Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!

Lowassa aingie upinzani lakini awe Mbunge tu ili apewe uwaziri Mkuu achape kazi naomba Ukawa mchukue maoni ya wananchi
 
Naona huna nia njema na Lowasa.
Kwa maoni yangu UKAWA yatosha.
Ushauri wa bure kwa Lowasa: akapunzike, siasa kwake basi. Ya CCM ikimshinda kwenda kutangatanga uzeeni hakutamfikisha popote isipokuwa atajizolea aibu na kuporomoshwa zaidi.
Atapumzika either way, akiingia UKAWA au akibaki CCM. Bora apumzike baada ya kuwakwaza kidogo CCM!
 
Kwani Lowasa naye alitoka nje ya Bunge la Katiba?.... Kwa nini sasa asimame kwa tiketi ya Ukawa?

Sina hakika kama alitoka lakini jana kwenye mkutano wa CHADEMA,Monduli Ndg Bananga alisema anamkaribisha Lowassa ndani ya Chadema kwa kuwa mzee huyo anatafutiwa tuhuma ambazo sio za kweli na hata kwenye bunge la katiba, Mzee Lowassa hakuongea chochote maana hakubaliani na marekebisho ya kihuni yaliyofanywa na CCM.
 
Tafakarini upya tena kwa mapana yake.
Hizi ashki zenu zilizojitokeza sasa zitaisha mda si mrefu mtakapofungua macho yenu na kuangalia with High Definition eyes.
Luku Vere
 
Mkuu kwanza naomba nikuhakikishie mimi sio CCM!, ila kwa wengi humu usipokuwa CCM kwao lazima uwe Chadema, mimi sio CCM wala sio Chadema, sina chama.

Tatizo langu mimi ni kuwa mkweli too much!, baada ya CCM kumsimamisha JPM, then 2015 ni CCM tena na JPM ndiye rais wetu!. Upinzani hauna mtu wa kushindana na JPM!. Kama CCM ingemsimamisha Membe, then Lowassa akahamia UKAWA, upinzani ungeingia ikulu kama kumsukumiza mlevi!.

Pasco
 
Mimi sijui watakuja na sababu gani kwa uamuzi wa kumpokea Edward Lowassa. Lakini kwa vyovyote vile uamuzi huu ni lazima uchukuliwe with great precautions.

Hebu turudi nyuma kidogo mwaka 2000 kama sijakosea pale NCCR MAGEUZI kilipochukua maamuzi magumu kama haya ambayo CHADEMA inashuriwa kuchukua leo kumpokea mtu maarufu sana EL mithiri ya Agustino Lyatonga Mrema wa mwaka 2000 alipojiunga nao na wakampokea kwa mbwembwe nyingi.

Naogopa sana yasije yakakikuta CHADEMA kama kilivyoikuta NCCR Mageuzi kwani badala ya neema ilikuwa ni mwanzo wa kusambaratika kwa chama na kurudi nyuma hatua nyingi japo kilipata manufaa ya muda mfupi ya kuingiza wabunge wengi bungeni kwa sbb ya umaarufu wa mtu Huyo.

Natambua pia kuwa nyakati hazilingani na ni ukweli pia Mrema na Lowassa ni watu wawili tofauti na wenye hulka tofauti pia na hata umaarufu wao umejengwa ktk misingi tofauti, lakini muhimu sana upinzani ukajifunza tokana Na historia hii na ikumbukwe kuwa watu hawa wanafanana kwa kitu kimoja kikubwa kabisa, wote ni wana CCM wenye uchu wa madaraka!

Kiukweli binafsi sina tatizo na uamuzi wowote utakaochukuliwa na viongozi wetu juu ya aidha kumpokea EL au kutokumpokea ili mradi tu wajiridhishe pasipo hata chembe ya mashaka kuwa uamuzi huo utakuwa na manufaa kwa chama ya sasa na ya muda mrefu na baadae na si kuturudisha nyuma.

Aidha ni lazima kuwe na sababu rahisi kuelezeka na kueleweka kwa wanachama na wafuasi juu ya uamuzi huo wa kumpokea mtu aliye tayari alishajengewa taswira hasi mbele ya jamii kiasi ambacho japo ana ufuasi mkubwa lakini pia jamii kubwa inamwona kama ni mtu asiye msafi, asiye na maadili ya kiuongozi. Ni lazima hili liwe addressed kiukamilifu ili watu waelewe kisha watoe sapoti yao na kuvunja hoja za wapinzani wetu.

