UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

[SUP]MTAZAMO KUHUSU HOTUBA YA RAIS KAMA ILIVYO KATIKA BANDIKO HAPO JUU[/SUP]

Bandiko la 3

(Kifungu AI)
Rais: Hili ni jambo zito nisingeweza kukaa kimya.
Watanzania wangeshangaa nini maoni ya Rais. Mimi ndiye mlezi wa taifa.
Hoja: Tume ilitambua kuwa wewe ndiye mlezi. Ilikufuata kukutaka utoe maoni yako.
Kwa mujibu wa majibu ya Rais (Kifungu AB) mazungumzo yako na akina Warioba hayakuwa ya kina.
Hivi mlezi ambaye leo umegundua uzito wa jambo hukuwa na la kusema wakati huo?

Watanzania wasingeshangaa Rais kwanini hakutoa maoni, jibu umeshalitoa (Kifungu AC)kwamba hukutaka kuingilia mchakato na kwamba(Kifungu A D)ulikataa kutoa maoni hata pale ulipoombwa.
(Kifungu AJ)
Rais: Kwa bahati nzuri nilitoa maoni yangu mahali penyewe, ndani ya bunge la katiba.
Hoja: Mh Rais ulikiuka sheria ya katiba inayoeleza utaratibu wa kutoa maoni.

Sheria hiyo uliyosaini haina mahali inapoelekeza kuwa baadhi ya watu watatoa maoni yao nje ya yale yaliyokusanywa na rasimu.

BMLK si mahali ulipotakiwa kutoa maoni yako, nafasi hiyo uliikataa.
BMLK ni sehemu ya kueleza uzoefu wako kama Rais na kulileta taifa pamoja kwa lengo moja.

Ulichokifanya ni kuligawa taifa kuliko ilivyokuwa kabla na hata katika historia. Rais ndiye chanzo cha matusi hasa alipowadhalilisha wazee wenzake.Ile dhana ya ulezi imekosa mahali pa kusimama.

(Kifungu AK)
Rais: Nilipotoa maoni yangu sikulazimisha au kushurutisha watu wayakubali.
Hoja: Kauli ya rais ni sheria . Kwa mujibu wa katiba ya leo, baada ya kura ya maoni atakayesaini katiba kuwa sheria ni Rais wa JMT. Hivyo Rais husubiri sheria ije katika dawati lake.

Katika bunge la katiba, Rais alisema ''S3 zisubiri aondoke'' Hapa ndipo pa kujiuliza, je hilo halikuwa kuwashawishi wajumbe kuwa kwa hali yoyote yeye hata saini hata kama wananchi wataridhia.

Kauli ya ''S3 hadi aondoke' zilieleza na kuelekeza kuwa katiba izingatie maoni yake na si ya wananchi vinginevyo hilo hataklikubali. Mh Rais hiyo ndio kulazimisha au kushurutisha na ulikuwa mwanzo wa tatizo


 
[SUP]MTAZAMO KUHUSU HOTUBA YA RAIS KAMA ILIVYO KATIKA BANDIKO HAPO JUU[/SUP]

Bandiko la 3

(Kifungu X)
Rais: Majadiliano ni muhimu bila hivyo uwezekano wa kupata 2/3 ya pande mbili haitawezekana.
Hoja: Mh Rais kama alitambua hili alipaswa kuondoa sintofahamu kuanzia sheria ya katiba ilipoanzishwa.

Mh Rais alisaini mswada wenye vifungu vyenye utata ukipingwa na Chadema. na kimoja ni hiki cha mamlaka ya BMLK.

Mswada huo ulishirikisha wabunge 100 wa JMT ambao ni chini ya akidi ya 2/3 kupitisha sheria.

Rais aliona kwavile CCM wanashinda aendelee, akasaini mswada uliokosa uhalali kwavile hakutaka majadiliano na wapinzani. Leo anasema majadiliano aliyoshindwa kuyafanya huko nyuma ni muhimu.

Lakini kubwa zaidi ni kuwa tayari ameshatambua kuwa 2/3 katika kura za maoni haitapatikana si Tanganyika si Zanzibar.Kwanini asisitishe mchakato huu ili tuokoe pesa.

Kwa vile hakusikiliza wadau kuanzia mwanzo, hili tatizo analo mabegani kwa muda mrefu.

Maisha ya Watanzania yapo mikononi mwake. Kila tone la jasho, maji, mate au damu litakalotoka, Rais hana namna ya kukwepa lawama.

Alianzisha mchakato, akauvuruga. Njia bora ni kuvunja bunge ili kupunguza madhara yanatoweza kutokea kama rasimu ya Rais na CCM itapitishwa.

Tuliyaona nchi jirani, hayakuja kama mvua. Yalianza vivi hivi.

(Kifungu Y)
Rais: Ombi langu kwa wanasiasa ni kutumia fursa ya mahjadiliano kuukwamua mchakato
Hoja: Rais alikaa kama mwenyekiti wa CCM na kuwafunga wabunge wake midomo, hakuwa anakwamua mambo.

Leo ndani ya CCM wapo walio tayari kuridhiana na wenzao, lakini hawawezi kwasababu huo si msimamo wa chama.

Mwenyekiti anataka majadiliano, chama chake kikiwa na msimamo imara usiyoyumba.
Hii ni nini kama si bla bla bla.

Maridhiano ni kuja kati na kati ili kukubali kutoa au kupokea katika hali ya muafaka.
Viongozi wa CCM akina Vuai, Nape, kinana na wengine wanasema kwa uwazi sera ya CCM ni S2.

Leo mwenyekiti wa CCM anasema maridhiano yanawezekana.

Maridhiano yanawezekanaje ikiwa ndani ya CCM hakuna maridhiano ni miguvu tu.

Maridhiano maana yake ni UKAWA wakubaliane na hoja za CCM.
Huu uhalali, mwenyekiti wa CCM anaupata wapi?

Kwanza arudi ndani ya chama, akemee wahafidhina na asafishe kauli za kibaguzi za viongozi wake. Halafu aruhusu wabunge wake wawe huru. Akimaliza aje kutaka maridhiano.

Tutaendelea na sehemu ya 4

Tutajadili kwanini rais anaegemea katika kanuni.

Bandiko la 5
Tutamalizia kwa kujumuisha nini alichokusudia, nini mkakati wake, wapi atafaulu na wapi atashindwa.
[
 
[SUP]MTAZAMO KUHUSU HOTUBA YA RAIS KAMA ILIVYO KATIKA BANDIKO HAPO JUU[/SUP]


Bandiko la 4


(Kifungu )

Rais: Amesisitiza UKAWA kurudi bungeni na kutumia kanuni zilizopo kumaliza tatizo.


Hoja: Mh anafahamu mgogoro wa kanuni ulikuwa mkubwa kuanzia awali.

Kanuni hazikukamilika kwa vifungu kama kile cha kupiga kura.


Kwasasa kuna makundi mawili, kundi la kura za wazi na siri.
Rais anajua msimamo wa CCM wa kura ya wazi kuwadhibiti wabunge na kuwanyima uhuru wa maoni
Msimamo huo haukulegezwa na umebaki kama ulivyo.

Leo anapowaomba UKAWA warudi bungeni kutumia kanuni zile zile zenye mgogoro ni kuhamisha mgogoro kutoka uraiani na kuupeleka bungeni bila suluhu.


Mh anafahamu kanuni zilizopo haziheshimiwi na wabunge wa ccm.
Kwa mfano, mwenyekiti wa bunge alikaidi maagizo ya kamati ya uongozi ya bunge kuhusu nani anze kuhutubia kati ya JK na Sitta.


Rais alifahamu hilo lilikuwa ni kuvunja kanuni,alikubali kwasababu lilimpendelea katika azma ya kuwanyanyasa wazee wa tume ya Warioba.


