Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

SUMATRA NA TEMESA hivi mnakagua kweli hivi vyombo na kuhakikisha zina life jackets za kutosha, life rings, sart, eperb, hand flares, masterlist onboard, manifest before boarding, Captains na Engineers reports, Certificates za crew wote nk..
Maana kwenye picha zinazozagaa hakuna hata moja nimeona kuna life jackets inazagaa eneo la karibu na tukio wakati imezama na masaa kadhaa toka imezama.. Hivu vitu ni basic inatakiwa tufanye tulinde usalama wa watu wetu na tuwe more professional dunia isije ikawa inatu dharau kila siku.
 
Pesa ikipatikana matumizi mapya yanajitokeza hahahaa
Mbona tayari watakuwa wameshayapata!! Unaweza ambiwa inatumika kuvuta maji kutoka ziwa victoria kwenda dodoma ili kuyapunguza kwani yamekuwa mengi sana, ndio maana ajari zimekuwa nyingi!! Hahaaaa! Hawa magamba ni shida kwa sanaa!!
 
kwa nilivyoelewa, Nahodha na mkuu wa kivuko ni miongoni mwa waliokufa, Nahodha aliyekufa ni deiwaka ila bado anaitwa nahodha maana ndio aliyekuwa responsible wakati chombo kinazama. Nahodha mwenyewe muajiriwa kama nahodha na anyetambulika na mamlaka kama nahodha halali wa kivuko hakuwa onboard alikuwa onshore.. Ni shida zile zile za wabongo kuwa wazembe kwenye kutimiza majukumu.
Nimekuelewa
 
Unafikili watu wangelijua wanaenda kufa nani angepanda kivuko,tumefichwa kifo na nauhakika angekuwepo MTU akawazuia hao ndugu zetu kupanda ,pangechimbika vyombo hivi navitumia Mara kwa Mara sisi abiria ambacho huwa tunajari nikuwahi basi bira kuangaria kuwahi bila kutathimini mazingila harisi ya usafili je kwawakati huo ni salaama,hivyo basi wewe unaelaumu ulitakiwa kuchambua kila hatua ,nikueleze tu acha mungu aitwe mungu katuficha kifo.
 
Kuwajibika ni moja ya tabia ya kiungwana hivyo tunamuomba huyo waziri awajibike kwa kujiuzulu kwa maafa yaliyo tokea chini ya wizara yake.
 
cha msingi ni kwamba
KIVUKO CHA POMBE kimeua, alikinunua mwaka 2004 akiwa waziri wa miundo mbinu, tukumbuke pia pombe alinunua kivuko kingine kibovu cha MV DAR ES SALAAM..
pia pombe kajenga hosteli mbovu za mlimani..
roho za watanzania zinatolewa kafara na huyu mwanasiasa..
Toka mwaka 2004 mpaka leo miaka mingapi?
 
Sitasahau zile rambirambi za tetemeko, walipozichukua na kwenda kujengea ofisi za CCM, na kukejeliwa juu badala ya kufarijiwa. Hadi leo wahanga wa lile janga wanateseka na hakuna anayejali.

Watu watoe rambirambi lakini zisiingie mikononi mwa hii serikali. Wapewe wahanga moja kwa moja, uwekwe utaratibu.
 
mpaka kufikia hpo braza Mmawia, tufafanulie kwa nini umeona ni vzr wazir aajibike?
 
Wewe ni zaidi ya kilaza mkubwa unabishana kama zuzu au kichaa wakati hiyo hotuba ya mbunge wa ukerewe bungeni ipo na clip yake ipo,wacheni masihara kwenye msiba mkubwa kiasi hiki
Yote aliyoyasema kwenye press ya Jana ni uongo mtupu. Mbunge wa Ukerewe kuweka kula kitu hadharani soon kuhusu hoja take ya kivuko aliyoitoa bungeni. Stay tuned nitawajuza kupitia hapa hapa!
 
Dah inauma sana ila nawaza tu tamko la RC isiwe ishu kiasi hicho, ni makosa ya kibinadamu, lakini pia nahisi alihofia maisha ya waokoaji, maana kwenye Maji kuna mamba, chunisi etc so may be alohofia waokoaji kwenye Giza kudhurika
Bado aliweza kuwapumbaza wananchi wakatulia. Kuna mangap serikali inawaongopea wananchi na wanatulia?Wangeweza hata kushinda huko majini na vifaa vyao lkn sio kuwaambia watu wanaosubir ndugu zao et tutaendelea kesho
 
Mbunge wa ukerewe ndugu Joseph Mkundi amesema kuwa Kivuko hicho kilifanyiwa ukarabati miezi miwili iliyopita, hivyo kilikuwa sawa na kilikuwa mbioni kubadilishiwa ratiba ikiwemo kuongeza idadi ya safari ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa eneo hilo.
Aidha, amesema kuwa yeye mwenyewe ni miongoni wa watu waliopoteza ndugu katika ajali hiyo ambapo amedai kuwa takribani ndugu zake watatu wamefariki kwenye ajali hiyo.
 
"Ndugu zangu mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha MV NYERERE,tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito,
mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.
Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.
Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema
na sisi abiria tujiongeze
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,
ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,
watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.

Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje

kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa,,walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.
nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao...fikisha salam mimi

John Kisekwa.
Pole sana mkuu.
Honestly speaking Mimi hata ningekuwa nipo juu huko nikarushwa majini siwezi ogelea hata sekunde walah!
Mungu atuepeshe tu na hongera kwa kuokoka.
 
Naona leo akili imekurudia sasa unaongea kizalendo badala ya kuongea upupu,nakupongeza
Hatuwezi kubali uchafuzi kwa wasio na hatia ,uzembe wa wachache serikalini ,usisababishe serikali nzima kulaumiwa,
Mbunge aweke wazi nini kilifanyika (hatua) baada ya kuiomba serikali kufanyia kazi ombi lake ,tusipepese macho,nongwa zimezidi mno
 
Yaani watu wote hao wamepoteza maisha mita chache kutoka nchi kavu tena mchana. Tuko nyuma sana kwenye suala la uokoaji na umakini. Hivi hawa wanajeshi wa navy naowanaga kwenye magwaride kazi zao ni nini sasa? Kweli walishindwa ku deploy rapidly kikosi kidogo na vifaa kuokoa watu?
 
Back
Top Bottom