Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ni majonzi makubwa mno, pale ninapowaona ndugu zangu wamelala wamenyamaza kimya! Walitoka Ukara kwenda hutafuta mkate wao wa kila siku na mahitaji ya watoto wa shule, safari ya kurudi ukara ikafika wakawapungia mkono ndugu zangu wa Bugorola wakiwa na matumaini na nyuso za furaha mahitaji yao yamekidhi matamanio ya mioyo yao.

Mita chache kivuko kikaanza kuonekana maeneo ya ukara hichooooo kinakaribia, watoto wakaanza kusogea karibu kuwapokea wazazi ndugu jamaa na marafiki zao, kumbe walikuwa wanakwenda kushuhudia kivuko kikiwaangamiza na kuwazamisha kabisa "wakara" dah! Nimlilie nani siku ya leo? Tangulieni mbele ya haki ndugu zangu, Mungu awape pumziko la milele msitarehe kwa amani katika nyumba yenu ya milele Amen!
 
Ambavyo kila siku miundo mbinu haipo?hilo nalo unalitetea au una umri chini ya mika 18?unaelewa unachotetea?tuache tabia ya kukumbatia maovu
Hii ni Mara ya ngapi kuona majanga makubwa?
 
Hapa tunaendelea kurisk maisha ya watu ninajua kutakuwa na watu mnahusianisha malalamiko ya watu na siasa but trust me tunatatizo kubwa sana hii nchi katika suala la usafiri wa majini na departments za uokozi whether we like it or not

Hii si mara ya kwanza kwa ajali kama hizi za kizembe kutokea na inaonekana dhahiri hatujawahi kujifunza kitu chochote kutokana na hayo

Kwa mkazi wa kanda ya ziwa anayesafiri mara kwa mara kwa meli na vivuko anaelewa ninachoongea ,

Tatizo la sisi wa Tanzania na waAfrica tunakuwa driven na emotions zaidi kuliko uhalisia , ukweli huwa unapigwa vita kwa nguvu siku zote na hii ni kansa inayotutafuna miaka yote na beleive it or not kuna janga lingine linakuja kutokea kama hatua madhubuti hazitachukuliw a , hatuna vivuko wala meli ila tuna vyuma chakavu vya usafiri wa majini + uzembe katika usimamizi wa usafiri wa majini + uhaba wa nguvu kazi yenye taaluma na vitendea kazi vya kisasa katika vitengo vyetu vya uokozi

Yaani nyie mnaona ni sawa mkuu wa mkoa kutoa order ya kusitishwa kwa shughuli za uokozi kisa giza limeingia ? , mitumbwi ya wavuvi ndo ilikuwa boat za uokozi dah ! Halafu bado hatuoni kuna tatizo ila tunaendelea kushabikia na kutetetea upumbavu kama huu , kweli hii inathibitisha IQ level na total mental inferiority kwa wengi wetu
 
Jamani mlitaka sfanye nini wakati hakuna vifaa vya kuokolea muda huo?? Na sio kwamba atakuwa alijiamulia tu mwenyewe, hao wazamiaji hawana vifaa vya kufanyia kazi kwenye mwanga itakuwa gizani?? Ni aibu kwa nchi, hatuko tayari kwenye majanga!! Ya nchi kavu tu yanatushinda itakuwa ya majini??
Kwanza tujiulize kivuko kilipinduka saa 8 mchana,je tuseme saa 10 au 12 kuna raia yyt anaweza bado akawa hai?Kwenye ferry kuna sehem yyt mtu anaweza jificha endapo kikazama na maji yasimfikie?

Mimi mafikiri ni alikosa kauli ya busara tu juu ya usitishwaji wa zoezi lkn naamini baada hata lisaa halijakatika toka izame hakuna raia aliyekuwa hai na waliopatikana hai ni wale walikuwa wanatapatapa nje ya kivuko na sio waliofunikwa.Hapa jamaa niseme tu walikosa utashi wa kisiasa jinsi ya kuwapumbaza wananchi na kwa Mimi wakiendelea tu na zoez kujifanya wanaokoa kumbe zoez ni kuopoa.
 