Hali ilikuwa ‘tense' kiasi maafisa usalama walitanda bungeni ili kuhakikisha UKAWA hawatoki bungeni. Kanuni hazikuwa na maana kwasababu zilivunjwa na Sitta kwa kushirikiana na Rais.


Mh anaposema UKAWA warudi kutumia kanuni alizoshindwa kuziheshimu na Sitta ni kuwadharau.


Pili, kanuni zinaeleza kuhusu matumizi ya lugha ndani ya bunge.

Sote tulishuhudia lugha za matusi, kashfa, kejeli , kuligawa taifa katika Uarabu, Uhindi, n.k.


Hakuna kiongozi yoyote katika ngazi ya BMK au taifa aliyesimama na kukemea jambo hilo.
Rais kama mlezi wa taifa alipaswa kusimama na kukemea. Hakusema hilo.

Mlezi wa taifa letu alishindwa kumkemaea waziri Lukuvi, akifanya uchochezi ndani ya kanisa.


Rais hakuweza kutumia sheria za nchi ndani ya katiba na mamlaka kukemea uovu.
Ni vipi aamini kanuni ambazo ni taratibu zisizo za kisheria zinaweza kuleta muafaka.


Inawezekanaje uhuni huo ushindikane, tuamini kurejea UKAWA kutaondoa tatizo kutumia kanuni.


Uhuni huo wa matusi, kejeli na ubaguzi ulifanywa na CCM kabla na baada ya kuondoka UKAWA. Rais hakuliongelea katika hotuba yake kutoudhi wahafidhina wa CCM.

Vipi kurejea kwa ukawa kutaondoa tofauti kwa kutumia maandishi yanayoitwa kanuni.


Kanuni ni maandishi tu, kinachotakiwa ni dhamira ya kuyaheshimu maandiko hayo.


Rais na mwenyekiti waCCM hakuweza, Sitta hakuweza, wajumbe wa CCM hawakuweza.

Leo tunawezeja kusema eti kanuni zitumike kwa UKAWA ili kuondoa tofauti.

Huku kama si kujidanganya ni kitu gani.


Inaendelea sehemu ya 5 na mwisho.


 
SEHEMU YA 5 (A)

MAJUMUISHO YA DHAMIRA YA HOTUBA YA JANA


Hotuba haikuwa na ufumbuzi wa tatizo bali kujivua lawama anazoelekezewa Raia. Hakufanikiwa kwani njia alizotumia hazikuwa sahihi.

Hotuba ilijaa upotoshaji dhidi ya UKAWA haina lengo la kuleta taifa pamoja.

Rais ameshindwa.


Pili, Rai alilenga kuwasema wazee wa tume. Ingekuwa busara angekaa kimya.

Wazee wa tume wamesema waliongea na rais kila hatua.


Jibu lake kuwa maongezi hayakuwa ya kina linaacha maswali.

Lakini itakapotokea tume ikathibitisha kina cha maongezi, mheshimiwa atakuwa amepoteza heshima.


Tatu, lengo lake lilikuwa kuwashitaki UKAWA kwa wananchi kama kikwazo cha katiba.

Amedanya kwa kutumia njia za kanuni, na kukwepa kiini cha mzozo.


Kiini ni muundo wa serikali ambao ameongelea mstari mmoja tu.


Katika mstari , amesema hana tatizo na muundo wa S3 akisahau aliwahi kusema S3 zisybiri aondoke. Rais hawezi kuwa na kauli tata akiwa mlezi wa taifa.


MBINU ZA CCM

Rais anataka kikao kiendelee baada ya mashataka yake dhidi ya UKAWA kwa wananchi.

Anafahamu akidi ya kuendelea itapatikana kwani inahitaji nusu ya wajumbe.

Wajumbe wa CCM tu wanatengeneza nusu ya akidi. Hilo litafanikiwa


Tatizo ni pale inapohitaji 2/3 ya kila upande.

Kwa upande wa Tanganyika itapatikana kwasababu CCM wanaburuzwa tu hata kama kuna mnada wa wa kuuza nchi hii. Kwa upande wa ZNZ 2/3 inakosa wajumbe 16.


NJIA ZA KUPATA 16 YA WAJUMBE WA ZANZIBAR


Kunajitihada za kurubuni wabuge wa ZNZ ili wapatikane 16.

Tatizo wanalokumbana nalo, wapo wabunge 9 wa CCM kutoka znz wasiokubaliana na mfumo wa S2. Hap itakuwa na kujaza maji katika ndoo inayovuja.


Pili,njia ya kuwapendeza Wazanzibar ili wakubaliane na mfumo husika.

Tumemsikia mara nyingi Sitta akisema yapo mazuri kwa wazanzibar ndani ya katiba.


Siku za karibuni kumekuwa na maoni ya katiba kujadiliwa kwa mambo mengine bila vifungu cha kwanza na Sitta.
Hili limelenga kuwapendeza wazanzibar, mwisho wakubaliane na muundo wa S2

Hoja zitajengwa kuhusu utayari wa JMT kutoa nafasi zaidi kwa wazanzibar katika uongozi, kuongezeka kiwango cha fedha kwenda Zanzibar na kuwapa upendeleo katika maeneo kama ajira, elimu, ardhi n.k wakikubali S2. Hoja zitajengwa kuonyesha watakachokosa wznz kwa S3.
Ili mradi kuwapendeza
 
SEHEMU YA TANO (B)
MATATIZO YA NJIA WANAZOTUMIA JK& CCM KUENDLEA NA BUNGE


Njia zilizotajwa 1,2 zitafanikiwa kiwango cha BMK, rasimu ya yao ya CCM itapatikana. Hata hivyo kuna matatizo mawili yatajitokeza


1. Njia za kuwapendeza Wazanzibar waunge mkono hazitawapendeza Watanganyika.

Wabunge wao wataridhia, lakini Watanganyika mitaani hawataridhia.


Haiwezekani kuwapendeza wazanzibar bila kuwaudhi Watanganyika.

Haiwezekani kukawa na ufumbuzi upande mmoja na kupuuza ya Watanganyika.


Hatua yoyote ya kuwapendeza Wazaznibar kimasilahi itakuwa ni kuwaumiza Watanganyika.


Kwa maneno mengine ni kuwabebesha mzigo zaidi Watanganyika ili muungano wa S2 uendelee kuwepo.


2. Rasimu lazima ipigiwe kura za maoni. Hilo ni tatizo kwasababu iliyoelezwa hapo juu. Uwezekano wa kupata 2/3 Tanganyika nao unaingia hatiani. Kwa upande wa Zanzibar 2/3 haitapakiana


Zanzibar haitapatikana kwasababu viongozi wao wa CCM wanaamini S2.

Huko mitaani kwa takwimu za tume ni mkataba.


Na kama haupo ni S3 kwasababu heri ya shari kuliko shari kamili.

Hivyo Unguja itapata ½ na Pemba itapata ½.


Katika hali mbaya zaidi, unguja CCM inaweza ikapata chini ya nusu kwasababu wapo Waunguja wasiotaka S2 kwasababu tu wameamini kuwa ni mfumo mbaya wa Nyerere.


NINI KITATOKEA
Kwa hali zote hapo juu hakuna uwezekano wa kupata 2/3, huo utakuwa mwisho wa rasimu ya CCM.

Hilo likitokea kuna lingine litafuata. Wananchi watakuwa wamejifunza kuwa, umiliki wa nchi kumbe u- mikononi mwao. Wanaweza kutaka wanachokusudia ikawezekana.

Hasira hizo zitahamishiwa katika uchaguzi mkuu.


Hata mbinu za wizi wa kura zikitumika, kutakuwa na matokeo muhimu sana.


