Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Aliyetoa kafara hamumuulizii mnamuulizia Mbowe.mimba zingeingia kwa Bluetooth au whatsap mngekuwa MNA mapacha.
 
Wenzako jana wameacha kuokoa wale wameenda saa tatu kuokota maiti majini baada yakujua wote watakuwa wamekufa, iwe kwa kukosa hewa au maji kuwazidia,

Nahisi hii ajali ingetokea kaskazin au Mara huko wangeambiwa wamejitakia wenyewe

Nchi imezungukwa na maji inashindwa kuwa na wazamiaji wanaotumia tochi za ndani ya maji, yani wanatushinda hadi wanaozamia pweza pale bahari ya hindi
 
We ni mchochezi kesho saa4 asubuhi uje central kwa mahojiano zaidi
 
Hutupati ng'o sisi wenye mioyo safi.
Wenye moyo safi watachanga usijichanganye kama wewe una roho ya korosho , Rip waliofariki
memorial-candles-main_0.jpg
 
Dalili zimeanza kuonesha, baadhi ya Wanasiasa kudai watu flani wawajibike,wajiudhuru, mawazo ambayo yako kisiasa zaidi, ni kweli ipo sababu iliyopelekea kutokea ajali hiyo mbaya, sababu zinaweza kuwa ni za uzembe wa kibinadamu,au za kitaalamu(mechanical problems), hivyo kwenda moja kwa moja kwenye(human error) tutakuwa hatuwatendei haki wataokumbwa na sakata.

Itakuwa kisiasa zaidi, hivyo kabla ya yote Mashauri uchunguzi wakina ufanyike, isije kutokea kama ile ya Muhimbili kupasua kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa, maamzi ambayo yalipelekea kuwapoteza !adakitari bingwa wa mifupa na wenye uwezo mkubwa, ambao Mara moja Botswana iliwachukua hadi leo wanafanya maajabu huko.

Ikumbukwe mfano Prof. Kinasha alieleza kwamba alikuwa ameshafanya upasuaji wa kichwa kwa watu 1,008 na wote walipona, na huyu ambaye ni bahati mbaya alikuwa wa 1,009. Sasa akahukumiwa kwa kosa moja tu !!!!

Hii ilikuwa kisiasa zaidi ikiongozwa na Prof. Mwakyusa, Sikatai kuwa uzembe ni mbaya na unaweza kugharimu maisha ya watu, jambo ambalo kamwe halikubaliki wala kuvumilika.

Lakini pia sikubaliani kuona kuwa watu wanaadhibiwa kwa mintarafu ya kisiasa, watu kutafuta kiki za kuonekana na jamii kwamba wamechukua hatua. Ajali hutokea kokote kule hata Ulaya na marekani, mfano Nyambizi ilizama, je nani aliwajibishwa?

Ndege aina ya Conctord iliua watu kibao je nani alifukuzwa kazi? Tusilione limetokea hapa kwetu, sasa ukawa muda wa wanasiasa kuishutumu Serikali nakuitaka kufukuza watumishi wake kwa madai kwamba wamefanya uzembe.

Kikubwa hapa ili Wanasiasa waoneshe kukomaa kwao wanatakiwa kuitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya sababu zilizopelekea ajali hii mbaya. Huu ni Ushauri tu na si vinginevyo.
1)Madai kwamba kivuko kilijaza kupitiliza,inaashira matatizo katika usafiri wa maji,Hii no siasa tosha
2)Kotojulikana idadi kamili ya abiria mpaka wakati huu,inaonesha matatizo katika usimamizi,Hii ni siasa tosha
3)Kushindwa kuendelea kuokoa wakati wa usiku, inaonesha hakuna maandilizi ya kupunguza madhara,Hii ni siasa tosha
4)Mbunge wa eneo husika kutaadharisha mapema kuhusu maafa ya aina hii,ni siasa tosha
Huwezi kulitenga jambo hili na siasa kamwe,limejaa siasa kila Kona.
 
Simply "Basic"
Halafu tumekuwa na past experience ya hii kitu. Tumewahi pata haya majanga.
Na sababu kama hii..

"Boti ilikuwa na zaidi ya watu 400"

3 times the number it's capable of..
Hili nalo litapita na hazitaisha wiki mbili tutakuwa tumeshasahau. Ndiyo shida yetu. Ukiangalia ajali zilizokwisha tokea siku za nyuma ungefikiri tungekuwa na watu makini kweli kweli. Lakini wapi. Mwaka ujao utakuta kivuko kingine kimebeba watu mara saba ya uwezo wake.
 
Chadema kula kitu mnafeli kuanzia uchaguzi hadi namna ya kutimiza majukumu yenu.....uhakika pengo la Dr Slaa halitazibika!
Kila mtu anaehoji mna mweka label ya chadema.
Na hii inaonyesha jinsi gani mlivyokuwa shortsighted.

Hongera kwa kuchagua ujinga na kuongozwa na tumbo lako.

Mmesitisha zoez la uokoaji jana sababu ya giza. Kweli misukule nyie mna tabu sana
 
Ni sawa ila unapokuwa na mfumo ambao watu wake hawajajiandaa na majanga, pindi linapotokea hata akili ya kujiongeza hawana!! Na tatizo kubwa pia ni kutegemea vivuko vya abiria ndio vitumike, kwani vingi viko mwanza na kutoka mwanza hadi huko ni parefu na vingi unakuta viko kwenye safari zake!!! Ila waambiwe kuna magendo ziwani, utaziona zile boti za kwenye movie
Au CHADEMA wanafanya mkutano baharini
 
Aise imenikumbusha wimbo wa Marijani Rajabu.........Dunia ya sasa imani imekwisha mioyo ya watu imebadilika wala hakuna uaminifu tena.............
Asee nimekomenti huu uzi kwa kukumbukia hicho kibao cha nguli na manju wa muziki na mashairi Marijani Rajabu.
 
Yaani hadi Rais Kenyata kasema watatoa msaada wa vitu vitakavyohitajika kwa uokozi tu. Nadhani amestukia zile bati n.k bukoba. Haha hahaaa. Cha kufanya ni kuwatembelea wafiwa manyumbani tu.
kumbeee " hahaa " Daaahh aibu sana Aisee
 
Back
Top Bottom