Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Wanasitisha vipi uokoaji? Hivi vitu vinatia hasira. Kwa hiyo kesho wataenda kuokoa maiti? Ni binadamu gani anaweza kuishi ndani ya maji kwa zaidi ya masaa kumi huku akipigwa baridi!? JWTZ hawana meli au boti ziwani Victoria? Polisi nao hawana vifaa vya uokozi? Hata kama umaskini hii too much.
Poleni mliofiwa,

poleni mliojeruhiwa,

Mwenyezi Mungu awanusuru na kuwalinda waliopo ziwani wakiwa hai.

Mungu awapokee kwa amani waliofariki
 
Si utani ngoja nikutajie listi

1. Kingunge alitembelewa mwishowe akavuta

2. Maria na Consolata mwishowe akavuta

3. Samuele Sita mwishowe kavuta

4. Yule aliyechora nembo ya taifa mwishowe kavuta

5. Mzee Majuto naye alivuta

6. Mzee mmoja wa CCM (jina nimelisahau) naye kavuta

7. Wengine niliowasahau nao wamevuta

Yaani hawaponi kabisa!

Duh nimeaanza kumuogopa kwa kweli ata nikiumwa nikimsikia anakuja ntakimbia na dripu zangu maana maisha matamu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hii ya watu kuwa na mamlaka na tamaa ya pesa na kujaza watu na mizigo zaidi.. inasikitisha sana

Kama ni hivyo kitu ambacho wengi tumekuwa tunahisi.. basi watu wachukuliwr hatua ya kesi na kufungwa jela maisha.. iwe funzo kwa wengine wenye tamaa ya pesa.. na pia Raia wafundishwe kukataa kuendelea na safari wakiona haya ya kujazana kupitiliza
Hawa jamaa juzi tu Rais kawalipa malimbikizo yao yote ya mishahara!
 
Ila nimeshtushwa na hii habari ya kusitishwa zoezi la uokoaji. Hivi ukisitisha mpaka kesho utategemea kuokoa au kuopoa miili!! Sijaelewa kabisa.
Una mahaba na jiwe,kwa hiyo roho ya jiwe ni bora kuliko roho za hao waliozama?

Jiwe ndo mamaako vile? kama ndo yeye ewaaa..tuko busy kukutafuta mdogo wako.
 
Wtf kisa giza? huyu mseng.e si angekaa kimya kuliko kuongea haya mashudu aisee
 
Wanasitisha vipi uokoaji? Hivi vitu vinatia hasira. Kwa hiyo kesho wataenda kuokoa maiti? Ni binadamu gani anaweza kuishi ndani ya maji kwa zaidi ya masaa kumi huku akipigwa baridi!? JWTZ hawana meli au boti ziwani Victoria? Polisi nao hawana vifaa vya uokozi? Hata kama umaskini hii too much.
Poleni mliofiwa,

poleni mliojeruhiwa,

Mwenyezi Mungu awanusuru na kuwalinda waliopo ziwani wakiwa hai.

Mungu awapokee kwa amani waliofariki
Wanavyo wa kupiga chadema hata kama ingekuwa ni Giza totoro vya uokozi hakuna. Wanashindwa hata kuwapata mafuta taa ya karabai wavuvi na posho wazurure usiku kucha kufanya uokozi.Ngoja tuendelee kurudia uchaguzi tu ndo tukiwezacho.
 
Mimi bado sijamwelewa huyo mkuu wa mkoa....
Anasema tunasitisha uokoaji mpaka kesho asubuhi kwa sababu giza limeingia!!!

Maswali makuu ya kujiuliza.
1/Watu waliopo hai chini ya maji(kama wapo), wataendelea kukaa kwenye maji wakiwa hai mpaka kesho?
2/Nini maana ya dharula, ikiwa unaweza kuhairisha?
3/Wameshindwa kupambana na giza ili uokoaji uendelee?

Hivi ile kauli ya hapa kazi tu ni blah blah ya kuwachota wajinga tu?
 