Kwamba, idadi kubwa sana ya wabunge wa CCM watapoteza viti kwa umaarufu utakaojitokeza kwa upinzani. Kumbuka wapinzani watalibeba suala la katiba kama ilani ya uchaguzi.

CCM hawawezi kutumia S2 kama ilani kwasababu itakuwa imeshakataliwa na wananchi.
Na wala hakuna mbunge atakayesimamia suala lililokataliwa na wananchi.

Kwa upande mwingine wapinzani watalibeba kama bakora, na wananchi watataka kujua misimamo ya wabunge wa CCM

Wabunge wa CCM watakuwa na njia mbili tu za kujitetea
1. Kukubali sera ya serikali mbili kama ilani inavyosema, huku wakipoteza kura na umaarufu
2. Kukubali matakwa ya wananchi ya S3 na kuipa nguvu hoja hiyo zaidi ya ilivyo sasa.

Hivyo Bunge litapoteza 2/3 ya CCM ya sasa hata kama Rais atatoka huko


Hoja ya katiba itarudi na ikiwa na nguvu zaidi kupitia wapinzani.


  1. Kwamba hakuna kuhangaika tena, S2 zitakuwa zimeakataliwa
  2. Kwamba, CCM itakuwa imepoteza uhalali(legitimacy) ya kusimamia mageuzi kama ya katiba. Wananchi watachukua ukanda wa kuandika katiba yao.

Hadi hapo CCM wanaweza kuwa safarini kuelekea walipopumzika UNIP na KANU.



Tusemezane.

 
YAOKANAYO NA HOTUBA YA RAIS


BILA UKAWA, CCM WANACHANGAMOTO KUBWA SANA

CCM NDANI YA BUNGE LA KATIBA WATAVURUGANA

KIWEWE CHA UCHAGUZI KINATIA KIWEWE


Uwepo wa UKAWA ndio unawaunganisha CCM. Kitendo cha UKAWA kususa bunge kinakuja na changamoto kwa CCM.

1. Uwezekano wa rasimu kukwama mbele ya safari ni aslimia 95 kwasababu tulizoeleza.Kura ya maoni haiwapi nafasi Zanzibar.

2. Hofu ya katiba kukosa uhalali wa kidemokrasia na kisiasa hata kama itapata uhalali wa kisheria.

3. Kuvurugana wenyewe ndani ya bunge kwavile adui yao UKAWA hayupo. Na hapo tunafanunua

CCM itaweza kuingiza hoja ya S2 inayoambatana na mbadiliko makubwa ya rasimu iliyotengenezwa kwa muundo wa S3

CCM watakuwa na fursa moja na hasara kwa upande mwingine

1. Fursa:
Kubadili vifungu kutatoa nafasi kwa CCM 'kuhonga' pipi na lawalawa kwa Wazanzibar ili wasahau mfumo wa S3.

Vifungu vitakavyobadilishwa kuwapendeza Wazanzibar ni kama hivi, kutaja kwa uchache

a) Kuendelea kuitambua Zanzibar kama nchi na serikali yake ili kutowaudhi wznz
b)Kumweka Rais wa znz kama makamu wa Rais wa JMT ili kuondoa lalamiko la wznz
c)Kuwapa fursa za kukopa na JMT kuchukua dhamana ya deni kama ilivyoanza miezi michache iliyopita
d)Kuwapa upendeleo katika fursa za muungano kama ajira,elimu n.k. kisheria kama ilivyopendekezwa asilimia 21 ya ajira
e) Kuwapa fursa za kibiashara kama vile kuruhusu bidhaa kutoka znz bila ushuru
f)Kuweka kisheria viwango vya misaada vinavyopaswa kwenda znz
g) Kuwaongezea mgao wa pato la taifa kutoka asilimia 4.5 kwenda mbele zaidi ya hapo
h)Kutoa na kuweka nafasi za madaraka kama zile za mabalozi wanazolalamikia sasa.
i) Kutoa fursa za znz kujiunga na taasisi na mashirika ya kimataifa, kama sehemu ya malalamiko yao.

Orodha inaendelea haya ni kwa uchache.

2. Changamoto
Kutokana na malalamiko ya wazanzibar, wapo wana CCM wengi wameelewa kinachoendelea.
Hali hiyo imejengwa na kudodosa mambo yaliyokuwa yamejificha ambayo wznz wameyaweka wazi kwa kutojua.

Wabunge wa CCM kutoka Tanganyika na wa makundi maalumu watajiuliza swali moja.
i.e Yote hayo wanayopewa wazanzibar kama zawadi, ni kitu gani Tanganyika inafaidika nacho.

Suala litakalojitokeza si la kisiasa tena bali la kiuchumi.
Watanganyika(wachache) kwa kuelewa hakuna UKAWA wa kuwasemea, watajikuta wanaingia katika malumbano na CCM zanzibar katika hoja na maswali:

Je, haki hizo wanazodai wazanzibar, nini wajibu wao katika kuhudumia muungano?

Dhana ya Tanganyika kuvaa koti itakwisha kwavile tu wamekubali kutoa zaidi ya kupata?

Je,kutoa zawadi itaondoa dharau na kiburi cha kuvunja katiba kama walivyofanya wznz?

Je, gharama anazobeba Mtanganyika nini faida yake katika muungano na kwanini aibebe Mtanganyika mwenyewe?

Ikifika hapo suala la uchumi litaangaliwa kwa undani zaidi ya kisiasa.
Wabunge wa CCM wenye uchungu na nchi yao watajiuliza, hivi zawadi wanazopewa wznz ni faida gani.Hoja ikiwa investment vs return

Na katika investment, kumbukeni wapo wenye matamanio yao ya uongozi hivyo wana interest na ''investment zao''.

Katika nchi yetu Tanganyika,asilimia 97 ni big electoral college katika chaguzi
Hawa nao watajiuliza, je ni busara kuendelea kuwaudhi Watanganyika kwa zawadi za wznz?

Kutazuka mtafaruku kati ya CCM znz na CCM Tanganyika kila mmoja akiangalia masilahi ya upande wake na ya siku za usoni.

Ndani ya bunge hilo lisilokuwa na adui UKAWA, CCM watavurugana tu.Imeshatokea wabunge wa CCM Tgk kuwaambia wznz tumewachoka. Hilo halitaepukika wakibaki wenyewe ukumbini.

Hii wanasema ni 'one too many' au a tip of ice berg in the ocean.

Kwa mtazamo huo, CCM wanawataka sana ukawa kwa mambo hayo matatu
1. Kujenga uhalali wa kidemokrasia na kisiasa
2. Kupata 2/3 kwa njia zitakazowashirika UKAWA ili kufanya katiba iwe na sura ya utaifa
3. Kuepuka migogoro watakapobaki wenyewe.

Maswala hayo ndiyo yanayomsukuma Rais, Sitta na CCM kuwataka UKAWA warudi.

CCM ni wazuri sana wa kuangalia siku za usoni na hatari wameshaiona.

Suala linalowatatiza CCM si kuandika katiba ikapata uhalali.
Wanaweza kufanya lolote hata kuiba kura za maoni.

Tatizo linalowakwaza ni matokeo ''results'' yatakayoambatana na hatua zao za kibabe, kwanza kwa mustakabali wao ndani ya bunge lijalo na mustakabali wao ndani ya chama wenyewe kwa wenyewe.

Tusemezane
 
KWANINI UKAWA WASIRUDI BUNGENI

KUREJEA NI KUSALIM AMRI KWA WAHAFIDHINAWA CCM

WABUNGE WA CCM, VIONGOZI WA DINI NA WASOMI WAMESALIM AMRI. UKAWA WANASUBIRIWA

Katika uzi huu tuliwaonya UKAWA kuhusu nguvu mpya inayotumika ya kuwatumia viongozi wa dini kuwataka UKAWA warudi bungeni. Lengo la CCM ni kuhakikisha UKAWA wanakuwa sehemu ya maamuzi yao ili kujenga uhalali wa uharamu wa kile wanachokitaka.