Tukumbuke pia kuwa CHADEMA hawa hawa waliwahi kumweka katika orodha ya watu wafisidi wa nchi hii kupitia "the list of shame" ya Dr W.P. Slaa ya viwanja vya Mwembeyanga mwaka 2007 km sijakosea. Sasa kwa hili ni sharti waje na maelezo ya kina Ku - reverse msimamo wao huo juu ya mtu huyu ili wanachama na wafuasi na jamii kwa ujumla ielewe na iwaunge mkono na kisha tusonge mbele kwa pamoja ili kuitoa CCM. Kwamba ni nini kimefanyika mtu huyu kawa msafi-tena hata kuwa mtu wa upande wao!!

Ipo kazi kwelikweli, lakini labda watafanikiwa na pia yeye mwenyewe EL kuuthibitishia umma kuwa,sivyo wapinzani wake wamfikiriavyo bali ukweli juu yake ni huu na huu na hivyo jamii ibadili mtazamo hasi juu yake!

Otherwise, tusisahau usemi huu, majuto ni mjukuu!
 
Lowassa aingie upinzani lakini awe Mbunge tu ili apewe uwaziri Mkuu achape kazi naomba Ukawa mchukue maoni ya wananchi

Naweza kukubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa kwa sbb umaarufu wa Lowassa na wafuasi wake watakaoamua kumfuata ni wazi kuwa atakuwa msaada kiasi kikubwa kwa upinzani. Akifanya hivyo, kuna possibility ya 90% ya majimbo yote ya mkoa wa Arusha na Manyara na mikoa jirani ya hii kwenda upinzani.

Tatizo ni kuwa hakuna guarantee kuwa upinzani utashinda kiti cha urais japo akitumika kumnadi mgombea uraisi wa upinzani, kuna uwezekano mkubwa wa kushinda na hivyo assumption yako ya yeye kuja kuwa PM ika materialize.

However, ni lazima upinzani na bwana mwenyewe kwa pamoja wauthibitishie umma pasipo shaka kuwa hahusiki na tuhuma za ufisadi zinazomkabili ili kuondoa taswira hasi aliyojengewa na wapinzani wake mbele ya jamii ili sasa aaminike na apate sapoti pana na kubwa zaidi!!

Hiki ndicho kikwazo cha EL na ndicho kigugumizi cha upinzani kuchukua uamuzi wa moja kwa moja na wa mara moja kumpokea!!
 

Wewe ndo umeongea ukweli,CCM imeoza na CCM wenyewe walijua hilo na hapo ndipo wakazichanga karata na kumteua Maghufuli, kwanza kanda ya ziwa karbia wote wapo nyuma ya maghufuli kwenye issue ya uraisi, na kule ndo wapiga kura wengi walipo, robo tatu ya watanzania wapo kule, kuteuliwa kwa Maghufuli kumeshusha sana mvuto wa Lowasa (ila wengi humu JF hawajui hilo), sa hvi stori nyingi kule zimezagaa wakimuongelea Maghufuli kana kwamba ni Mungu wao, na leo atakuwa Furahisha yaani ni shiida, namshauri Lowasa atulie tu asije kufa kabla ya mda wake....!!!!
 
Aise nami naunga mkono...EL atatufaa kuangusha hili joka ccm,ijulikane kumpa nafasi si kwamba ukawa hakuna bright man.
 
 
mtoa mada una mapungufu kidogo ya kufikri na kujenga hoja, japo hujajipambanua kwa kina na umedai huna chama lakini andishi lako linaonyesha dhahiri kuwa wewe ni shabiki wa team wa LOWASA amabaye ana shutuma kibao za Rushwa na kashifa ya Richmond ndiyo inayo mutafuna popote pale atakapo enda lazima gamba la richmond litaendelea kumutafuna. Lowasa hafai kuiongoza nchi hii hata kama atapitia upinzani bado hafai na UKAWA hawapaswi kumupokea na kumupa nafasi hiyo.mimi ni mwana UKAWA damu damu niliye choshwa na mfumo wa ccm kwa kila kona hata asimamishwe nabii lakini akiwa ndani ya ccm atakuwa mwinzi.
KWA NINI LOWASA HAFAI KUWA KIONGOZI KWA CHAMA CHOCHOTE.
Loawasa hafai kwanza ana kashifa ya Richmond inamutafuna ambayo kashifa hiyo iliibuliwa na wapinzani ambao leo hii unamushauri Lowasa akajiunge nao wakati wapinzani kwa mda tofauti wamemtuhumu Lowasa.
pili mbinu alizo tumia Lowasa kutangaza nia ilikuwa imejaa ufisadi na Rushwa kwa kila kona na lengo la Lowasa ilikuwa ni kufanya kila awezalo kuingia ikulu, hili ni kosa kubwa ambalo Lowasa hafai kuwa kiongozi ndani na nje Ukawa
Team iliyokuwa imemuzunguka Lowasa wote wale wana kashifa mbali mbali za rushwa na ufisadi na walikuwa kwa pamoja kila kona wakati anatangaza nia je akija ukawa ataasafishika vipi?

