Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!

magufuli sijamsamehe kwa mambo haya mawili 1.nyumba za serikali ambazo viwanja vyake vinathamani ya billions yeye akauza nyumba millions ,,najua wengine watasema alipata shinikizo lkn kama mtendaji mzuri angejipambanua pale
.2. Meli ya ferry bagamoyo ya masaa sita ...haya mawili sikumuelewa kabisa......
 
Baada ya CCM kumsimamisha jembe Magufuli, Lowassa ahamie UKAWA kwenda kufanya nini?!. Kama CCM ingemsimamisha Membe, hata mimi ningeuka mkono hoja!. Lowassa hili analijua wazi na ahami ng'oo!.

Pasco
ingekuwa sawa kama angeshindwa kwenye kamati kuu .lakini sio kwenye genge la kamati ya maadili .na. Kikwete ni mwenyekiti.Pasco kumbuka pia Lowasa ana siri nzito juu ya sakataa la richmond kumhusu Jk kuwasiliana na makatibu wa wizara akiwa nje ya nchi kuhusu ualali wa kuendelea na richmond .nakuwacha kuwasiliana na waziri mkuu Lowasa .Pasco nakuaminia wewe nimjuzi katika habari na uchambuzi wa siasa .sitegemei usahau hili .so njia bora ya kuficha siri nikummaliza mjua siri .ili uwe salama .unammalizia wapi adui sirini kwenye kamati ambayo wewe ndio mshika bunduki.ukimwacha aje hadharani kwenye kamati kuu itabidi ukampeni ili amalizwa .ningumu na haswa tatizo likiwa ni lako sirini.fikiria .Pasco Karibu chadema aupendezi gweji kama wewe kujidai huko Neutral .karibu m4c .nafasi ya kazi msemaje wa rais Dr Slaa .karibu
 

Kuna tem Lowassa mzalendo?
 
ni ushauri mzuri huenda wenye tafiti ila wengi watacomment bila fafiti.ni mawazo mazuri na huenda bado mpinzani wa kweli atatoka ccm na huenda likatimia la baba wa taifa
 

Mawazo yako ni mazuri,unajua watu hawajui kama tunatakiwa kuondokana na mfumo CCM na tusipochezesha akili CCM itaendelea kutawala,ni lazima viongozi wajifunze kutumia lines of weakness huku wakijitenga na tamaa na ubinafsi.
 
Mkuu KILLERS KISS GUY, kwanza karibu jirani, nchi yetu yetu ni nzuri, ukiishajua tuu kuandika Kiswahili, unaandikishwa BVR. Mimi nimezipenda tuu hizi 'mu' zako!, karibu kwetu, na BVR ikipita pande zako, kajiandikishe tuu, hautashtukiwa!.

Pasco
 
Serena

Ulichoandika na kusisitiza ni kuwa:

Ikiwa UKAWA hawatompata LOWASA wasahau kushinda uchaguzi mkuu wa 2015.

Kwa maana rahisi ni kuwa umedharau kazi zilizofanywa na wapinzani hawa wa CCM. Unamaanisha miaka mitano ya kuimarisha upinzani imepotea bure.

Ngoja wenyewe waje.
 
Mkuu morenja, kwanza asante kwa sababu usemayo ni kweli, Lowassa anaijua siri ya Richmond na mimi niliamini ndio karata yake ya mwisho ya turufu ya kuombea uteuzi, lakini kilichotokea, JK ni mafia wa ukweli, amemchinjia kule kule chini, na kumpiga dafrau kwa kumsimamishia Jembe JPM!. Nilitegemea angesimamishwa Membe, Lowassa angevuka upande wa pili, na kuichukua nchi kama ameokota!.

Asante kunikaribisha Chadema, kiukweli siasa nazipenda, ila kwa fani yangu ya habari, ninapaswa kuwa neutral wakati wote ili kuweza kupratice impartiality kwenye kutimiza majukumu yangu. Uandishi wangu ni kwa kujitolea, mimi ni mwandishi wa mitaani, nimeishakuwa kama kuku wa kienyeji, sifugiki!, ila pia namkubali sana msemaji wa rais Dr. Slaa aliyepo sasa, anajitahidi sana, ila kuna vitu vidogo vidogo tuu vya kurekebisha akiishaingia ikulu!.

