Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kudos!
Yaani nadhani hata adui akitushambulia usiku kupitia ziwa Victoria tutasema hatuna taa ya kumlika kufanya mashambulizi.
Ina maana Mwanza hatuna Navy force yenye boti na vifaa vya uokozi?
Jeshi letu la wanamaji hawawezi ku respond kwa catastrophe kama hii, sasa tutakuwa tayari lini?
Tunasubiri South Africa watuletee wanamaji kuokoa kama walivyofanya miaka 22 iliyopita??
Yaani hatupo tayari kwa disaster yeyote.
Yaani tunasikitisha kama taifa na bahati mbaya sana hatua zozote za tahadhari huwa ni za muda mfupi tu baadaye zinaisha mfano baada ya ile meli iliyokuwa inaenda zenji kuzama kuna baadhi ya vitu vilivyofanyika kama kutoa elimu kupitia TBC na vyombo mbalimbali vya habari juu ya nini cha kufanya ikitokea ajali pamoja na kuvaa life jacket lkn baada ya muda hatukuoni tena, la pili baada ya chuo cha Kenya kuvamiwa na alshabab kuna hatua za kiusalama zilichukuliwa kwenye baadhi ya vyuo za ukaguzi kwa wanaoingia na kutoka na tahadhari kadhaa lkn Leo hazipo unaweza kuingia na kutoka bila kuulizwa chochote

Yaani mipango yetu siyo endelevu kana kwamba janga likitokea ndiyo halirudi tena nadhani ni wakati viongozi wakabadilika na kuweka mipango ya kudumu ya namna ya kukabiliana na majanga na siyo kuwa na mipango ya muda mfupi tu maana tunapoteza watanzania wenzetu wengi sana watu 100+ ni wengi sanaa
 
Pia alie kuwa kiongozi wa bunge siku mbunge wa Ukerewe alipo uliza swali akajibiwa utumbo kwa sababu za ijinga na ushabiki wa kipimbavu wa wabunge wa Ccm nae aachie ngazi.
Ki uhalisia Ccm na serikali yake wanatakiwa kulaaniwa kwa hili tatizo
Kila ALIYESHIRIKI,kamaule mfano wako wa mbunge kujibiwa kipumbavu katika hali ya kishabiki aliyekuwa kiongozi naye pia AWAJIBISHWE.
Nchi hii si nchi ya CHAMA fulani bali ni Watanzainia wote pasipo kujali vyama vyao.
Nakubalianan nawe kuwa kila mtu na msalaba wake.
 
Dalili zimeanza kuonesha, baadhi ya Wanasiasa kudai watu flani wawajibike,wajiudhuru, mawazo ambayo yako kisiasa zaidi, ni kweli ipo sababu iliyopelekea kutokea ajali hiyo mbaya, sababu zinaweza kuwa ni za uzembe wa kibinadamu,au za kitaalamu(mechanical problems), hivyo kwenda moja kwa moja kwenye(human error) tutakuwa hatuwatendei haki wataokumbwa na sakata. Itakuwa kisiasa zaidi, hivyo kabla ya yote Mashauri uchunguzi wakina ufanyike, isije kutokea kama ile ya Muhimbili kupasua kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa, maamzi ambayo yalipelekea kuwapoteza !adakitari bingwa wa mifupa na wenye uwezo mkubwa, ambao Mara moja Botswana iliwachukua hadi leo wanafanya maajabu huko. Ikumbukwe mfano Prof. Kinasha alieleza kwamba alikuwa ameshafanya upasuaji wa kichwa kwa watu 1,008 na wote walipona, na huyu ambaye ni bahati mbaya alikuwa wa 1,009. Sasa akahukumiwa kwa kosa moja tu !!!! Hii ilikuwa kisiasa zaidi ikiongozwa na Prof. Mwakyusa, Sikatai kuwa uzembe ni mbaya na unaweza kugharimu maisha ya watu, jambo ambalo kamwe halikubaliki wala kuvumilika. Lakini pia sikubaliani kuona kuwa watu wanaadhibiwa kwa mintarafu ya kisiasa, watu kutafuta kiki za kuonekana na jamii kwamba wamechukua hatua. Ajali hutokea kokote kule hata Ulaya na marekani, mfano Nyambizi ilizama, je nani aliwajibishwa? Ndege aina ya Conctord iliua watu kibao je nani alifukuzwa kazi? Tusilione limetokea hapa kwetu, sasa ukawa muda wa wanasiasa kuishutumu Serikali nakuitaka kufukuza watumishi wake kwa madai kwamba wamefanya uzembe. Kikubwa hapa ili Wanasiasa waoneshe kukomaa kwao wanatakiwa kuitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya sababu zilizopelekea ajali hii mbaya. Huu ni Ushauri tu na si vinginevyo.
Sii ajabu ukakuta Maccm wamevaa ma nhuo yao ya kijani kwenye uokoaji ili hali mbunge alisha piga kelele kuhusu hili jambo akajibiwa walivyo weza kujibu.. Mungu ana waona Ccm
 
