Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Hivi mnadhani ccm ni chama chepesi sana??? Hebu jaribuni kama mtaweza, mkipata hata nusu ya kura mimi nitakuwa wa kwanza kujitoa ccm.

Mandla.

We ni njaa tu, nani anajali kama unajitoa au unabaki CCM...

Bilioni 200 Mwigulu Nchemba alizopiga juzi na IPTL ndio zitaipeleke CCM kaburini. Mwigulu na wenzie wameiba bilioni 200 na mgao wa umeme unaendelea bila ratiba. Vijana hawana ajira wanaishie kuendesha bodaboda, wakulima wanakosa pembejeo vocha zote mnagawana mafisadi. Hospitalini hakuna dawa, wajawazito wanajifungua sakafuni. Sasa CCM itachaguliwa tena kwa kipi ilichowafanyia watanzania?

Tunajua mmeanza kuua Albino kupata ushirikina wa kushindia uchaguzi lakini safari hii Mwenyezi Mungu atasimama upande wa haki kwa ajili ya watu wa Jamhuri ya Tanganyika na watu wa Jamhuri ya Zanzibar
 
Pigeni mahesabu ya kula zote za vyama vya ukawa 2010 kisha mlinganishe na za ccm mtapata majibu, msione watu wanajaa ktk mikutano, muulizeni Mrema walikuwa wanalisukuma gari lake for long distance.
Nawaahidi mtagawana mbao baada ya uchaguzi.

Nani asiyejua kwamba Mkapa alipigwa chini na Mrema ila CCM ikatumia ubabe?

Tiba
 

Kwa bandiko hili, nitapendekeza kwa Nape uongezewe book zingine 3 ili upate kumi leo.

Tiba
 
na ndiyo kitakachofanyika mkuu na kwenye kampeni tunabkisapoti hicho chama...

Naona Chadema imenogewa na ndoa ya CUF mpaka inataka kuachia majimbo ya ubunge na urais 2015.
 
Mtatiwa adabu pamoja na kuweka mgombea mmoja kura zenu zote wanaukawa hazifiki hata robo ya kura za mgombea wa ccm,mnasikitisha sana mnadhani ninyi ndiyo mnafikiri peke yenu kumbe hata wenzenu wanafikra pia wakati ukifika majibu mtayapata tu.

Ccm haina mgombea wa kupambana na Dr Slaa, hata 2010 milichakachua. Kama kutakuwa na tume huru mtajificha mapema sana. Mark my words!
 
Ccm haina mgombea wa kupambana na Dr Slaa, hata 2010 milichakachua. Kama kutakuwa na tume huru mtajificha mapema sana. Mark my words!
Watanzania hawana imani na hiki kibabu
 
Mf Pinda na wengineo,kwani kuwataarifu wananchi kuhusu katiba mpya sio muhimu!Ukawa nawapa big up acha magamba waendelee na sera zao za kuuza nchi
 
Heko na pokea heshima zako mama Maria Nyerere kwa kuwaumbua makondana vibaraka wenzie kwa kuipeleka nchi kubaya
 

Umemwambia ukweli. Ukweli tutakao usimamia mpaka mwisho.
 
Andika tu Kiswahili.
Uwepo wa upinzani imara ndio chachu ya maendeleo kwa kuimakinisha CCM na kuipa tumbo Joto. Msiubeze upinzani wote tunanufaika nao

Kuhusu mgombea mmoja. Naona ni jambo lililoibuka bila plan. Tuliwaona CUF km wenza wa CCM hata kuwatusi.
Mbatia na NCCR CCM B. Hapajawahi kuwa na mchakato wa kuona vipi tunaweza kuoanisha sera ili tuwe na mgombea mmoja. Itatekelezwa ipi mwishowe? Au vyama havina sera za kisiasa kiuchumi na n.k?

Kuna utafiti kuona vipi itaathiri kura za CUF Pwani iwe hasi au chanya? CDM kwa ujumla je?
Mgombea mmoja limekuja kwa sbb ya katiba mpya sio kwa sababu ya mipango makini ya kuoanisha shabaha za vyama kuwezesha hilo.

Nadhani linatumika km namna ya kuwaonyesha wananchi kuwa UKAWA ni wamoja lakini sioni wao kuwa wamoja ktk suala la uchaguzi. Kuna kazi ya kufanya.

Inaweza kuwa na athari mbaya sana km umakini utakosekana ikatokea wakashindwa kuelewana.

Tusiishi kwa matukio tuishi kwa mipango. Kasoro hizi zirekebishwe haraka.
 
Wakuu,tumemsikia Dr Slaa mwishoni mwa wiki hii akitamka kwamba UKAWA itamsimamisha mgombea mmoja kwenye urais..

Toa pendekezo lako ungependa nani awe mgombea ticket ya Urais na mgombea mwenza wake..
 
Pigo gani? Ccm toka vimeingia vyama vingi ccm aijawai kushinda kiuhalali

uhalali UPI mkuu wa kisheria au!? vipi kalenga na chalize? tatizo let tuna wa-underestimate mno, Kiu yetu ya kupenda mabadiliko imetufanya tuwe vipofu wa kuto ona hasa mbinu za kukabiliana na adui zetu.tujipange safari bado ni ndefu hii
 
Ukawa wana wafuasi wengi sana, na watachukua viti vingi 2015 kama umoja wao utadumu na wataendelea na hii spidi.

Kuhusu urais, Dr asahau, ndani ya UKAWA kuna wengi wenye uwezo.

Anaweza kuwa Tundu Lisu na mgombea mwenza akawa Jusa kwa sababu ndio wenye sauti kuu kwa sasa ndani ya ukawa. Isingekuwa umri, David Kafulira angefaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…