Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Mkuu umeongea kweli tupu!

Kwa mujibu wa watu walioko kule ambao wamepata maelezo kutoka kwa manusura, inasemekana kivuko mbali ya kuwa na watu wengi, kulikuwa na mizigo mingi hasa mahindi na saruji, na magari makubwa mawili. Inasemekana wakati kinakaribia kufika ng'ambo ilibidi kukata kona ili kwenda kwenye uelekeo sahihi wa kupark. Sasa wakati wa kukata kona hapo ndo mzigo wa upande mmoja ulihamia upande wa pili hivyo balance ikakosekana kika -overturn upside down.

Haya ni maelezo ya awali lakini.
Ni sahihi. Kuna muokoaji wa kwanza kabisa kufika amenitonya
 
Awamu hii ya Utawala, uhai wa watu si chochote, si lolote.

Pesa nyingi zinapotea kwa marudio ya chaguzi fake lakini mambo kama haya hazingatiwi.

Yaani nchi kubwa kama hii inakosa tochi za kumulika.

Hata ajali ile ya juzi Rusumo hadi Helkopita ilitoka Rwanda kwenda kuokoa uteketeaji wa mali kwenye ajali ya moto.

Kitengo cha usalama hasa cha dharura na uokoaji kinatakiwa kilichokamilika sio hichi cha kusitisha kazi kisa giza.

Kwa serikali hii tutapiga kelele leo, kesho na kesho kutwa halafu jambo litasahaulika hadi itokee ajali nyingine tena maana utekelezaji wa makosa haupo kabisa
Zimamoto na uokoaji ndo idara mbofu kuliko majshi yote, hawana vifaa, maslahi duni na wanadharaulika hata mkuu wao hatembei na msafara gari angalau 2
 
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Idara ya uhamasishaji na chipukizi UVCCM Taifa Ndugu Hassan Bomboko inasema Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Kheri Denis James (MCC) amesikitishwa na kuguswa na ajali mbaya ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika ziwa Victoria iliyotokea leo ambapo wapo waliojeruhiwa na wengine kufariki dunia hivyo ametoa salamu za pole kwa wote walioguswa na kuathirika na tukio hili la kuhuzunisha na kusikitisha.

Taarifa hiyo imeendelea kusema Ndugu Kheri anawaombea majeruhi kupata nafuu, ndugu na wote waliopoteza jamaa zao wawe na subira katika kipindi hiki kigumu. View attachment 872725
Angekua Lissu hii taarifa angeiita UVCCMorial rubbish!!

Makosa kibao: Bugorara, Ukala , "safari zake ZA kati ya..."
 
Afu Siku unamsikia jiwe anasema " kwani serikali ndio ilisababisha kivuko kuzama"[emoji27] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
Mkuu umeongea kweli tupu!

Kwa mujibu wa watu walioko kule ambao wamepata maelezo kutoka kwa manusura, inasemekana kivuko mbali ya kuwa na watu wengi, kulikuwa na mizigo mingi hasa mahindi na saruji, na magari makubwa mawili. Inasemekana wakati kinakaribia kufika ng'ambo ilibidi kukata kona ili kwenda kwenye uelekeo sahihi wa kupark. Sasa wakati wa kukata kona hapo ndo mzigo wa upande mmoja ulihamia upande wa pili hivyo balance ikakosekana kika -overturn upside down.

Haya ni maelezo ya awali lakini.
That is possible. Sasa kulitokea na shifting of the cargo na kufanya centre of gravity kushift hivyo metecentric height kubalika na kupelekea negative G. Hapo mpinduko ni lazima
 
Ni ngumu sana kujua kivuko kimebeba wangapi, hata kwa kutumia ticket hawawezi jua kimezama na wangapi

Tutegemee kuna watanzania wengine hawataokolewa

Ingejulikana idadi kamili yeah ila haijulikani
Miili itandelea kuokotwa kwenye fukwe za Nansio na wavuvi watavua sana watu coz hakuna vyombo vya uhakika ni mitumbwi tu
 
Hivi ugumu wa kujua watu waliokuwemo hata kwa makidirio unatoka wapi!?

Si waangalie vitabu vya risiti au rekodi za risiti za kieletroniki kama zinatumika huko wataweza kukadiria watu walikuwa wangapi
 
serikali imeelekeza bajeti zake kununua wapinzani badala ya kusaidia wananchi
Bro huu sio muda wa lawama tuwaombeeni wenzetu wapate usalama na mikono ya mungu ipate kuwasimamia siku katika hali waliyonayo
 
Business as usual: Kwa sababu aliyetoa hoja ya kutengenezwa kwa kivuko hiki ni Mbunge wa CDM, basi alijibiwa kimkakati na likapita. Ila leo tunaendeleza unafiki wetu wa kupost picha za mishumaa na kuandika kimombo R.I.P.
Najua fika kuwa hiyo RIP yenu sio ile ila mlimaanisha Return if possible. Ndio, si ni ile kauli mbiu yetu ya kutopeleka maendeleo kwa wale waliochagua upinzani sasa inazaa matunda.
Nawaona mlivyokaa kimya leo. Tujifunze kupitia hili na tuanze upya sasa.
 
Back
Top Bottom