Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Urafiki wa wanasiasa huwa ni wa mashaka siku zote, hivyo mpaka ifike hiyo 2015 niwaone wakisimamisha huyo mgombea ndo ntaamin.
 
Nilidhani teyari kumbe wana mpango hapo baadaye! Wakiwa teyar nipatieni kadi namba moja!
 
tatizo watu hawataki kujua malengo ya cdm.cdm hawataki kutawala wanataka kumletea maendeleo.Tofauti na CCM ambao wanaamini wao tu ndio wana akiki timamu
Maendeleo yapi unayaongelea kufungua viwanda vya gongo.
 
Nitahama hii nchi kama hiyo ndo safu ya uongozi!Khaa!
 

....now they are talking....njia pekee ya kuwatoa ccm madarakani ni kwa UKAWA kuunganisha nguvu zao zoote....na kumweka mgombea mmoja tu anayekubalika na vyama vyote vya upinzani...na pia kuweka wagombea ubunge wanaokubalika kutokana na maeneo na vyama vyao vya upinzani.....ni kwa njia hii pekee UKAWA wataongeza wabune bungeni...na hivyo kuweza kuwadhibiti ccm.....na pia kwa njia hii wataweza kushinda hata urais.....

....kama kweli UKAWA wameamua hivi nawapongeza sana.....maana ni kwa kuungana peke yake watawatoa ccm....katiba mpya iwe chachu ya kuwaunanisha na wasirudi nyuma....waache ubinafsi na tofauti zao....wajifunze Kenya walivyoitoa KANU madarakani.....

...Finally.....wakina Mbowe (Hai)...Lipumba(Tabora) na Mbatia(Vunjo) wasigombee urais....wao waende majimboni mwao wakagombee ubunge...hata kina Mtatiro woote wajipange kugombea ubunge....wakipata ubunge watakua na nafasi za kushika uongozi wa juu kama watashinda uchaguzia wa urais kama UKAWA.....kwa urais UKAWA waandae watu makini(mithili ya kina Lissu ama Dr.Slaa)...na kule Zenj yupo tayari mtu makini (Maalim Seif)....Kwa kufanya hivi kuna uwezekano mkubwa kabisa UKAWA wakawatoa ccm madarakani come 2015.....acheni ubinafsi....unganeni hadi kieleweke....bila hivyo ccm haitoki madarakani kamwe.....mmeona wanavyowasumbua bungeni....jifunzeni......badilikeni...
 
Nilishawahi shauri vyama viungane lakini CHADEMA wakatupuuza, kuwa wao wapo vizuri 2015 lazima wachukuwe nchi. Nashukuru sasa wameona kuwa bila umoja CCM kutoka madarakani ni ngumu.
 

kwanzia hapa tunaweza kuzungumzia Kifo cha CCM
... umoja ni nguvu..
Si CHADEMA ,CUF wala NCCR wanaweza kuing'oa CCM Bila kuungana .
Hatua ni nzuri saana
 
Kwa ufupi ni kuwa siku watakayofanya makubaliano hayo asubuhi, mchana tu wataanza kuyakiuka na watakufa kwa pamoja kwenye kapu lao!Hata huu ukawa wenyewe hauwezi kuwa kitu kimoja cha kudumu kwani muda si mrefu bajeti zitafika kikomo!na hawawezi kuendelea kutoa pesa mfukoni mwao au kwenye vyama vyao!nani hakujua kuwa UKAWA walisusia vikao vya katiba zikiwa zimebaki pungufu ya siku 4 tu za malipo?na BMK likianza mwezi wa 8 watahudhuri kuanzia kikao cha kwanza ili wapate posho!!Wote hawa wanapigania matumbo yao tu,sioni madhara yoyote ya muundo wa sasa wa muungano kwenye maisha yangu ya kawaida, wala sioni faida ya muundo wa serikali 3 kwenye maisha yangu hata ikiwa serikali 1 sitaathirika!Labda kama naota ndoto sa kuwa mwanasiasa (ndoto ambayo bado sijaiota) ndio nitakomaa na serikali 3 ili vyeo viongezeke na mie niambulie!Kwa jembe nitakomboka na kwa amani nitaneemeka Full stop!
 
endeleeni kujidanganya tu hicho ni kifo cha mende
 
Kazi ipo navyomjua Dr.Slaa na Lipumba kila mmoja anataka kuwa mgombea na pro-Chadema hawawezi kumpigia kura Prof Lipumba, na pro-CUF hawawezi kumpigia kura Dr.Slaa.
 
sidhan kama wazo hili litapita kwan viongozi wetu kila mmoja ana ndoto ya urais
 
Yaani lipumba aache kugombea urais,slaa aache kugombea urais? Maalim seif aache kugombea urais? Jua litachomoza magharibi

Ha ha ha maana huyo Lipumba tokea 95 anauwaza Urais afu leo hii umwambie ngoja MBOOwe agombee si utani huo? Maana jamaa CUF km Museveni wa Uganda
 
Suala ni jema endapo hakutatokea umimi naana ndicho huwa kinawavuruga
 
tunataka tuwapime kwanza kwenye hili la katiba kama mtaweza,,,uchaguzi bado sana shughulikrni na katiba kwanza tuone kazi yenu, either isipatikane au ipatikane ya wananchi na c ya ccm

wewe ni mtawala au mashabiki wa chama twawala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…