Nimesoma kwa kina andiko lako Pascal Mayalla, naamini mtu yeyote aliyesoma shule na hiyo elimu ikamstaarabisha hawezi kukubaliana na hoja yako kwamba eti watu hawawajibiki kwa makosa ambayo ama ni moja kwa moja wamehusika au ni kwa migongo ya wsnawaongoza, Tumeshuhudia, akina Tibaijuka. Muhongo, Kitwanga. Nape, Nchemba, Je hao walipowajibika ilikuwa enzi ya Baba wa Taifa hili? Hasira yako hakika inatokana na ndugu yako kuwajibika ? Au inatokana na chuki yako binafsi? Binafsi nakufahamu sana pengine kuliko hata unavyojifahamu wewe. Kila Mara mandiko yako huwa ni ant system, lakini unasahau kuwa Taifa hili limekusomesha , linakupa fursa ya kujivinjari mitandaoni kwa gharama nafuu kabisa, kuwa na shukrani kwa Serikali yako. Siyo kila siku kuibeza.