Kwa mfano, tumewasikia CCM wakisema waliotoka ni baadhi ya wapinzani na wajumbe maalumu.
Maana yake ni kuwa wapinzani kama Mrema,Hamad Rashid na wale wa kuteuliwa waliobaki

Kutokana na nguvu ya UKAWA, CCM hawana chaguo bali kuwahimiza UKAWA warudi kuendelea kuharamisha mchakato.

Tulionya UKAWA wawe makini na kauli za viongozi wa dini wanaotaka warudi tu bungeni bila kueleza kiini cha mzozo na suluhu.

Majuzi baada ya kupoteza muda mwingi na uharibifu kufanywa na viongozi wa dini, UKAWA wakajitokeza kuwajibu.
Hii ilikuwa too late kwasababu wimbo wa 'rudini' ulishakuwa single mitaani na kufifisha madai yao ya kufuatwa kwa rasimu ya Warioba na kifungu husika(1 na 6). Kosa la UKAWA kama ilivyozoeleka kwao.

Pili, kumetokea makundi ya jamii yakitoa maoni kuhusu nini kifuatwe.
Chama cha wanasheria Tanzania (TLS) kimeweka wazi tafsiri ya kifungu kinachogombewa.
TLS imesema bunge lijadili rasimu ya Warioba na si kubadili kwa mujibu wa sheria.
Kutokana na presha ya viongozi wa dini, hoja hii nayo inafifia, tukibaki na rudini bungeni.

Tatu, vikao vyote vya usuluhishi havikuweza kuleta pande husika pamoja.
CCM wakigomea na UKAWA wakitaka Rasimu ifuatwe. Hili lina maana, wahafidhina wa CCM hawawezi kubadili msimamo wao asilani.

Wahafidhina wana nguvu sana. Wameweza kuwaweka 'mahabusu' wabunge wao.Na sote tunafahamu wabunge wa CCM wameweka rehani akili na fikra zao. Wanaweza kuombwa Wake au Waume zao watumiwe kwa burudani ndani ya chama na wao kukaa kimya.

Wahafidhina wameweza kumtisha mwenyekiti wao hadi kuacha masilahi ya taifa kisheria na kutetea misimamo yao.
Wahafidhina wameweza kuwatumia viongozi wa dini kuweka shinikizo lisilo na sababu kwa UKAWA.

Kwasasa kuna kundi limejitokeza la wasomi linalowataka UKAWA warudi bungeni.
Hoja ya kundi hili lenye 'mrengo' wa ushawishi wa wahafidhina ni Kwamba, UKAWA warudi kupambana ndani ya bunge.

Endapo majadiliano ya UKAWA na CCM hayakuzaa matunda, huu ni ujumbe kuwa CCM hawakubali makosa ya kutaka kubadili na kuandika katiba yao. Leo UKAWA warudi uwanjani tukijua timu nyingine ina wachezaji 14 na refarii? unapigana nini hapo?

UKAWA wakirudi bungeni tayari watakuwa wameidhinisha rasimu ya CCM kujadiliwa na kupitishwa. Hakuna namna wanaweza kulizuia hilo tena ndani na nje ya bunge. Kwa kurudi, Wahafidhina wa CCM walioteka makundi yaliyotajwa hapo juu wataendelea na nguvu zao na in fact itakuwa ni kuwatia moyo waendelee na uhalaifu

UKAWA wanakumbuka jinsi wahafidhina walivyomtisha Rais na kubadili sheria za bunge la JMT.
Walitishia hadi mswada uliopitishwa na watu 100 ukasainiwa na Rais.

Ndivyo walivyomtishia mwenyekiti Sitta hadi kuvunja kanuni, ndivyo walivyowawekea matambara na pamba chafu midomoni, wabunge wa CCM.

UKAWA wakikubali kurudi, huko ni kuusaliti umma ulio nyuma yao, na itakuwa ni hatua nzuri sana ya kujisalimisha kwa wahafidhina. Hali hiyo itaendelea hadi kura ya maoni kwasababu kikwazo kikubwa kwa wahafidhina kwa sasa ni UKAWA kurudi bungeni.

UKAWA wana hoja moja tu, kwamba, waulize swali lifuatalo. Wanarudi bungeni kujadili rasimu ipi?
Kama ni ile ya Warioba, warudi haraka sana.
Kama ni kutengua rasimu ya Warioba, basi wawaachie wahafidhina

UKAWA walizembea presha ya ya viongozi wa dini kuoa majibu.
Leo presha hiyo imefunika sehemu kubwa ya hoja yao.

Kuna presha imeanza ya kuwatumia wasomi, ambao kama viongozi wa dini wanakwepa ukweli wa tatizo na kuwataka UKAWA warejee bungeni tu kujaza idadi na akidi.

UKAWA wakikubali kurudi bungeni, inabidi watoke na kuwaomba radhi wananchi na pia watangaze hadharani kusalim amri kwa wahafidhina wa CCM kama walivyosalim amri viongozi wa dini, wabunge wa CCM na mwenyekiti wa CCM

Tusemezane
 
JEURI YA AKINA SITTA INAWEZA KUWA NA HERI MBELE YA SAFARI

CCM WENYEWE WATASAIDIA KUTANZUA KITENDAWILI

WATAZITAKA SERIKALI 3 WAKIWA WAMEJERUHIANA NA KUCHELEWA

Mpango wa Samwel Sitta kuendelea na bunge ili ‘kuonyesha' mazuri yaliyomo ndani ya rasimu una tatizo mbele ya safari.

Si mazuri tu ytakayoonekana ili kuwapendeza Wazanzibar, mabaya yatajitokeza pia.

Bandiko lililotangulia tumeonyesha wznz watakavyopewa zawadi,mwisho wa siku wakubali mfumo wa wahafidhina

Kutokana na kauli za wazanzibar dhidi ya muungano, mgawanyiko utatokea

Wazanzibar wakitetea masilahi yao na ‘Watanzania' wakitetea nchi.
Wazanzibar watalazimisha watanzania wajisikie kama Watangayika kwavile madai yao ni uzanzibar na si Utanzania. Utanganyika utazaliwa rasmi hata kama si kwa kutaja.

Zawadi watakazopewa(rejea bandiko juu) zitatoka kwa wahafidhiana.
Lengo likiwa ni kubakiza S2 kwa maslahi yao

Kutajitokeza wanaCCM wazalendo watakaokerwa na Uzanzibar, na wao kujinasibu na Utanganyika.

Kwavile suala kubwa litakuwa ni uchumi, Watanganyika watatoa majibu ya mambo yanayolalamikiwa

1. Kuvua koti la muungano
Watanganyika wataomba kuwepo tofauti za mambo ya muungano dhahiri ili kuondoa lawama za kuvaa koti na si kuwajibika na koti.

Katika kufanya hivyo, watapenda kujua koti walilovaa wanalivua kwa kiasi gani.
Kuvua koti kutaambatana na gharama za kulihudumia koti hilo kutoka pande zote.
Koti litakuwa halina mmiliki kama ilivyo sasa,hivyo usafi wake utahitaji kushirikiana.