Kibaya ZAIDI kivuko hakuna hata kifaa cha kujiokoa,,,kwa kifupi TANZANIA tunafanya kazi kwa mazoea,Au sijuwi UZEMBE,,,nashindwa kuelewa,,,,hata hivi VIVUKO VINAVYOFANYA KAZI MAGOGONI DAR ....KIGAMBONI ,,,watu hawana IDADI MAALUM,, hata LIFE JACKETS PIA NI CHACHE kulinganisha na ABIRIA,,.NA PIA LIFE JACKETS ZENYEWE ZIMEPIGWA KUFULI KTK CHUMBA MAALUM,,,sasa najiuliza IKITOKEA AJALI HAPA,,,hayo MAJACKETS watu watayatoaje?AU TUTAJIOKOA VP ikiwa mwwnye FUNGUO WA CHUMBA CHA JACKETS HAYUPO ON BOARD?
 
Ila nimeshtushwa na hii habari ya kusitishwa zoezi la uokoaji. Hivi ukisitisha mpaka kesho utategemea kuokoa au kuopoa miili!! Sijaelewa kabisa.
kama wangeendelea usiku huu wangemwokoa nani ndugu meli imezama na watu wako ndani ya maji tangu saa nane? wanasitisha ili kupunguza uwezekano wa ongezeko la vifo.
 
Jitihada za uokozi zinaendelea....
Mamia ya watu wanahofiwa kufariki baada ya kivuko cha MV Nyerere walichokuwa wanasafiria kuzama katika ziwa Viktoria mkoani Mwanza magharibi mwa Tanzania.
Wizara ya uchukuzi na mawasiliano Tanzania TEMESA imetoa taarifa ikithibitisha mkasa huo kilichotokea kati ya Ukara na Bugolora wilayani Ukerewe majira ya mchana.
Maafisa wa serikali nchini wamethibitisha kwamba shughuli ya kuwaokoa manusura inaendelea.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba kivukio hicho kilikuwa kimebeba mamia ya abiria.
Kamishna wa eneo jirani la Mara, Adam Malima ameeleza kwamba maafisa kadhaa kutoka enoe hilo wakiwemo polisi na jehsi la majini wanaelekea kujiung akatika jitihada za uokozi.
''Hatuijui hali halisi tunakwenda kuikagua kwanza alafu baadaye tutatoa tamko rasmi.
Malima ameeleza kwamba maboti ya polisi na jeshi watashirikaian akatika zoezi hilo la uokozi.
''Tunaomba mungu atupe subira kwa wakati huu, na tusishuhudie idadi kubwa ya vifo'

Mkasa huo umewashutusha wengi nchini kama mwanamke mmoja aliyeshuhudia mkasa huo ambaye alionekana kujawa na hisia.
''Tazama Tazama.. Kivuko kile pale kimezama …….miili inaelea, imezama sasa hivi''.

Mikasa ya vivukio kuzama Tanzania



Tanzania ina historia ya ajali za vivukio kuzama, kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kilikuwa ni mnamo Mei 1996, wakati MV Bukoba kilipozama kutoka Mwanza katika ziwa lilo hilo Viktoria magharibi mwa Tanzania na kusababisha vifo vya takriban watu 1000.
Rekodi rasmi hatahivyo iliopo ni watu 894 waliofariki.
Kumewahi kushuhudiwa pia mikasa mingine kama vile Mv Skagit kivukio kilichozama mnamo 2012 wakatikikiwa kimebeba abiria 290 wakiwemo watalaii 17 kutoka pwani ya Zanzibar.
Mwanza ni mji muhimu wenye bandari Tanzania katika ziwa Viktoria, inayopokea bidhaa kama pamba chai, kahawa zinazotoka magharibi mwa nchi hiyo.
Ziwa viktoria ni la pili kwa ukubwa duniani baada ya ziwa Superior Amerika kaskazini.
 
Back
Top Bottom