Inanikumbusha miaka ya 80s wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya pili iliyokua inongozwa na Mzee Mwinyi, wakati huo Kigamboni ilikua ipo kwenye Wilaya ya Temeke, kulikua na kivuko kibovu sana

Mbunge wa Temeke kipindi hicho aliyekua anaitwa Masudi Ally alitoa shilingi kwenye bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi akipinga Serikali kushindwa kutekeleza ahadi zake za kununua kivuko kipya kwa ajili ya watu wa Kigamboni

Alikalishwa chemba na kushinikizwa/kushawishiwa airudishe shilingi na kulikua na zogo kubwa Bungeni(ilikua ni Mfumo wa Chama kimoja), Waziri Mkuua akiwa Warioba kama sikosei

Haikupita hata wiki moja Ferry ile ikawamwaga watu baharini na vifo kadhaa vikatokea! Mh. Masudi alikaa kimya kabisa na wanasiasa wengine na wananchi ndio wakawa wanalalamika kwa kitendo cha Serikali kua inapuuza mambo ya msingi yanayohusu roho za raia wake

Kitu cha kushangaza Mheshimiwa Masudi hakurudi Bungeni katika uchaguzi uliofuata maana Kamati Kuu Ya Halmashauri Kuu Ya CCM ilikula kichwa, jina lake halikurudi ili apigiwe kura na wananchi!
 
Kitengo Cha uokoaji kipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Na Mwenye gari alifuta Bajeti ya Maafa tangu kashika sterling Kwa hoja Kuwa enzi zile Za Mkwere watu walikuwa wanapiga hizo hela

Ajali kubwa Kama ile cordination yake haiwezi Kuwa chini ofisi ya RC


Ni kweli, lakini kama ajali imetokea mita 50 tu toka nchi kavu, basi kiongozi angejiongeza, creativity ni moja ya sifa za kiongozi, ilikuwa tangu mchana afanye maandalizi ya kupata vifaa kwa ajili hiyo, kama ni generators na waya pamoja na bulbs wangekopa, naamini hata ndugu wa wahanga wangeweza kulipa deni iwapo serikali ingeshindwa
 
Unafiki mwingine bana,mbona wanajeshi wetu walipofariki siku ya kuaga miili yao hukumsema mtu ambaye hakuhudhuria kuaga?Maana wewe kazi yako ni kuangalia nani yupo na nani hayupo.Hatushindani ktk misiba ila yafaa tushindane ktk kukinga.
 
Ni rahisi kusema ni mapenzi ya Mungu lakini, binafsi hiyo itakuwa ni sababu ya kijinga. Vyombo vya usafiri vimetengenezwa kitaalamu. Vinatakiwa kuendeshwa kitaalamu kwa kufuata utaratibu au sheria zilizojalibiwa na kuonyesha mafanikio. Wanaoviendesha ni watu waliofunzwa na kusomea taratibu za kuviendesha. Ndivyo ilivyo kwa Ndege, magari pamoja na meli kama hii MV Nyerere iliyozama.

Tatizo liko wapi hadi tuwe na ajali za aina hii? Tujiulize kwa nguvu sana kwa ajali kama hii ya meli ambayo siyo mara ya kwanza. Ilikuwa hivyo na MV Butiama, MV Kipepeo, MV spice sasa ni MV Nyerere! Napenda niseme haya yote yanatokana na ujinga wa waliosomea kuendesha vyombo hivyo. Kila wakati sababu inayotolewa ni kuzidisha uwezo wa vyombo hivyo. Sisi ni watu wa aina gani tusiweza kujifunza kutokana na makosa ya nyuma? manahodha hawa ni wajinga kiasi gani kuliko wanayama wa kufugwa wanaoweza kujifunza kutokana na matendo?

