Katika hali ya kushangaza Chadema kimeishiwa sera kabla ya uchaguzi ujao 2015. Walichokifanya viongozi wa Chadema ni sawa na Muislam kumkashifu Mkritu kuwa na Najisi au Kafiri kisha akakubali kumuoa au kuolewa na Mkristu huyo huyo na kusahau alivyokuwa anamkashifu. Je ni nani asiye kumbuka jinsi CUF & NCCR- MAGEUZI walivyo kashifiwa eti wameolewa na CCM?, Leo hii vyama hivyo vimekuwa visafi hadi kuungana nao?. Je baada ya vuguvugu la Katiba kupita vyama hivi vitaendelea kuungana na kutengeneza chama kimoja ama vitasambaratika na kusimamia Katiba zao?.
Wito wangu kwenu ni kuwa rudini Bungeni ili Katiba isitungwe kwa uharaka bila kuzingatia vigezo, tofauti na hivyo tutapata Katiba ya pande moja. Fikirini upya na punguzeni misimamo kwani muda uliobaki mkirudi tu kutakuwepo na mabadiliko makubwa. Msiseme wanakura pesa za Wananchi huku nanyi mlishazitafuna, hii ni sawa na kushirikiana kumchuna Ng'ombe kisha mkachukuwa kipande cha nyama na kusema " wale ndo wamekura nyama au ndo watakura nyama"
:rockon::rockon::rockon: