Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issack Kamwelwe amesema uokoaji wa miili ya waliofariki dunia baada ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere utakamilika leo Septemba 21, 2018 kabla ya saa 12 jioni.



Amesema hata majeneza kwa ajili ya mazishi ya waliofariki dunia yameshaandaliwa na yapo tayari.
Kamwelwe ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akihojiwa na kituo cha Utangazaji cha Taifa (TBC), akiwa eneo la tukio Kisiwa cha Ukara wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.



Soma Zaidi: VIDEO: Mbatia: Ajali ya MV Nyerere ni ya kujitakia
Amesema uwepo wa majeneza hayo unaashiria kuwa shughuli ya mazishi itafanyika kadri itakavyowezekana.
“Hapa leo hatulali maana nimekuja na timu nzima jeshi lipo hapa, polisi wapo hapa na masanduku pia,”amesema.



“Shughuli za mazishi zitafanywa kwa kufuata taratibu zote ikiwemo kuzingatia mila na desturi na kwa kuzingatia taratibu za kidini kwa vile viongozi wote wa dini wapo.”



Alipoulizwa kuhusu sababu za kuzama kwa kivuko hicho, Kamwelwe amesema hawezi kulielezea jambo hilo kwa maelezo kuwa jambo hilo litafahamika baadaye.
Hivi unasemaje eti zoezi la uokoaji litakamilika leo tarehe 21 jioni!!?

Inamaana milii yote ikifika hiyo saa 12 itakuwa imeshapatikana !??

Au wanafikri hili zoezi ni kama jinsi wanavyoiba kura na kusema zoezi la uhesabuji litakamilka saa12 jioni!?

Pathetics.
 
Mataifa makubwa na maskin kijografia ni shida tu bora tufanye partition kwa mara nyingine.
 
Kwani hii ndio ajali ya kwanza ya uzembe hadi watu wawajibike?!. MV Bukoba aliwajibika nani?. MV Spice Island amewajibika nani?.
Kifo cha Daudi Mwangosi, amewajibika nani?!. .
Kifo cha Akwiline amewajibika nani?!
Mpaka watu wangapi wafe ndipo watu wawajibike?.

Utamaduni wa kuwajibika, umekufa na Nyerere!,
Mimi ni muhanga wa uwajibikaji, wakati wa Nyerere, baba yangu, Mzee Andrew Mayalla, ndiye alikuwa RSO wa Mwanza, kuna mahabusu wawili, Masanja Makulla Mazengenuka na Issack Mwanamkoboku, walikufa mikonani mwa polisi katika mahojiano baada ya kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya vikogwe.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hasssan Mwinyi alijiuzulu!,
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Mzena, alijiuzulu!,
Mkuu wa jeshi la Polisi, IGP, Pundugu alijiuzulu!.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Peter Kisumo, alijiuzulu!
RSO wa Mwanza, RPC, RSO na OCD kwanza walistaafishwa kwa manufaa ya umma, kisha wakafunguliwa mashitaka ya Kesi ya Mauaji Mwanza!.

Uwajibikaji ni enzi za Nyerere!.

Ingekuwa Nyerere yupo, hata mtu aliyeuza Nyumba za serikali kwa kuwagawia hata vimada wake, hadi kuuza nyumba za line police!, asingethubutu hata kuwaza kuchukua fomu!. Mtu amelitia taifa hasara ya kulipishwa fudia kibao kwa maamuzi tuu ya papara!.Mtu amenunua kivuko mtumba kwa mabilioni ya shilingi, halafu hakikufanya kazi!.

Kuwajibika kumekwenda na Nyerere, sasa ni zama za kupeana pole tuu!.

Poleni kwa yote!.

P.
Mkuu upo? Nimekusifu leo kwa "biased neutrallity" Naanza kukuelewa!
 
Jinga kuu wewe walahi!
Leo mpaka koo litakukauka kwa maana tokea asubuhi unajitahidi kutetea mabwana zako [emoji23][emoji23][emoji23]ila sijui hata kama wameshakupa jelo ukanywe maji!!?
 
Angalo hata helicopter ingeshusha maboya chap,wengi wangenusurika!!
 
Ndo mlisubiri mazishi na rambirambi.
Mpaka siku kiongozi azame ziwani ndo mamlaka zitashtuka.
Kweli mnatuletea mambo ya mzaha Ndugu zetu wamepotea.
Hata orodha ya majina kama kwenye mabasi inajulikana leo kivuko hata kuandika majina kwa daftari ya shillingi 500 na kuiacha bandarini napo tunasubiri nchi marafiki /wahisani?
Miaka 22 iliyopita watu hawakujulika wengi kwenye ile meli na leo ni yale yale, tunajifunza kwenye kama Taifa? Kweli tupo serious?
SUMATRA hili sio jukumu lenu? Bandari mpo? Wizara ya uchukuzi je?
Aliyekuwa anaandika majina nae amezama...[emoji24] [emoji24]
 
Sorry mkuu hich kivukoo kulikuwa na watu wangap... Kuna sehemu nmesoma nmeona n 500 vp Kuna ukwel juu ya hilo. . Afu had zoezi linactishwa inamaana watu waliopatikana+ miili n 81 ko tuna watu 390+ hatujui walipo...,au Kuna wengine wameogelea had nchi kavu?
Ndugu hesabu zilikupiga chenga kama Mimi!?
 
Hakuna
Na hii ndo inaleta shida sana hapa nchini,mtu kuhitaji kudanganywa na si kupewa ukweli,kiasi mmezoea kudanganya na kudanganywa ndo imekua sehemu ya maisha yetu,kimefika kipindi cha ukweli na uwazi nao hamuutaki na mnashauli mkuu wa mkoa angedanganya eti hiyo ndiyo hekima na busara.kweli uongozi wa sasa una kazi kubwa sana kueleweka kwa wananchi.ndiyo maana wananchi wengi ukipita vijiweni na sehemu za kazi wanawaza kauli ya kuwalidhisha ili wafurahi hata kama ni uongo.wakipewa ukweli kwa kua ni mchungu wanauchukia,mkuu wa mkoa yupo sawa kabisa kusema ukweli wa kilichopo kuliko kudanganya
Hakuna ukweli wowote ni upuuzi tu, hivi kama wewe ndugu zako wangekuwa mle ukasikia kauli kama hiyo ungesema uongozi ni mzuri kwakuwa umesema ukweli? Unacheza na uhai wa mtu, yaani unadiriki kwenda kulala wakati mtoto, ndugu au jamaa yako unajua yumo majini hata kama ni mfu tayari ujasiri wa kusitisha zoezi unaotoa wapi? Alafu bila haibu eti GIZA!!!!!! Hebu acha utani UHAI WA MTU HAUNA MBADALA.
 
Gharama zakurudia uchaguzi wa diwani ni 200-250 mil. wakati ubunge ni 2-3 bil. lakini hapohapo RC na washauri wake wameshindwa kufanya hata harambee ya vifaa vya uokoaji na mwanga.

Makonda ana mapungufu yake lakini kwenye hili tungeshuhudia ubunifu wake mkubwa.Mongella kafanya ukatili sana kwa uamuzi wake wa jana.
 
Back
Top Bottom