Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Zoezi la uokoaji limesitishwa hadi kesho kutokana na giza nene ziwani. Miili 44 imeokolewa na mahututi 37
Nashangaa kauli hii anaanzaje kuitoa mtu timamu?

Wanapaswa kujiangalia na kujitathmini upya.
 
RIP marehemu wetu,Mungu awaponye majeruhi wote.Poleni wote kwa janga hili.Muhimu kwa hatua hii tusihoji tuwape moyo team ya waokozi na huduma ya 1 majeruhi
 
Mnakataa nn hebu angalia tu ma bus ya mwendo kasi yanajazaje na je ule ndio uwezo wake?
 
Kwahiyo tangia hiyo meli ianze kufanya safari miaka yote hiyo leo ndio wamepunguza maji kwenye hayo MABOYA ya chini?
Hiyo huwani tabia ya meli zote zinapozidisha mzigo hupunguza uzito wa chini li msari usonekane kuzama iruhusiwe kuondoka, meli inapoondoka mzigo unakuwa evenly distributed hivyo meli kuwa stable, stability hukosekana inapokaribia kufika ambapo abiria wengi hutoka sehemu walizokuwa wamekaa na kurundikana sehemu moja (mfano Mv Bukoba) na kwa kuwa chini maji yanayotakiwa kuipa stability meli yametolewa meli hupinduka.
 
Sijajua, shida ni nini hasa!
1. Tamaa ya wenye vyombo hivyo mpaka kuzidisha abiria?
2. Elimu ndogo ya abiria kuhusu usalama wao na vyombo wanavyovitumia?
3. Uhaba wa vyombo vya usafiri?
4. Kutojali kwa wenye mamlaka?
Inawezekana ikawa mchanganyiko wa sababu zote hizo ulizotaja.
 
Hii ya watu kuwa na mamlaka na tamaa ya pesa na kujaza watu na mizigo zaidi.. inasikitisha sana

Kama ni hivyo kitu ambacho wengi tumekuwa tunahisi.. basi watu wachukuliwr hatua ya kesi na kufungwa jela maisha.. iwe funzo kwa wengine wenye tamaa ya pesa.. na pia Raia wafundishwe kukataa kuendelea na safari wakiona haya ya kujazana kupitiliza
 
Kwakweli aibu kubwa kwa serikali ya Tanzania kwamba vikosi vya uokoaji havifanyi kazi usiku kwa sababu ya Giza?
Hivi hii serikali kweli inajari wananchi wake? Hivi mkuu Wa mkoa kama mwanao nae angekua kwenye hivyo meli ungediriki kutamka zoezi la.uokoaji limesitishwa?
Kama watu wanaweza kulowa dagaa usiku Wa manane tena kwa chemli mmeshindwa kuokoa watu?

Dah nimeumia sana namuwaza MTU yule ambae bado yuko hai ndani ya meli anasubiri uokozi
Namuwaza MTU yule ambae yuko hai ila analiwa na samaki akiwa anajiona mzimamzima, Leo ndio umetimia ule msemo Wa PAMBANA NA.HALI YAKO

Mkuu Wa mkoa anaenda zake kulala kashasema zoezi litaendelea kesho ambao bado mpo hai pambaneni na hali zenu

This is Africa😢😢😢😢😢

Mungu tusaidie
 
Sijajua, shida ni nini hasa!
1. Tamaa ya wenye vyombo hivyo mpaka kuzidisha abiria?
2. Elimu ndogo ya abiria kuhusu usalama wao na vyombo wanavyovitumia?
3. Uhaba wa vyombo vya usafiri?
4. Kutojali kwa wenye mamlaka?
sababu zote ni sahihi
 
Sijajua, shida ni nini hasa!
1. Tamaa ya wenye vyombo hivyo mpaka kuzidisha abiria?
2. Elimu ndogo ya abiria kuhusu usalama wao na vyombo wanavyovitumia?
3. Uhaba wa vyombo vya usafiri?
4. Kutojali kwa wenye mamlaka?
TATIZO NI MAZOEA MKUU,KWAMBA "MIAKA YOTE HUWA INABEBA HIVI NA HAIJAPINDUKA"
 
Back
Top Bottom