Ni aibu kuona mtu amesoma na kuelewa idadi ya abiria pamoja na uzito wa mizigo unaostahili kubebwa na vyombo hivyo. Nahodha anafahamu zana za uokoaji zilizoandaliwa kutokana na idadi ya abiria wanaobebwa na vyombo hivyo. Nahodha anafahamu uwezo na madaraka aliyonayo kuzuia abiria walio nje ya uwezo wa chombo chake. Sasa tuseme wazi kwamba watu hawa wanasomea unahodha lakini, wana viendesha kwa ujinga wao. Yaonekana wanashindwa kufuata mafunzo yao badala yake wanaongeza vipaji vyao vya kijinga na kuleta ajali kama hizi. Hii ni kwa wote. Hata magari yanaendeshwa kwa ujinga huo na wakati mwingine kujaribu kuonyesha kwamba watengenezaji hawakuelewa uwezo wa vyombo. Ukiwaangalia wakiwa kwenye kazi zao hizi, wanaonyesha umwamba wa kijinga na ufahamu wa kijinga, na mikogo ya kijinga kabisa kiasi kwamba wangeelimika, tusingekuwa na ajali kama hizi zambazo wakati mwingine, tunalazimisha kutoa majibu ya kiroho, eti ni mapenzi ya Mungu. Kusema hivyo
Uliyoongea ni kweli kabisa , mapungufu ni lazima yasemwe huu ni uzembe wa hali ya juu sana hakuna cha mapenzi ya Mungu hapo tuache unafiki
 
sumatra inapaswa kuvunjwa ili kuwe na mamlaka tofauti za kudhibiti usafiri. anga wajitegemee, maji wajitegemee, reli wajitegemee na magari pia wajitegemee,sumatra wana mzigo mkubwa hawawezi kuregulate kote huko

SUMATRA ni hovyo kabisa, ukitaka kuamini nenda kwenye mabasi ya abiria utachoka! Mbaya zaidi ukiwapigia simu kwenye namba zao za bure walizoandika kwenye mabango yaliyotengenezwa kwa gharama kubwa kabisa, wanakuambia sisi tupo HQ, wasiliana na ofisi ya Mkoa ulipo, na wakati mwingine wanakujibu sisi hatufanyii kazi taarifa za simu, fika mwenyewe ofisini kwetu. Imagine kwa hali kama hiyo utasema SUMATRA ipo kwa kazi gani?
 
Na likivuk la.MV Magogoni leo limekata umeme katikati ya maji, wacha nichanganyikiwe, pantoni ikabidi lirudishwe na abiria kushushwa. Nimeleta uzi hapa lakini umefutwa, sijui kwanini
Ndege zinakata moto angani itakuwa MV Magogoni? Wewe kila kitu kwako kibaya. Mara daraja liko mbali sijui ulitaka lijengwe mlangoni kwako. Mara kivuko kinachelewa...kila kitu kwako kibaya, maisha yanakuwa magumu sana ukimind things out of your control.
 
Jana rais wetu ametangaza maombolezo ya siku Nne. Katika hizi siku nafaham kuwa bendera zitapepea nusu mlingoti, je mbali na hili la bendera kuwa nusu mlingoti ni mambo gani ambayo kama wananchi hatupaswi/tunapaswa kufanya na ni sheria kbsa kiasi kwamba ukienda kinyume chake unachukuliwa sheria? Wenye ufaham tunaomba watusaidie
 
Jana rais wetu ametangaza maombolezo ya siku Nne. Katika hizi siku nafaham kuwa bendera zitapepea nusu mlingoti, je mbali na hili la bendera kuwa nusu mlingoti ni mambo gani ambayo kama wananchi hatupaswi/tunapaswa kufanya na ni sheria kbsa kiasi kwamba ukienda kinyume chake unachukuliwa sheria? Wenye ufaham tunaomba watusaidie
tutaona mengi awamu hii
 
Kuna hitajika sana wataalamu wa meli kufanya uchunguzi wa hii ajali na kuja na majibu ya kueleweka, hizi assumptions za overloading, kupinduka, captain deiwaka, kivuko kibovu, Mara watu walikimbilia mbele, Mara unequal load distribution zisije ndio zikatoa majibu..
 
Back
Top Bottom