UKAWA WAKIMPKEA BASI WATANZANIA WATAKOSA IMANI NAO.
UKAWA ndilo tumanini jipya la watanzania kwa ajiri ya ukombozi mpya na kumuondoa madarakani mkoloni mweusi ccm, itakuwa ni aibu kwa ukawa wamuchukue Lowasa na pia apewe nafasi ya juu ya kugombea uraisi, Lowasa ni mtu ambaye anafanya kila means kuhakikisha anashinda jambo ambalo linaweza ku coast ukawa na kuwapa nafasi nzuri ccm kuweza kuwachafua ukawa kwa kumupokea fisadi aliye tukuka, pili ukawa hawa hawa kwa nyakati tofauti wanasema ccm haifai na Lowasa ni mwa ccm je watatumia maji ya aina gani kumuosha Lowasa tatakate machoni mwa watanzania.
tatu UKAWA dhamila yetu kuu ni kumutoa ccm madarakani ambapo jambo hili linaneda kutimia mwezi wa kumi, hivyo lowasa hatufai

kama ccm imeoza tayari na lowasa ameoza maana na yeye ni zao la ccm tena la mda mrefu, ifike hatua tukumbuke historia inasemaje mwaka 1995 Nyerere alisema kuwa Lowasa hafai coz ni fisadi, je iweje leo hii lowasa apewe nafasi ndani ya UKAWA.
 

SWALI

Lowasa ameomba kuingia Upinzani?
 
mawazo yako ni mazuri sana tunaungana na wewe kuwaomba viongozi wa UKAWA wafanye chini juu wampate Lowasa wakipuuza hayo mawazo hakutokuwa na njia nyingine ya kuitoa ccm madarakani, kwani kwa mikataba waliowekeana na nchi za nje hawatatupa hiyo nafasi tena
 
Point Muhimu hapa ni kumtoa kwanza nyoka ndani, vitu tutavipanga baada ya nyoka kuwa ametoka nje.

Angalia lakini huyo nyoka ni hatari akikuwahi umekufa. Chadema ni chama cha wezi hakutakuwa na ajabu kumpokea mliokuwa mkimuita mwizi,nia yenu sio kumkomboa Mtz bali kula kwa zamu. Kamwe hatudanyiki bora mwizi huyu mdokozi kuliko nyie majambazi mtaimaliza nchi kabisa na baadae kuanza kutuua
 
Angalia lakini huyo nyoka ni hatari akikuwahi umekufa. Chadema ni chama cha wezi hakutakuwa na ajabu kumpokea mliokuwa mkimuita mwizi,nia yenu sio kumkomboa Mtz bali kula kwa zamu. Kamwe hatudanyiki bora mwizi huyu mdokozi kuliko nyie majambazi mtaimaliza nchi kabisa na baadae kuanza kutuua. Hivi kwa akili yenu haswa ya bangi na viroba mnafikiria Lowassa anaweza kukubali kuwatumikia?
 
ACT acheni kupima upepo..kama mnamtaka Lowassa mchukueni tuu lakini hamna haja ya kumhusisha na chadema ili mpate feedback ya mawazo ya wananchi..makene alishaliweka hili suala wazi kabisa
 
Lowasa na UKAWA ni two immiscible solvents..Hawakai pamoja..Mmoja ni very polar na mwingine ni non polar

Lowasa ili ayeyuke kwenye UKAWA inabidi aloose polarity yake kwa kuitisha press na kueleza kinagaubaga nani mwenye Richmond na mchakato mzima ulivyokuwa.Aeleze ni deal ngapi amepiga akiwa serikalini na awataje wenzake na mbinu wanazozitumia.

Awataje wanasiasa walio nyuma ya wauza unga,wawindaji wa tembo,wauaji wa albino etc.Ataje mbinu wanazotumia CCM kuiba kura...Yani aseme kila kitu kwa ukweli wake ili waTZ waujue ukweli wa viongozi wao

Then aombe radhi kwa waTZ na kwa Mungu wake maana ufisadi walioufanya una uhusiano wa moja kwa moja/usio wa moja kwa moja na baadhi ya vifo vya watu hapa nchini na hapo ndio 'like will dissolve like'

Bila kufanya hivyo..UKAWA itakayompokea ijiandae kuanguka vibaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…