Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kwa ufupi
Mbunge huyo wa Ukerewe (Chadema), Joseph Mkundi alizungumza bungeni na kuiomba Serikali kukitazama kivuko hicho kwa jicho la pili kwa kuwa kimekuwa na matatizo, kuonya kuwa huenda kuna siku kikazama ikiwa hatua zozote hazitachukuliwa

Dar es Salaam. Unaweza kusema yaliyotabiriwa na mbunge wa Ukerewe (Chadema), Joseph Mkundi juu ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere yametimia.

Ndivyo unavyoweza kusema baada ya jana mchana kivuko hicho kuzama katika Ziwa Victoria mita 50 kabla ya kutia nanga huku abiria 37 waliokuwa kwenye kivuko hicho wakifariki dunia hadi zoezi la uokoaji lilipositishwa jana jioni.

Kivuko hicho kilichokuwa kikitokea katika Kisiwa cha Bugolora kuelekea Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, kinadaiwa kilikuwa kimepakia zaidi ya abiria 100, wengi wakiwa wanaelekea kwenye gulio.

Katika moja ya swali alilouliza bungeni hivi karibuni, Mkundi alitaka kupata kauli ya Serikali jinsi itakavyoshughulikia kivuko hicho ili kisije kusababisha maafa.

Video inayomuonyesha mbunge huyo akiuliza swali hilo bungeni ilianza kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii jana jioni baada ya kivuko hicho kuzama.

“Naomba kupata kauli ya Serikali, ni suala ambalo tumekuwa tunalishughulikia mara kwa mara, tuna kivuko kinachounganisha Ukerewe na kisiwa cha Ukara, kivuko hiki kinahudumia watu zaidi ya 50,000,” amesema.

“Kimekuwa kinaleta shida mara kwa mara na nimekuwa nawasiliana na wizara, sipendi siku moja tuje hapa kuomba rambirambi kwa sababu ya wananchi waliozama katika kivuko kile.”
 
Nina sababu ya msingi kutosikiliza. huwezi kusikiliza kichaa (amejisema yeye na wala si mimi) and make any sense from his/her words! Ni hiyo tu sababu yangu.
Sawa uko sahihi ila Alikuuliza nani kama unasikiliza au laa au kuna mahali paliandikwa kasikilize mpaka uje na povu?
 
Msithubutu kabisa.Kama haina kazi nipigie nikuelekeze uifanyie nini hiyo hela.Kwani yeye ndo amekizamisha Bwana?
Wewe ndio wakupigie simu uwaelekeze pa kuzipeleka , du labda mwenye korosho mwenzio ndio akupigie
 
Bwashee mwambie Mangi Mtuhuru amechemka, au kwa kuwa Kule upepo wa kaskazi hauvumi!
hapana, hajachemka mbona Mkuu wa nchi hajaenda. yeye ndiyo mwenye mji hawa wengine ni wapishi tu kama alivyosema Nyerere. Hili ni tukio kubwa inabidi aende kuliko kufungua zahanati, barabara etc kama anavyofanya kila leo!
 
Hakuna sababu ya kuunda tume...
Kama uzembe umeshafanyika hyo ndy shida ya Hao Wasimamizi wa vivuko kufanya kzi kwa mazoea!

Ova
 
Wakati mzee Mwinyi anajiuzulu alikuwa kwenye zile mahabusu walizojaza watu hadi wakafa ? Kwanini Mzee alijiuzulu badala ya RPC ,OCD nk ?
 
Labda kwa mtutu
Hela ya mwenye roho ya korosho , Mungu haipokei , kwa hiyo wewe usichange , hela yako tumia utakavyo , na wengine wenye roho
kama yako wakutumie wewe ukanywee mbege.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…