Ndugu wanabodi:
Hivi sisi Watanzania nano katuloga? TBC na vyombo binafsi vimeshindwa kujiunga mubashara kwenye shughuli ya uopoaji maiti lakini hats kupiga nyimbo za maombolezo imeshindikana kweli?
Nimesema shughuli ya uopoaji kwa sababu serikali ingekuwa serious na maisha ya Watanzania wenzetu ingepeleka jenereta jana ili shughuli ya uokoaji iendelee Jana usiku.
Watanzania zaidi ya 126 ni msiba mkubwa wa taifa lakini radio na luninga ya taifa wameshindwa kujiunga mubashara hatua kwa hatua badala yake wanaendelea na mambo yao yasio na maslahi kwa Taifa.
Naamin kwa Wazungu habari ingekuwa ndio hiyo kuwa mubashara muda wote kwa kila kituo cha luninga na redio.Na wasingekubali kusitisha shughuli ya uokoaji eti kisa giza
Tumeshindwa kuthamini uhai wa wenzetu, kweli ngozi nyeusi ni wabinafsi haijapata kutokea