Wangewasha hata mishumaa basi.
by the way, mita 100 toka nchi kavu siyo mbali kihivyo pale wangeweza hata kuita kivuko kingine kiende pale kikiwa kimebeba gari zenye taa za mwanga mkali au wangewahi kunyofoa hata zile taa za mwanga mkali unaosafiri mbali angani mida ya usiku kuashiria sehemu ilipo taa hiyo pana Club...
Just kwa kuunga unga tu tungefanikiwa kitu fulani
Ni sawa ila unapokuwa na mfumo ambao watu wake hawajajiandaa na majanga, pindi linapotokea hata akili ya kujiongeza hawana!! Na tatizo kubwa pia ni kutegemea vivuko vya abiria ndio vitumike, kwani vingi viko mwanza na kutoka mwanza hadi huko ni parefu na vingi unakuta viko kwenye safari zake!!! Ila waambiwe kuna magendo ziwani, utaziona zile boti za kwenye movie
 
Eti macho yake yako Hulu ..!?
Mpka leo ningetarajia ameshafika huko
 
Ni kawaida maraisi kutoa pole

Lakini kwanini hatujifunzi kutokana na makosa
Doria kwenye maji hakuna? Na uokoaji hakuna
Ajali za barabara zisizoisha na majini tukio linatokea hatujiulizi tunakosea wapi na hatua stahiki hazifuatwi

Hao waliofiwa hata wapewe nini haitasaidia
Maadamu bado wasimamizi wetu wapo ofisini bila kufukuzwa au kujiuzuru bado napinga kuwa our system stinks
 
Hakuna kujiuzulu Bashite kashindwa kujiuzulu itakuwa wa Uchukuzi mtakuwa mnamwonea jamani
Hapa hamna cha Bashite ama ndugu ya Bashite tunachokizungumzia hapa ni KIKUU sana kuliko hicho unachokizungimza.
Haya ni MAISHA ya watu mamia WALIOKUFA sababu ya UZEMBE!.
Watu wakae ofisini wakifanya nini?
 
Ilizama Mv Bukoba,Spice Island na vyombo vingine vingi,mawaziri hawakujiuzulu au kufukuzwa kazi,kwani wafukuzwe sasa?.
Tusitafute short cut,tatizo la ajari za majini ni kubwa mno linataka ufumbuzi wa kudumu.
Ukiangalia kwa undani linaanzia ubora wa chombo tokea michoro yake,usimamizi wa ujenzi wa chombo,utoaji wa leseni ya chombo na leseni za waendesha chombo.
Hili jambo ni la kitaalamu zaidi,tuwape wataalamu wenye vigezo na uzoefu uliotukuka walishughulikie kwa kina.
 
Back
Top Bottom