HORSE POWER
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 2,238
- 1,577
Habari wana JF.
Kwanza kabisa niharakishe kutamka hapa kwamba sipingi viboko mashuleni.Viboko 'huamsha' wazembe,halikadhalika husaidia kurekebisha nidhamu'kwa kiasi fulani'. Lakini adhabu ya viboko ina namna yake na idadi yake.Lengo la viboko ni kunyoosha na sio kukomoa.
Tatizo tulilo nalo leo ni lundo la walimu makatili mashuleni wanaonyuka fimbo watoto mashuleni utadhani wanaua nyoka.Udhalimu upo shule nyingi nchini ila 'wakubwa' wetu kama kawaida wapo kimya.
Moja ya shule inayolalamikiwa sana ni Shule ya Sekondari Salma Kikwete iliyopo Dar.Kuna binti wa rafiki yangu wa karibu ametandikwa viboko zaidi ya kumi mpaka amevimba makalio kisa hakwenda na hela ya mtihani.Malamiko ni mengi kuhusu shule hiyo na ukatili wao na hakuna hatua zinazochukuliwa.
Nataka niwakumbushe wakubwa wetu wanaozembea kwenye mambo ya hatari kama haya;ipo siku wazazi wataamua kwenda kuwashughulikia wenyewe hao makatili pale shuleni.Sasa hatutaki watu wafikie huko.DC,Mkurugenzi,Afisa Elimu,Bodi ya Shule,Mwenyekiti wa S/Mtaa na Mtendaji wake,Diwani,Mbunge na wengine;je ni kweli hamjui au hamjali?