kivyako
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 14,340
- 12,055
Wanataka wakapumzike, hawana haraka!Nashangaa kauli hii anaanzaje kuitoa mtu timamu?
Wanapaswa kujiangalia na kujitathmini upya.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanataka wakapumzike, hawana haraka!Nashangaa kauli hii anaanzaje kuitoa mtu timamu?
Wanapaswa kujiangalia na kujitathmini upya.
Ugumu uko wapi? Mbona inapotokea ajali sehemu nyingine mfano ndege tunajua ilikuwa na abiria kadhaa na wahudumu kadhaa
Hili halihitaji science yoyote. Una gari lako limebeba watu 7 hivi unahitaji sayansi gani kujua wapo 7
Huu ni uzembe tu. Taarifa za awali zingeonyesha kivuko kina watu wangapi. Hili si gumu, wagumu ni sisi Watanzania na Waafrika kila kitu ni bora liende.
Utakuwaje na chombo usichojua uwezo wake na kimebeba uwezo gani?
WELL SAID BROTHER![emoji115][emoji106].Kuna mambo yanasikitisha
Tani 25 ni sawa na kilo 25,000. Abiria 100 katika wastani wa kilo 70 kwa abiria ni sawa na kilo 7000 sawa na tani 7. Magari 3 hayajaelezwa ni aina gani hivyo hatujui uwezo wake.
Tufanye assumption kila gari lina tani 4,magari 3 ni tani 12. Ukijumlisha 12 na 7 ni tani 19.
Haiwezekani kivuko kuwa na uwezo wa tani 25 sawa na abiria 100 na mgari 3! hesabu hazikubali
Pili, abiria wanopanda lazima wawe na ticket au wawe registered. Hadi muda kivuko kinazama taarifa za idadi ya wasafiri zingekuwa zimeshapatikana. Hakuna!, tunasubiri taarifa zipikwe!
Hili halihitaji sayansi, ni kwamba, wanaopanda wanajulikana sasa kwanini idadi isijulikane?
Tatu, Watanzania na Waafrika ni watu wa ajabu sana. Hatuwezi kufikiri mambo makubwa na muhimu kwasababu akili zetu zimeelekea katika vitu visivyo na maana.
Kila siku utasikia siasa , na siasa zenyewe ni hizi za kununua. Matumizi kwa mambo yasiyomsaidia mwananchi au kuumizana wenyewe kwa wenyewe
Nguvu kubwa zimeelekezwa kukabiliana na wanasiasa badala ya kuelekeza nguvu hizo katika kuzuia madhara kama ujazo wa ziada wa abiria, kutafuta vyanzo vya ajali na kudhibiti n.k.
Kuzama kwa MV Bukoba ilikuwa funzo kubwa, leo tungeshajua nini kimetokea na kwanini
Tungechukua tahadhari kabla kuzuia matatizo kama haya.
Eti bado hatujui hata kuchukua takwimu za wasafiri licha ya funzo la MV Bukoba!! Mungu wangu
Hatutajua watu wangapi wamefariki kwasababu hatuna utaratibu , kila kitu tunafanya kwa kubahatisha tu, pandeni hata 1000 ni kazi ya mungu. Wenye dhamana fikra zote ni siasa tu
Mag3 Pascal Mayalla JokaKuu Mwalimu
Msalimie Lijua LikaliKilombero tulipiga kelele wakajenga daraja, wajenge madaraja kwenye vivuko vyote
Kwahiyo tukubaliane tu kuwa yaliyotokea ni sawa sawa, na kwamba uwezo wetu wa kufikiri umefikia kikomo.
Mbona vivuko vingine dunia hutoa taarifa hizo?
Wao wanawezaje sisi hatuwezi.
Hata boti za watalii tu wala si vivuko zina utaratibu wa kujua idadi ya abiria, sisi tunaendelea kuishi kwa njia za ramli. Akili zetu ni kupambana na mambo yasiyo na maana ndiyo maana hatuwezi kujifunza kutokana na makosa kama MV Bukoba.
Sasa unashangaa nini kutokujua idadi ya watu .......kivuko cha hapo kigamboni geti likifunguliwa kila mtu spidi ndani ....kila mtu anawahi anapokwenda .....sawa na mwendo kasi utahesabu abiria wangapi wapo kwenye gari ..... ni ajari kivuko kime overload basiNi ajabu sana kutoa taarifa kuwa haijulikani watu walikuwa wangapi
Hebu acheni kucheza na maisha ya watu jamani
Siyo kila kitu ni kulaumu tu, unakumbuka wale vijana 12 na mwalimu wao waliozingirwa na maji Thailand ilichukua muda gani kuwaokoa? Na kwa hali ilivyo humo hakuna mtu aliye hai labda kwa miujiza tu.Kwenye mafunzo ya huduma ya kwanza unashauriwa kujilinda kwanza wewe mtoa mhuduma ndiyo utoe huduma kwa mhusika.
Unakuta mtu kakatwa mapanga anavuja damu wewe kwa kujiona umepitia mafunzo ya huduma ya kwanza unamvamia tu bila hata gloves, utaenda na maji.Hapo wamesitisha zoezi kwa kuhofia maafa zaidi.
Duuu wewe!Si utani ngoja nikutajie listi
1. Kingunge alitembelewa mwishowe akavuta
2. Maria na Consolata mwishowe akavuta
3. Samuele Sita mwishowe kavuta
4. Yule aliyechora nembo ya taifa mwishowe kavuta
5. Mzee Majuto naye alivuta
6. Mzee mmoja wa CCM (jina nimelisahau) naye kavuta
7. Wengine niliowasahau nao wamevuta
Yaani hawaponi kabisa!
Duh nimeaanza kumuogopa kwa kweli ata nikiumwa nikimsikia anakuja ntakimbia na dripu zangu maana maisha matamu
rIpTaarifa nilizozipata haraka sasa hivi ni kuwa watu wengi sana wanahisiwa kufa maji baada ya kivuko kubinuka juu chini, chini juu katika kisiwa cha UKALA wilayani Ukerewe.
====
Taarifa Kwa Umma Kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme-TEMESA Kuhusu Kuzama Kwa Kivuko Cha MV.Nyerere
View attachment 872340
Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara. Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka.
Amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho.
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko na watatoa taarifa baadaye.
Kivuko cha MV. NYERERE kilinunuliwa na kuanza kutoa huduma mwaka 2004. Kilifungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 JULY 2018. Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja.
UPDATES: 1900HRS
=> Watu watano wamekufa na wengine 32 wameokolewa mpaka sasa ila hali zao ni mbaya kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere.
=> "Mtu Hajalipwa Mshahara Halafu Anasikia Trilion 1 Imepotea Inauma" -Joseph Mkundi
Mbunge Joseph Mkundi akitahadharisha kuhusu kivuko cha MV Nyerere Apr 24, 2018
Alikuwa akichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano iliyopo chini ya Waziri wake, Profesa Makame Mbarawa.
UPDATES:
AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE: WATU 44 WAMEFARIKI, ZOEZI LA UOKOAJI LASITISHWA HADI KESHO
Mbali na idadi hiyo ya waliofariki, Watu 37 wameokolewa katika ajali huku hali zao zikiwa mbaya
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema zoezi la uokoaji limesitishwa kutokana na giza kuingia
Poleni sana kwa maafa hayo wenzetu wa ukerewe
Awanusuru chakula cha samaki orMwenyezi Mungu awanusuru
Dah....una fire extinguisher nyumbani?[emoji41]