Amani iwe nanyi wapendwa.
Rais wetu mpendwa Dr Magufuli jana ametoa salamu za pole kwa wote waliofikwa na msiba kutokana na ajali ya Mv Nyerere, pia salamu hizo zimelengwa kwa watanzania wote kwa ujumla ndiyo maana akatangaza siku nne za maombolezo na bendera za taifa kupepea nusu mlingoti nchi nzima.
Jambo la pili amewashukia kama mwewe baadhi ya wanasiasa viherehere waliofilisika kichwani ,ambao kwao ajali ya Mv Nyerere wameigeuza kuwa fursa ya kupata kiki kisiasa.
Ikumbukwe kuwa mara baada ya kutokea ajali hiyo mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe aliitisha vyombo vya habari na kuanza kutafuta kiki kwa kujigeuza mahakama na kuanza kushutumu na kuhukumu watu kwa mambo asiyoyajua vizuri.
Pia Zito Kabwe na James Mbatia hawakuwa nyuma katika kutumia msiba huu kama mitaji yao ya kiki za kisiasa .
Inasikitisha sana viongozi wa vyama vya upinzani badala ya kuwahi eneo la ajali kwenda kutoa msaada kwa wapiga kura wao ,wanabaki twiter kukejeli wafiwa na kujijenga binafsi kisiasa bila kutoa msaada wowote!!!
Hongera sana Rais Magufuli kwa kuwavua nguo hawa wanasiasa uchwara ,wachumia tumbo na wanafiki ,ambao wao muda wote wanawaza siasa tu huku vyama vyao vikiwafia kwa kukimbiwa na wananchi..