The Boldly
JF-Expert Member
- May 21, 2017
- 2,377
- 5,147
Nimewahi siti
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wanadai eti kakutwa kajipaka oil mwili mzima duh hi inamana gan sasaSiku mbili ndani ya maji nitakuwa wa mwisho kuamini alikua miongoni mwa waliozama na hicho kivuko....
Unaposema serikali haina lawama ya moja kwa moja huku ukidokeza ajira za kubebana sikuelewi hapo. Ni Nani aliyewaajiri hao mafundi wa kubebwa? Nadhani ni mmiliki wa meli, Nani mmiliki wa meli serikali, Then serikali haipaswi lawama. Wamiliki wa mabasi yanapopata ajali za kizembe kama hii wanashtakiwa pamoja na watumishi wao hasa pale watumishi wao wanapokuwa hawana baadhi ya sifa, lakini kwa serikali haipaswi kulaumiwa kwa mujibu wa maoni yako!! Serikali inapokea mapato ya abiria 250 kila siku kwa kivuko chenye uwezo wa kubeba abiria 100, inachekelea vinono vinavyoingia bila kujua vinatoka wapi? Yaani baba mwenye nyumba unamwachia mkeo hela ya dagaa mchana ukirudi unakuta mama kapika nyama ya kuku unakula kwa raha zote huku ukisifia ubunifu wa mkeo, kesho akifumaniwa na mume wa mtu hustahili lawama!!Simtetei mtu, serikali haitakuja jikoni au chooni kwako kukupigia kelele kuhusu usafi ili usipate kipinduapindua, au ofisini kwako kama hutawajibika kikamilifu utakuwa unaishi na janga ambalo siku moja litachoka kukuvumilia…
ni hali hii ya kutokujari na kuishi kwa mazoea badala kwa umahili wa kazi yako ndio kunakopelekea majanga kama haya…ni wazi kuwa hawa wafanyakazi wa kivuko hicho na vingine vingi…na hata kwenye mabasi/magari, hali wakijua madhara yatokanayo na kuzidisha mzigo ukilinganisha na uwezo wa chombo ktk taaluma yao ya usafirishaji wanaleta mzaha na kuzoelea mzaha…na kama wahenga walivyosema…'mzaha mzaha hutumbua usaha' haya yametimia kwa manahodha na wote wanaoendesha Mv Nyerere 'wamekibinua na kuwaua hao waliokuwa wanawasokomeza kwenye kachombo hako! Serikali haina lawama ya moja kwa moja ktk hili bali kuna watu waliopewa kazi ya kuiendesha Mv Nyerere ndio waliotuangusha kwa kuibebesha zaidi ya uwezo! Inawezekana hata ktk uteuzi au uajiri wa wataalamu hao walipitia njia ya panya na hivyo kutokuwa na sifa sitahili!
Aaaaah rafiki kwanini ulihamakhaaa hv upo? Mana nilitaka nikufungulie uzi wa kukutafta, Au upo MMU mana kule nilishahamaga
Huyo Zwazwa naye wa kumsikiliza?Nimeacha kuendelea kunsikiliza Kangi Lugola TBC, badala ya kueleza miakkati na kuongeza nguvu za uokoaji anaanza mipasho.
Kuwa kuna watu wanasema serikali haitaweza kuokoa watu etc.
Hawa jamaa akili zao sijui zipoje
Ndugu yangu Coaster2015 sijui unamaanisha nini unaposema nanufaika...maana kama vile mtz yeyote anayepambana kwa kudra za Mwenyezi Mungu ndivyo nami nafaidika!Sio chuki Hero, hiyo ndio hali halisi kwa sasa hapa nchini, Mwl nyerere aliwahi kusema, Tunahitaji Utawala Bora, Siasa safi na Watu ili kuyatafuta maendeleo ya kweli, sasa hivyo vitu vikikosekana mambo yanakuwa sio sawa, inawezekana nyie wanufaika na mfumo huu mnaona Sawa tu.
Kwanza napenda kutoa pole sana kwa msiba mkuu uliowapata ndugu zetu wa Visiwa vya Ukerewe na Ukara (UK)baada ya ajali ya Meli ya MV Nyerere. Huu ni msiba ambao umewagusa Watanzania wote bila kujali itikadi zao za Kidini na Kisiasa.
Hata hivo katika mazingira yasiyoweza kuepukika lazima tuseme kuwa CHADEMA watakuwa wameathirika kwa kiwango kikubwa sama kwa vile hii ni ngome ya CHADEMA kwa maana ya jimbo la CHADEMA ambapo Mhe. MbungeJosedph Mkundi ndiye chaguo la Wana Ukerewe.
Mhe. Mkundi aliwahi kuzungumzia ubove wa MV Nyerere lakini kwa vile ni Mbunge wa CHADEMA Serikali na CCM yake walimpuuza kuwa hana hoja kwa vile yeye anatoka upinzani!!!
Tumemsikia Mhe. Rais akitoa salamu za rambirambi na maombolezo ya siku 4 kwa msiba huu mkubwa na akaonya kwamba Wanasiasa wasitake kutafuta KICK za kisiasa kutokana na ajali hii. Sijaelewa Rais ana maanisha nini watu kutafuta kick za Kisiasa....?!Maana kama Watanzania na Wanasiasa wana anza kuhoji kwanini ajali imetokea wakti tayari kulikuwa na viashiria vya Kivuko cha MV Nyerere naMbunge wa eneo husika alipeleka taarifa hiyo Mwezi April, 2018(mwaka huu)Bungeni lakini haikufanyiwa kazi....1!!
Leo ajali imetokea Watz na Wana- UK wanahoji kulikoni lakini Raisi anawaambia Wanasiasa waache kutafuta kick za Kisiasa...!!!Hivi nani anayetafuta Kick za Kisiasa hapa? Je, ni Mbunge aliyepeleka hoja hii Bungeni kabla ya ajali kutokea au ni Serikali ambayo haikuchukua hatua kuzuia kuzuia ajali hii isitokee au ni Rais anayeanza kutoa vitisho kwa Watanzania na Wanasiasa wasihoji, kudadisi na kukumbushia alichosema Mbunge wa Jimbo husika??
Angalia hotuba ya Rais Magufuli akiwa Ukerewe hivi majuzi tarehe 4 Septemba, 2018. Magufuli hakuzungumzia lolote kuhusu hichi Kivuko cha Ukerewe.....Hii hotuba ni sawa na kula matapishi...maana hapa anaponda Wabunge wa Upinzani akiwemo Mbunge wa UK kuikataa Bajeti ya Serikali hivyo HASTAHILI KUPEWA MRADI wowote ukiwemo huu wa kukarabatu au kukibadilisha Kivuko cha MV. Nyerere kilichpata ajali. Je, nani anatafuta kick hapa?
Dhambi ya Ubaguzi wa Itikadi za Kisaisa inalitafuna Taifa......Hatari sana.
hatutakiwi kua wavivu wa kufikiri mwisho hata hao waliochangia utasema wanafanya siasa.Nimeandika nimefuta nimeandika nimefuta ila tusaidiane hapa ccm ukara wanafanya nini? Wameweka kambi na jezi yao ya kijani ila marufuku kwa wengine kusema juu ya msiba au kufanya lolote ni uchochezi kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani.
Na marufuku kisema serikalo inahusika na kizama kwa kivuko maana serikali haihusiki na haikuwapakia hao melarehemu