2. Zanzibar watataka mgawanyo sawa wa madaraka, misaada na mikopo(malalamiko)
Hapo watafungua Pandora box na kuulizwa, gharama za muungano wanachiangiaje

Uchumi utakapoingia maelewano hayatakuwepo miongoni mwa wanaCCM
1. Tanganyika itataka ‘kila mmoja awajibike '' katika muungano na si kufaidika tu
2. Zanzibar watatumia turufu ya udogo na uchache kukwepa uwajibikaji

Majibu ya maswali hayo yatahitaji data za uchumi na kutenga shughuli za kila nchi.
Kijamii, itabidi znz wakubali kubadili katiba yao ili iendane na zawadi watakazoahidiwa
Ikumbukwe ni CCMznz ndio walipitisha katiba ya 2010 inayolalamikiwa na CCM-bara

CCMzanzibar wataogopa kukubaliana na suala hilo ili kutopoteza umaarufu wao znz

Itakaofika hapo rasimu ya Warioba itaonekana kwa uwazi zaidi kuliko wanavyojidanganya sasa

Yatajitokeza makundi matatu miongoni mwa wanaCCM hao
1. CCM Zanzibar
2. CCM Tanganyika
3. CCM wahafidhina

Lazima mgogoro utatokea.
Kwa mantiki hiyo UKAWA hawana sababu za kurudi bungeni bila suluhu ya maana.

Rasimu ya Warioba itarudi ilikotoka kwa majadiliano au kwa CCM kuvurugana.

Endapo Sitta anaitakia CCM heri, inambidi afikirie kama uamuzi wake utakuwa na manufaa kwa chama chake. Tayari ameshindwa mtihani wa BMK kama tulivyowahi kumueleza huko nyuma.
Hili nalo linaelekea kukamilisha matokeo ya mtihani wake kuelekea 2015

Lakini pia linaweza kutusaidia sana kuharakisha safari ya CCM maktaba walipopumzika UNIP na KANU. Historia siku zote hujirudia. KANU ilivuruga kwa ubabe kama Sitta wakati wa katiba.
UNIP ilivuruga wakati wa katiba kama CCM. Huenda historia inataka kutupendelea na sisi.

Tusemezane

 
UKAWA, JIULIZENI: S2 ZIMEINGAIJE KATIKA RASIMU

ULIZENI MUONYESHWE S2 MABORESHO ZIMETAJWA WAPI KATIKA RASIMU?


Mara baada ya ufunguvi wa BMK katika hali ya kuvunja kanuni ya 7, hatua ilifuata ilikuwa kujadili rasimu.
Mjadala ulikuwa kuhusu vifungu namba 1 na 6 vinavyojadili muundo wa muungano.

Hoja iliyokuwepo ni rasimu na muundo wa serikali, ambao kwa mujibu wa rasimu ni 3.
Hatua ya kwanza ilikuwa kugawa wajumbe wa BMK katika ndogo zenye wajumbe 50 ili kurahisisha majadiliano.

Kila kamati ilikuwa na wajumbe kutoka sehemu mbili za muungano. Hata hivyo ieleweke kuwa hakukuwa na wajumbe wa Tanganyika. Waliokuwepo ni wa JMT ambao walibatizwa na kusimishwa haraka na kuwa wajumbe wa Tanganyika.
Tukapata wajumbe wa Tanganyika kiajabu ajabu na wale wa Zanzibar kisheria.a

Hoja hii inaeleza jinsi ulaghai ulivyoharibu mchakato. Wabunge wa JMT wameapa kutetea JMT ikiwemo Zanzibar.
Wale wa Zanzibar wameapa kuitetea ZNZ. Ni mjumbe gani aliwakilisha Tanganyika? Kosa tunalolidharau lenye hekma.

Anyways, kilichotakiwa katika kamati za wajumbe ni 2/3 kukubali au kukataa muundo kwa mujibu wa rasimu.
Katika uwasilisha wa maoni, ilipaswa kusemwa wajumbe idadi kadhaa, mfano, 1/2 au 2/3 au 3/4 wameafiki au hawakuafiki muundo wa uliopendekezwa.

Kinyume chake tukasikia maoni ya 'wengi na wachache'' kitu ambacho hakikuwa sahihi.
Hata pale waliotaka S3 walikuwa wengi, wajumbe waliokataa walitajwa kama wengi.
Ilikuwa ni ulaghai kuonyesha wengi ni wa CCM na wachache ni wapinzani.
Haikutakiwa kuwa hivyo kwasababu wote walikuwa wajumbe wa bunge moja.

Katika maoni hayo ya 'wengi' tulisikia wakipenekeza mfumo wa S2. Hiki nacho ni kituko! Nyaraka iliyokuwa mbele ya bunge haikuongelea mfumo wa S2 wala haikutoa option ya mifumo mingine. The final document ilikuwa ni S3 kama muundo

UKAWA WACHEZA JUU YA ULAGHAI

Kwa bahati mabya, UKAWA kwa kutojua wakajikuta katika kuimba 'walio wachache''.
Wakakaa kimya pale insunation ya S2 ilipofanyika. Walichotakiwa kuuliza ni kuwa nyaraka iliyoko mbele yao haizungumzii S2.

Na wala kanuni za bunge hazikuelekeza kutoa ushauri wa mfumo mwingine.
Hili ni kosa la UKAWA na wala hawajaliona hata walipotoka.

CCM NA LUGHA ZA KILAGHAI ZINAZOFANYA KAZI VEMA

Hoja ya CCM kuhusu takwimu za tume inasema, kwanini Warioba hakuweka machaguo mengine, mkataba au S2 au S1

UKAWA hawaelezi ukweli unaotokana na hadidu za rejea walizopewa.
Kwamba, hadidu ziliwataka wakusanye maoni, wayafanyie tathmini na waje na draft kamili.
Ndio maana kulikuwa na hatua mbili za rasimu.

CCM hao hao wanaohoji takwimu nyingine, wameweza kupenya mfumo wao wa S2 kinyume na malalamiko yao.
Katika maoni, hatujasikia CCM wakisema waliotaka mkataba au S1 wana maoni gani.
Hapa ni kuwa wamechagua kile kinachowafaa na kutumia udhaifu wa UKAWA katika kuwalaghai.

CCM wanasema, wataendelea na bunge kujadili mambo mengine muhimu kuliko muundo.
Ni CCM hao hao wanaosema roho ya katiba ipo katika muundo ambao ni vifungu 1 na 6.
Sasa kama ni hivyo, wanawezaje kujadili maeneo mengine wakaiacha roho ya katiba? Ulaghai mkubwa huu.

Ni kwa mantiki hiyo hakuna nia njema ya kuandika katiba kutoka kwa CCM. Mwenyekiti wao alisema S3 hadi aondoke
Ulaghai unaendelea na hakuna sababu za kuamini kuwa UKAWA wanaweza kurudi na kupamba nao.

UKAW watambue kuwa ulaghai huu unafanyika chini ya uongozi wa CCM kazi hiyo ikifanywa na Samwel Sitta.
Kudanganyika kuwa warudi kufuata kanuni kama alivyosema JK ni kujidanganya.
Kanuni namb 7 imevunjwa na Samwel Sitta kwa maelekezo ya JK, leo kuna kanuni gani imebaki tena kuheshimiwa

UKAWA msimamo wa kutorudi ndio utalisaidia taifa na kuwajengea heshima siku za usoni.
Kukubalina na matakwa ya Wahafidhina, ni kukubali kusalimu amri.

Kumbukeni kuwa :
1. Wahafidhina wameshawateka wabunge wa CCM,kusweka pamba na matambara vinywani mwao
2. Wameshamtisha mkuu kiasi cha kubadili msimamo kwa kona ya ghafla bila indicator
3. Walishammaliza mwenyekiti wa bunge siku nyingi
4. Wamewaweka wasomi katika mifuko ya suruala zao.

Kundi lililobaki na linalowasumbua ni ninyi UKAWA.
Wakifanikiwa basi mtakuwa mumehalalisha umafia na ndio mwanzo wa nchi kuselelea kusikojulikana.

