Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Dah...ungeshauri wafanye nini chief? Ukirejea vifaa na utaalam walio nao..[emoji41]

hahahahhaa karne ya 21 na miaka zaidi ya 50 ya uhuru unaongelea utaalamu na vifaa?? haiwezi kuwa excuse hiyo ni uzembe huo..
 
Kwanza nitoe pole kwa wote waliopatwa na janga ya ajali ya kivuko ukerewe. Mungu awatie nguvu ndio maisha haya.
Watu wamepoteza maisha kwa uzembe wa wahusika hasa serikali ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa kivuko. Hili ni tatizo ambalo lingeweza kuzuiliwa mapema endapo hatua za mapema zingechukuliwa.
Kutokana na mfumo mbaya wa takwimu na ubebaji wa idadi kubwa ya watu kwenye vyombo vyetu vya usafiri, ajali hii inawezq ikasababisha misiba yenye mashaka na huzuni kwa watu kutokana na kutokuwa na idadi kamili ya wahanga wa ajali hii hivyo kuna uwezekano mkubwa wa watu kupotelea majini pasipo kujulikana walipo na serikali isijue.
TUTEGEMEE idadi ya wahanga waajali kutokana na miili itakayopatikana tu watakaopotea haitajulikana.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Nimemsikia mkuu wa wilaya ya akisema kupitia kipindi cha BBC Dira ya Dunia kwamba kivuko kilichopinduka na kuzama kilikuwa na zaidi ya abiria 400 wakati uwezo wake ni abiria 100. Kama takwimu hizi ni za kweli basi nategemea utenguzi wa vigogo kadhaa pale wizarani asap. Aisha waziri anaweza kujifunza jambo Jena la kufanya kutoka kwa mpendwa mstaafu Mwinyi.
Source BBC Dira ya Dunia!
 
Sio kila sehemu muweke siasa na hoja za kipumbavu kama hizi, mnajifanya kujua kila jambo end of the day mwaonekana ka mitaa.hiratu, unajua kinachosababisha marine vessel hasa melii nini?
Kunapokosekana uwiano wa uzito kati ya mzigo wa chini (watertanks) na ule wa juu (abiria na mizigo) hiyo ndo huwa sababu kubwa ya meli kuoverturn hata kama ni mpya.

Maafisa wa meli wanapozidisha mzigo hupunguza maji ya chini ili kudanganya wakaguzi...hiki ndicho kilichotokea hata kwa Mv Bukoba, unapopunguza mzigo wa chii na kuzidisha wa juu nadhani unajua nini kitatokea endapo ukiweka chupa ya dasani yenye maji nusu ndani ya besini na ukafunga kitu kizito juu ya chupa chenye uzito kuzidi hayo maji nusu. Ni Rais aliyewatuma kuover load? hizi kejeri na dhihaka dhidi ya Rais zinatoka wapi?
Kwahiyo tangia hiyo meli ianze kufanya safari miaka yote hiyo leo ndio wamepunguza maji kwenye hayo MABOYA ya chini?
 
Ngoma imezama mchanaaa yaan mchana kweupeeee... Ila mpaka wanasitisha zoezi ilo usiku huu only 44 watu...

Ivi jamaa ziko serious kweli au wanazengua???
Ikiwa wewe ndiwe rais wa nchi unapataje usingizi ikiwa raia wako wako chini ya maji kwa usiku mzima?. Waafrika Mungu aturehemu sana. Huu uongozi wa kupitia *** wa *** utalimaliza bara la Africa. Tunakosa utu alafu bila ya aibu li mtu linasema wazi wazi uokozi mpaka kesho hivi tuna akili kweli?. Alafu kesho limtu limoja litakuja na mitungi ya gas ya uchomeleaji kutoboa hiyo meli ili watu watokemo kupitia juu.
 
Hoja yako nzuri ila inaelekea bado hatujajifunza kutokana na ajali zilizopita maana ajali kama hiyo ilitokea miaka 22 iliyopita ya Mv Bukoba kupinduka na ilichukua muda waokoaji kufika eneo la tukio na hata waliofika hawakuweza kuokoa

Kutokana na ajali hiyo ya Mv Bukoba. Ina maana hatujajipanga kweli huku mtu mmoja akizunguuka kuangalia kero za wananchi akiwa anahutubia helicopter ipo juu...walishindwa kusafirisha waokoaji kwa ndege faster eneo la tukio?

Umeongea kweli Mkuu inaudhi sana ,alafu utasikia mpumbavu mmoja anajiuzuru ubunge kuunga mkono juhudi ,ukiangalia juhudi huzioni.,

Yaani tunashindwa kuwa na kikosi cha uokoaji chenye vifaa vya kutosha kwa dharula kama hii,

Angalia vikosi vya zima moto na uokoaji vilivyochoka,

Jambo jingine baya zaidi abiria wanapanda chombo bila hata ya kupewa life jackets wavae,zile life jackets ndiyo usalama wao wanapokuwa safarini ndani ya maji..

Ni sawa na dereva wa pikipiki kuvaa helmet au abiria kufunga mkanda ndani ya bus,tungeweza kupunguza idadi ya vifo kwenye ajali hii.

Ngoja Sumatra waje na drama zao hili linawahusu sana...waje watuambie nini maana ya Safety First kwa vyombo vya Majini.

Huenda chombo pia kilikosa uwiano na Chief Engineer pamoja na Chief officers waljiridhisha kiasi gani kabla ya chombo kuanza safari,hapa lazima Captain wa Meli awajibike.
 
Ila nimeshtushwa na hii habari ya kusitishwa zoezi la uokoaji. Hivi ukisitisha mpaka kesho utategemea kuokoa au kuopoa miili!! Sijaelewa kabisa.
 
Zoezi la uokoaji limesitishwa hadi kesho kutokana na giza nene ziwani-RC. Miili 44 imeokolewa na mahututi 37
 
Sio kila sehemu muweke siasa na hoja za kipumbavu kama hizi, mnajifanya kujua kila jambo end of the day mwaonekana ka mitaa.hiratu, unajua kinachosababisha marine vessel hasa melii nini?
Kunapokosekana uwiano wa uzito kati ya mzigo wa chini (watertanks) na ule wa juu (abiria na mizigo) hiyo ndo huwa sababu kubwa ya meli kuoverturn hata kama ni mpya.

Maafisa wa meli wanapozidisha mzigo hupunguza maji ya chini ili kudanganya wakaguzi...hiki ndicho kilichotokea hata kwa Mv Bukoba, unapopunguza mzigo wa chii na kuzidisha wa juu nadhani unajua nini kitatokea endapo ukiweka chupa ya dasani yenye maji nusu ndani ya besini na ukafunga kitu kizito juu ya chupa chenye uzito kuzidi hayo maji nusu. Ni Rais aliyewatuma kuover load? hizi kejeri na dhihaka dhidi ya Rais zinatoka wapi?
Una mahaba na jiwe,kwa hiyo roho ya jiwe ni bora kuliko roho za hao waliozama?
 
Back
Top Bottom