya abiria kutojulikana ndo inanisikitisha inamaana ticket hazijulikani zilikatwa ngapi na sio za EFD kweli watu bado watakua wanapiga tu.
 

Mv Bukoba iliwezaje kusafiri usiku kucha tokea Bukoba ikaja kupindukia Mwanza kukiwa kushakucha? tatizo ni kujitia ujuaji kwa kila kitu, jana nilieleza humu sababu pekee ya meli kupinduka ni kukosa stability, hii husababishwa na maofisa wa meli kuzidisha mzigo, kumbuka chombo cha majini kinapoundwa huwekewa mstari wa ukomo wa mzigo ili kuwawezesha watumiaji na wakaguzi kubaini uzito stahiki kabla ya kuanza safari.


Meli inapoundwa huwekewa matanki ya maji kwa chini ili yaipe stability, kutokana na tamaa maafisa wanapoona wamezidisha mzigo na ili wasishtukiwe hupunguza maji kwenye matanki ili meli ipande juu mstari uonekane ili waruhusiwe kuondoka, kitendo hiki hupoteza stability ya meli,mzigo ukizidi tu upande mmoja meli itaoverturn sababu chini ni kwepesi kuliko juu, meli inapoondoka watu huwa wametulia sehemu zao na hivyo mzigo huwa evenly distributed, meli inapokaribia kutua nanga watu hurundikana sehemu moja hivyo meli kupinduka.
 
Tangu jana walivyositisha uokoaji wakasema wametoa majeruhi 37 ambao walikuwa na hali mbaya, sijui na sijasikia kama ameshapatikana majeruhi mwingine
 
Umeteleza kidogo mkuu muhanga alikuwa baba yako sio wewe
 

..my friend, it is pre-mature kusema with confidence kuwa kivuko kimezama kwa sababu moja tu -- kuzidisha abiria na mizigo.

..unaposema wasimamizi wa kivuko wamekufa, hizo taarifa zimetoka wapi? kwa uelewa wangu kuna survivors ktk ajali hii.

..kwa msingi huo walionusurika wanatakiwa kwanza watambuliwe, wapewe ushauri nasaha, na wahojiwe kuhusu safari yao na tukio zima la ajali.

.."vital evidence" kwa upande wangu ni zaidi ya majina na idadi ya watu, na kiwango cha mizigo kwenye kivuko. "Vital evidence" nyingine ni ripoti za matengenezo na ufundi za kivuko, pamoja na mawasiliano ya waendesha kivuko siku ya tukio.
 

Mungu hadhihakiwi!Waliosababisha kuzama kwa kivuko Watanzania wanawajua na dunia nzima inawajua!
Mbunge wa UK kutoka CHADEMA alitimiza wajibu wake kwa KUFIKISHA BUNGENI KILIO CHA WANA UKEREWE KUWA KIVUKO HICHO HAKIKUWA SALAMA KWA WAPIGA KURA WAKE!!!MLITAKA AFANYEJE ZAIDI YA HAPO?

Tatizo ni Serikali ya Magufuli na CCM yake kupuuza HOJA ZA MBUNGE KWA VILE TU NI KUTOKA UPINZANI...!!Hivi nani asiyejua kuwa Rais Magufuli AMESHATOA MAELEKEZO YA KUTOPELEKA FEDHA KWENYE MAJIMBO YA UPINZANI???Huku ni kuwabagua Watz kwa ITIKADI ZA KISIASA AMBAYO NI DHAMBI YA UBAGUZI....!!

Baba wa Taifa aliwahi kusema,""UKIANZA DHAMBI YA UBAGUZI HUWEZI KUIACHA NI SAWA NA KULA NYAMA YA MTU...NA DHAMBI HIYO ITAWATAFUNA....NA ACHA IWATAFUNE''.
 
Unataka dunia ijue kuwa kivuko kilibeba watu 500 zaidi ya uwezo wake? Lakini pia dunia itajuaje kuwa tunaweza kuopoa miili ya marehemu kwa haraka kama hatutamaliza leo! Broh usiwe siriaz sana utakufa kwa stress, fata namna nchi inavoenda, ikienda kibwege nawewe kuwa bwege, ikishtuka nawewe shtuka.
 
Imbalance ya watu ambao ni uwezo wa kivuko haiwezi kipindua... DESIGNER WANAWEKAGA NA POINT LOAD AT ONE LOCATION... Otherwise Kungekuwa na matangazo ya kutojaa sehemu moja... HUWEZI DESIGN KITU HALAFU UKATEGEMEA WATU WASIJAE SEHEMU MOJA NA HUWAAMBII... and you dont have control ya wapi wakae na wenye uzito gani...

KIFUPI ILIBEBA KULIKO UWEZO WAKE NA WENGI WAKAJAA SEHEMU MOJA...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…