Tusemezane
 
HAKUKUWA NA NIA NJEMA YA KATIBA
NI MAZINGIRA YALIYOMLAZIMISHA RAIS
MUUNGANO NDICHO KIINI CHA MZOZO HUU


Wana duru, ni vema tukaeleza kwa undani uhalifu wa kukwamisha katiba ulivyoanza.
Wapo wasemao kulikuwa na nia njema ya rais, wanaokwamisha ni wapinzani

Tutakuwa na mfululizo wa mabandiko tukionyesha kwa kadri, kwanini si suala la nia
Njema halikuwepo.

Na bahati mbaya hesabu zilizokuwa zimekusudiwa zimekwama dakika ya mwisho.

Sehemu ya I
Hoja ya katiba ni kilio cha wapinzani tangu mfumo wa vyama vingi.
Karibuni, hoja imepata nguvu zaidi hata kuwa ilani ya uchaguzi.

Vugu vugu la kisiasa za uhasama Zanzibar limetishia uwepo wa muungano
Na kubwa zaidi, nchi zote za Afrika mashariki zimefanya mageuzi ya katiba.
Suala la kuja Tanzania lilikuwa la muda tu. Katiba ingeandikwa kwa namna yoyote iwavyo

Shinikizo la katiba lilitoka ndani ya bunge.
Shughuli nyingi zilikwama kutokana na mchanganyiko wa muundo uliopo.

Pamoja na hayo, maswala ya uchumi yaliongeza shinikizo kutokana na mpangilio hovyo
wa muundo wa sasa. Ilikuwa ni dhahiri, lazima yawepo mageuzi ya katiba.

Hoja iliyomkabili Rais haikuwa kuandika katiba bali kulinda muungano.
Kilichoonekana haraka, swala hilo likiachwa upo uwezekano agenda
ikabebwa na vyombo vingine na hivyo na Muungano kuwa katika hati hati.

Rais akaamua kuwa ahead of game kama walivyofanya siku za nyuma.
Tume ya vyama vingi Rais Mwinyi alikubali kutokana na shinikizo la mabadiliko
ya kisiasa duniani.Mwalimu Nyerere alisema, sisi si kisiwa, lazima twende na dunia.

Rais Mwinyi akaunda tume ya Nyalali ili iwajibike kwake na kumpa nafasi ya kufanya atakalo
Kwa busara na mazingira, hakukuwa na namna ila kukubaliana na mfumo wa vyama vingi.

Kuunda tume siku zote hulenga kuhodhi umiliki wa jambo.
Kuundwa kwa tume nje ya kiongozi kunaweza kuwa na matokeo yakayomtatiza.

Mfano mzuri ni tume ya Mwakyembe ambayo matokeo yake tunayajua.
Tume hiyo haikuwajibika kwa rais bali bunge.
Mwisho wa siku Rais akakosa udhibiti na kukubaliana na maoni ya tume

Inapotokea kiongozi anaunda tume, maana yake anataka kujilinda yeye.
Tume haiwezi kumchunguza kwasababu inawajibika kwake.
Hiyo ndiyo imekuwa njia ya kukwepa mkono wa uwajibikaji.Kila mtu anaitumia

Hapa nitoe mfano wa mtaani. Baba atamwagiza mkewe kuchunguza kiini cha watoto
Kuanza kuvuta sigara wakiwa wadogo.
Mama atakuja na maoni ya kuwatuhumu watoto wa jirani na baba atakubaliana nayo.

Laiti majirani wangeunda tume, uchunguzi wao ungebaini kuwa baba ambaye ni mvutaji
Ndiye ame wa influence watoto.

Ili kukwepa kuwajibika siku zote baba atamwagiza mama
Kama tume. Hata kama taarifa ya mama ita mu-implicate baba, bado anayo nafasi ya kusema
Jambo hilo marufuku kujadiliwa, na ikawa hivyo. Ndivyo tume zinafanya kazi siku hizi

Tume zimeundwa lukuki kuhusu muungano

Inaendelea..
 
Inaendelea.....

Shemu ya II

Huko nyuma, Marais waliunda tume kuchunguza kero za muungano.
Kuna tume ya Nyalali, Kisanga, Warioba ya kwanza, Amina Salum na wengine wengi.

Zote hizo ziliwajibika kwa rais mhusika na matokeo yake yalikuwa hayamlazimishi rais kufanyia kazi
Ni kwa mantiki hiyo,suala la S3 limesemwa sana lakini halikuwa na utekelezaji.
Rais aliyekuwa madaraka hakufungwa na sheria yoyote kutekeleza au kujadili.

Awamu hii, suala halikuwa kero. Ilikuwa ni mabadiliko ya jumla ya katiba.
Katiba ni suala la wananchi,isingekuwa rahisi kwa Rais kuficha taarifa zake kama waliotangulia walivyofanya.

Tatizo likawa, ni kwa namna gani jambo hili linaweza kufanyika bila kuathiri muundo wa muungano?
Ndipo ikaja hoja Rais lazima achukue udhibiti wa mchakato(Pre-emptive strategy)
Lakini, je hilo linawezekana kwa uataratibu wa kuandika katiba?

Tukaona Rais akitangaza kuanzishwa kwa mchakato.
Kama mtakumbuka, mswada wa kwanza ulizuia kabisa kungumzia swala la muungano.

Ni hadi pale wajumbe walipopambana na hasira za watu hasa kule Zanzibar.
Mnakumbuka mswada ulichomwa moto mbele ya Samwel Sitta.

Hivyo Rais hakuwa na namna nyingine isipokuwa kukubali swala la muungano lijadiliwe.
Sheria ya kuanzisha machakato ikaweka masharti kuwa agenda ya muungano iwe kuulinda.

Katika mazingira ya kawaida, ilibidi Rais aitishe mkutano wa kitaifa ili kupata
mweleko wa taifa linalokusudiwa kujengwa
Baada ya hapo hadidu za rejea zingepatikana na mchakato wa BMK na kura ya maoni kufuata.

Utaratibu huo ukaonekana utakuwa na matatizo.
Mkutano wa kitaifa ungeweza hata kuamua kubadili au hata kuvunja muungano.

Wajumbe wa mkutano wa kitaifa wanatoka makundi mbali mbali ya kijamii na
huenda muungano ungekuwa katika majaribu

Wana mkakati wakaamua kukiruka kipengele hicho kwa maana ile ile ya kuandaa
mazingira ya kumpa Rais umiliki wa mchakato. Tatizo ikaanzia hapo.

Kumbuka tungeanzia mkutano wa kitaifa, mchakato usingekuwa mikononi mwa Rais.

Kukwepa mkutano wa kitaifa ikiwa ni faraja ya muda ambayo sasa yunalipa gharama zake.
Ni jambo lisiloepukika katika uandikaji wa katiba, Rais akaliepuka na sasa mzigo unamwelemea

Kuepuka mkutano wa kitaifa kulilenga kumpa udhibiti wa mchakato na ulinzi wa muungano.

Je, alipata udhibiti aliohitaji?

Inaendelea ......
 
Inaendelea ......
Sehemu ya III

Ni vipi Rais alipewa udhibiti wa mchakato.Kwanza ni yeye kutoa wazo.
Pili, kutumia serikali yake kuandaa sheria zihusianazo na mchakato.

Tatu, kupata nafasi ya kubadilisha matokeo akitumia sheria
zinazomlinda kihalali kabisa.

Ni kwa msingi huo, mswada wa kwanza ulikuwa kumpa Rais madaraka ya kuunda tume.
Hilo likafanikiwa.

Na kwa hilo, Rais aliweza kuipa tume hadidu za rejea kutoka na sheria ya Bunge la JMT.
Hadidu rejea hizo zilimwezesha kuweka kipengele cha kulindwa muungano.
Kwamba, tume isiende nje ya hapo

Sheria haikumpa nafasi ya hadidu za rejea kuhusu muundo wa muungano.
Hilo lilifanyika makusudi ili kuzuia uasi kama ule wa mswada wa
kuanzisha mchakato uliochomwa Zanzibar.