Pasco.
 
hahahahahahah......
munaijua ccm ama mnaiskia tu!! yan lowasa ahamie ukawa then ashinde?! ccm na ufisad wao wote lkn wamemkataa lowasa.......kwa kifup hashind na lowasa mwiz zaid ya ccm
 

A big concept...!!! naamini mpango huo ukijulikana CCM watamuua
 

Mm nakubaliana na mawazo yako kwa asilimia mia, mbona watu wanafikiria mambo mepesi sana? Hawafikirii kwamba ufisadi wake ndo umetufikisha hapa, wao wanachofikiri ni kuiondoa ccm madarakani tu, kama ikiondolewa na mafisadi ni faida gani tutapata? kama UKAWA hawatoshi kupambana na CCM basi waendelee kuwa wapinzani, hii nchi sio ya kuchagua mtu eti kwa ajili ya kutoa chama fulani. Kama UKAWA wana mawazo hayo mgando, basi nchi haiwezi kupiga hatua kwa utaratibu huo. Hivi pesa ya Lowasa alotumia kutangaza nia Arusha na kuzunguka Tz nzima, huwezi kujiuliza kazitoa wapi? Na kabla ya hapo alianza kampeni miaka mingi tu, akipewa mwaliko makanisani& misikitini alikuwa anatoa pesa nyingi sana. lazima tutafakari sana sana, na kwa sababu anapesa nyingi sana, akipewa nafasi UKAWA zile ndoto zao za kuleta maendeleo zitapotea kabisa, wala hatokuwepo tena kiongozi wa UKAWA kukemea jambo hilo, kwa sabu UKAWA itakuwa imetekwa na kundi hilo. Mm nadhani tuendelee na viongozi wetu wa UKAWA kwa maendeleo ya wanyonge.
 
Watanzania,
Hatimaye ombi langu kama thread hii inavyosoma inaelekea kutimia muda si mrefu. Nalo ni Lowassa kuingia UKAWA na kugombea nafasi ya URAIS. Nataka niwaambie UKAWA tena, hili ni pigo kubwa sana kwa CCM na wale wote wasiopenda kuona mfumo CCM ambao ni mfumo mbaya kupita yote duniani ikiondolewa madarakani. Naomba nirudie tena, kwasasa Watanzania wanatakiwa kumtoa mdudu CCM bila kujali nani mgombea wake, kwani CCM ni mfumo usio na tiba kwa mtu anayeshinda uongozi kupitia CCM.

Na kwa wale wote mliodhani Lowassa hana impact, sasa subirini muone mwisho wake. Pia niwaombe tu muache kulalamika sasa, si mlimtema kwamba hafai, na hata wale waliokuwa upande wake wote ndani ya CCM nao wanaangushwa kwenye kura za maoni (rejea Nchimbi, Pindi Chana, n.k.) ikiwa ni maagizo toka kwa Mwenyekiti wa CCM na Wazee wa Kitengo maalumu? Sasa mnalilia nini tena, kwani Lowassa ndio huyooo?

Yaani ni raha mstareheee kila kona kwa UKAWA, ebu jaribu kufikiria, Lowassa anapiga Kampeni sehemu moja ya nchi, Dr. Slaa naye anapiga kampeni sehemu nyingine, Prof. Lipumba naye ndani ya Nyumba, Lissu kama kawaida, Mbowe naye anapiga kotekote, n.k. Naomba CCM mje hapa mniambie huu mziki wa UKAWA utatulizwa na nani????? Je Mzee Pombe Magufuli na kauli mbiu yake SITAWAANGUSHA atauwezaaa?????? Thubutu yake.

Mbarakiwe sana, kwani hatimaye naiona Tanzania mpya nje ya mdudu CCM ikizaliwa chini ya mfumo mpya unaojali maslahi ya Watanzania UKAWA.
 

Magufuli hana jipya kama wenzake ndani ya CCM ndiyo maana ana kauli mbiu ya SITAWAANGUSHA, Je ni akina nani hao, kwani neno analotumia ni pana.
 
Baada ya Edward Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni Superman, namdurufu kidogo Lowassa kwa kujikumbusha niliwahi kusema nini kuhusu mtu huyu.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…