Sheria ya kuunda tume ilimpa nafasi Rais achague wajumbe wa tume.
Hapo napo ililengwa yeye kuwa na uwezo wa kuchagua makada
watakaosimamia dhamira ya muungano wa serikali 2 .

Tume ikaanza kukusanya maoni katika rasimu.
Rasimu ya kwanza ikaonyesha matakwa ya wananchi ni serikali 3.
Hapo Rais hakuwa na uwezo tena wa kudhibiti tume kufuata matakwa yake

Mkakati wa pili ukabuniwa
Mkakati wa pili, ikawa kuwatumia wabunge wa JMT na BLWA kuwa
sehemu ya wajumbe wa bunge maalumu

Hii ililenga kuingiza wajumbe kwa mfumo wa chama ili kuweza kuwadhibiti, tofauti na wajumbe wa nje.

Kwa kutambua hilo, wapinzani wakataka idadi ya wajumbe wa kuteuliwa iongezwe.
Kumbukeni, kulikuwa na sintofahamu ya kupata wajumbe wa kuteuliwa.

Wapinzani walitaka wajumbe wapatikane bila uteuzi.
Hilo lingepunguza nguvu ya udhibiti wa Rais.

Sheria ikasema, yeye atateua wajumbe kwa kufuata mapendekezo ya taasisi
na jumuiya mbali mbali.

Jambo hilo likampa uwezo wa kuteua makada aliotaka.
Yeye alichotakiwa ni kupokea orodha ndefu halafu achague
Kwa kufanya hivyo alikuwa na uwezo wa kuteua watu watakaokubaliana na
matakwa yake

Udhibiti wa tume,BMK na mchakato bado ungekuwa mikononi mwake

Inaendelea
 
Inaendelea......

Sehemu IV

Baada ya kubaini uwepo wa S3, serikali ikapeleka mswada haraka bungeni ili
kufanyia sheria marekebisho.

Marekebisho hayo yalilenga kuondoa kifungu 134 kinachowataka wajumbe
wa tume kuwa sehemu ya bunge la katiba.

Kuondoa wajumbe wa tume ndani ya BMK ilikuwa ni kupunguza nguvu zao
za ushawishi ili Rais abaki na udhibitiWa mchakato. Hilo likafaninikiwa.

Tatizo lilomkabili ni shinikizo la kuongeza wajumbe wa kuteuliwa ili wa neutralize
ile namba kubwa ya CCM kutoka Pande zote.

Hata hivyo mkakati huo kwa wapinzani una matokeo kidogo ingawa yana nguvu
kwa sasa.

Wajumbe wa makundi kutoka UKAWA ni wale wenye ushawishi ingawa ni wachache.

Idadi yao inapunguza 2/3 kutoka pande zote kwa kiasi kikubwa sana.
Hadi hapo bado Rais alikuwa na udhibiti wa mchakato ingawa nguvu zilikuwa zimepungua sana.

Ilibidi kuwe na mkakati mwingine wa kulinda ule ushawishi kidogo aliokuwa
amebaki nao Rais.

Mkakati ukabuniwa wa kura za wazi na siri kwa lengo la kudhibiti idadi chache tu
ya wabunge wa CCM ambao wengeweza kubadili matokeo zaidi.

CCM ikaitisha kikao na kuamua wabunge wake wawe na msimamo wa kura ya wazi.
Kura ya wazi ililenga kuwadhibiti wabunge wa CCM na hilo limefanikiwa.

Tatizo likajitokeza, ni namna gani rasimu inaweza kubadilishwa ili kuingiza hoja za S2 ambazo zilikuwa hazipo?

Inaendelea...
 
Inaendelea...

Sehemu ya V na mwisho

Ili kuweza kuingiza hoja ya S2 ilibidi kanuni ziandikwe kulingana na hilo.
Kwa bahati mbaya, kanuni ziliandikwa wakiwemo wapinzani na hivyo kuwa na udhibiti.

Mkakati mwingine ukabuniwa. Kumpata Spika anayeweza kuendesha BMK kwa
njia za kidikteta.

Ilifahamika kuwa Sitta alikuwa na heshima na kazi hiyo ingemfaa.
Ndio maana wajumbe wengine kama akina Chenge walishauriwa wajitoe.

Maana yake ilikuwa kutoudhi wajumbe wa CCM kutokana na taswira ya Chenge kisiasa.
Pia ulimpa Sitta rungu la kuendesha BMK kwa ubabe ambao leo unadhihirika kuwa hovyo

Mkakati mwingine ukawa kumtumia Mh Sitta kupinda kanuni ya 7 ili Rais ahutubie baada ya Warioba
Hilo lilimwezesha kujibu hoja za Warioba na hata kufanya upotoshaji.

Rais na Sitta walijua kuwa Warioba atakuwa nje ya bunge na hakuna mahali pa kujitetea
au kufanya ufafanuzi yeye na tume yake.

Mkakati wa kutumbukiza S2
Ilipofika muda wa kujadili rasimu, tukasikia maoni ya wengi yakisema mfumo ni S2.
Hakukuwa na maoni ya wengi, kilichokuwepo ni kamati na taarifa zilitakiwa ziwe idadi na maoni yao.

Ghafla rasimu ikaanza kubadilishwa. Rasimu haikupendekeza mfumo wa S2 mahali popote
Huo ulikuwa mkakati wa kuingiza maoni ambayo tume haikuyapendekeza.
Vinginevyo tungesikia ‘wengi wengine ' wakisema mkataba au S1

Hapo ndipo UKAWA wakabaini baada ya kukwepa vikwazo vyote, sasa inatumika hoja ya nguvu.

CCM walichokitaka ni kitu kimoja, S2 iwe sehemu ya majadiliano halafu watumie ule wingi wao wa
Wabunge wa JMT na BLW kupitisha wanachokitaka na kuua rasmi Rasimu ya Warioba.

Hii maana yake ni kuwa maoni ya wananchi wachache wanaotaka S2 dhidi ya wale wa S3 na mkataba ndiyo yatapelekwa kupigiwa kura.

Hivyo maoni ya wananchi wengi yatazikwa na hoja ya wahafidhinaItatamalaki.
Huko ni kuua demokrasia ili kulinda S2 kinyume na matakwa ya wananchi.

Ili kulinda haki za wananchi, kuzuia wahafidhina kuiumiza nchi, kukuza demokrasia na kupata
Katiba ya wanachi, UKAWA hawatakiwi kurudi bungeni.

Warudi bungeni pale ambapo moyo wa rasimu ya Warioba utakapoachwa kama ulivyo.

Nia ya Rais ilitokana na shinikizo na mazingira.

Nia ya kuwa na katiba ni wazo la watu
Rais amelifanyia kazi kwa njia za kulinda masilahi kinyume na wananchi.

Hivyo nia yake sasa inaonekana kutokuwa njema.
Ingalikuwa njema asingesema S3 hadi aondoke.

Hakukuwa na nia njema,kilichokuwepo ni mazingaombwe ambayo mwisho yamekwama.


Tusemezane.
 
CCM WAUNGANA NA DURU ZA SIASA
UPO UHALALI WA KISHERIA NA SIYO KISIASA

WABUNGE WA CCM YAMEWAKIFU, WATOA YA MOYONI


Wanaduru
Kwanza tutakayojadili ni kwa hisani ya gazeti la Mwananchi
Mwananchi: mwanzo - Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza

Tumesema katika uzi huu mara nyingi ya kuwa, CCM wanaweza kurudi bungeni wakaendelea na kuandika katiba yao.
Kisheria hawajavunja kifungu chochote na wana akidi ya kutosha.
Pengine watakosa 2/3 kama utaratibu navyotaka.

Hata hivyo, hoja yetu imekuwa, Uhalali wa kisheria si uhalali wa kisiasa na kidemokrasia.
Tunaona Mwigulu na Wassira wakikubaliana na hoja, na pengine ungekuwa si ukaidi wa CCM tusingekwama.

WABUNGE WA CCM WATAKA KUAHIRISHWA

Hoja ya kukosa uhalali wa kisiasa inashika kasi, wabunge wa CCM wanapokubali kuwa UKAWA ni muhimu.
Katika siasa, kuna makundi yasiyoweza kubezwa hata kidogo. UKAWA lina wafuasi wengi sana nyuma yao.

Siyo suala la akidi na wingi, kinachoangaliwa ni ushawishi wa kijamii.
UKAWA ina viongozi wa upinzani wanaoungwa mkono na sehemu kubwaya jamii.

Madai yao yanawagusa hata CCM wanaoitakia nchi hii amani na utulivu.
Anapotokea kiongozi kama Samwel Sitta na Anne Kilango wakitaka mchakato uendelee kwasababu akidi inatosha, inasikitisha.

Wingi (quantity) na ubora (Quality) ni vitu viwili tofauti.
Kwa mtazamo wa katiba, ubora si wa mtu, bali washiriki kwa ujumla wao.

BMK bila UKAWA linakosa ubora kwa mantiki, halina maridhiano. Hapa ubora ni maridhiano na wala isieleweke kama weledi wa mtu.

Wabunge wa CCM waliohoji wengi wameshauri bunge liahirishwe.
Hoja yao kubwa ni busara za kuangalia ''quality' kwamba, hawawezi kuandika katika bila maridhiano ndani ya jamii.
Hili ni la kupongezwa sana kwa wabunge hao wa CCM

Watu wengi wanaitupia lawama CCM. kwa undani CCM inagawanyika katika makundi mawili
1. CCM Moderate
2. CCM wahafidhina

Hawa CCM moderate ni wale wanaotanguliza masilahi ya wananchi.
Wanakubali jambo fulani lenye msilahi ya nchi liangaliwe kwa jicho la nchi.
Kwa bahati mbaya kundi hili halina nguvu ndani ya CCM. Ndicho kilichoplekea wakafungwa midomo na kura ya wazi.

Kundi la wahafidhina lina nguvu sana. Linaweza kupanga safu ya uongozi, nani aondolewe nani abaki.
Ndilo limemtisha hadi mkuu akabadili mwelekeo. Lina siri nyingi na lina pesa.

Hili ndilo linalopigiwa upatu na akina Mwigulu na Wassira.
Akina Nape wanalazimika tu kwasababu ni kazi, hawana nguvu

JOTO LINAPANDA

Nguvu ya umma inazidi kujitokeza kwa kasi. CCM wanalaumiwa kwa kuhujumu mchakato.
Kwa bahati mbaya, hukumu hachagui maridhiano au wahafidhina. Hukumu ni juu ya CCM

Hawa CCM moderate wameoiona hatari hiyo. CCM inazidi kupoteza uungwaji mkono hata miongoni mwa makundi yake.
Kilio si cha UKAWA, kimekuwa kilio cha taifa UKAWA wakipewa rungu la kukabliana na CCM

UKAWA wanazidi kuimarika huku CCM kwa ujumla wao wakizidi kupoteza umaarufu.

Ni kwa msingi huo, baadhi ya wabunge kama walivyosomeka katika gazeti la Mwananchi wanaona enough is enough.
Haiwezekani meli izame kwasababu ya wahafidhina. Wameamua kusema baada ya kukifu

Tutaendelea kuona wabunge wa CCM wakijitenga na CCM wahafidhina katika siku za karibuni.
Huko nyuma tumeeleza vurugu ndani ya CCM wenyewe, huu ni mwanzo tu wa kile tunachosema.

Tusemezane.
 
Hakuna chama cha siasa kinachoweza kupata 67% Zanzibar. Si CUF wala CCM.
Na ninaungana na Prof. Tibaijuka kuwa, CCM has nothing to loose kwa sababu katiba mpya si rahisi kupatikana kama tutategemea 67% ya Zanzibar.
The Status quo will prevail as predicted earlier.
 
Hakuna chama cha siasa kinachoweza kupata 67% Zanzibar. Si CUF wala CCM.
Na ninaungana na Prof. Tibaijuka kuwa, CCM has nothing to loose kwa sababu katiba mpya si rahisi kupatikana kama tutategemea 67% ya Zanzibar.
The Status quo will prevail as predicted earlier.
Uwezekano wa kupata 2/3 kwa chama kimoja Zanzibar upo.
Kwanza, ndani ya BMK kuna wajumbe wa kuteuliwa ambao misimamo yao haitegemei uchama.
Wanachama hao ndio wanainyima CCM 2/3 kwa upande wa Zanzibar kwa sasa kama BMK litaendelea.

Pili,wazanzibar hasa wa CCM wamegwanyika. Miongoni mwao wapo waumini wa S3.
Kinachoonekana kwa sasa ni wahafidhina kuwa na sauti kubwa na kuonekana ni CCM yote.

Kwa mfano, mvutano kati ya Pandu Kificho na waziri wa SMZ kuhusu msimamo wa BLW ni kiashirio kizuri.
Lakini pia, kuna watu wanaunga mkono kwa chini chini.
Rais wa zamani Karume ana ushawishi miongoni mwa wajumbe wa BLW na yupo upande wa S3.

Kama ulivyomuona Mansour Himid, ndivyo walivyo wajumbe wengine kichini chini.

Kimantiki kura ya wazi kwa CCM iliwekwa mahususi kuzuia 2/3 kupatikana kwa kutumia zanzibar.

Kikwazo kikubwa, ni BMLK baada ya hapo kura za maoni hazitakuwa na tatizo.
Kwakuelewa hilo CCM hawakubali kuvuka BMK.

Wanajua rasimu ya Warioba ikienda kwa wananchi kuizuia ni taabu sana.
Kumbuka wazanzibar walitaka mkataba, alternative yake ni S3

Hata kwa bara 2/3 inawezekana kabisa. Tatizo wabunge wa CCM wamesokomezwa matambara mdoni. Wapo kifungoni
Ni ngumu kuelewa wanasimamia nini wakiwa 'gerezani' lakini upo ushahidi wengi hawakubalini na mfumo uliopo.

Kama unafutilia, angalia waliobaki kuutetea mfumo huuni wangapi.
Wengi wamejitoa kwa kuelewa kuwa mwakani watasimama wenyewe mbele ya mahakama ya wananchi.

Disadvantage ya wabunge wa CCM ni kusema 'mimi nina msimamo ABC' kulingana na wananchi.
Hapo watakuwa na wakati mgumu kwenda kinyume na msimamo wa chama, wakati huo wakitakiwa kuwafariji wapiga kura.

Kwa upinzani, hilo litakuwa ni agenda ya vyama vyao. Watasema sisi, kwasababu imo katika ilani yao.
Hawatajitetea kama individuals

Kwa kuangalia hilo, wabunge wa CCM wamesoma hisia za wananchi wao. Ingekuwa mambo yamenyooka 2/3 ingepatikana.
 
Uwezekano wa kupata 2/3 kwa chama kimoja Zanzibar upo.
Kwanza, ndani ya BMK kuna wajumbe wa kuteuliwa ambao misimamo yao haitegemei uchama.
Wanachama hao ndio wanainyima CCM 2/3 kwa upande wa Zanzibar kwa sasa kama BMK litaendelea.

Pili,wazanzibar hasa wa CCM wamegwanyika. Miongoni mwao wapo waumini wa S3.
Kinachoonekana kwa sasa ni wahafidhina kuwa na sauti kubwa na kuonekana ni CCM yote.

Kwa mfano, mvutano kati ya Pandu Kificho na waziri wa SMZ kuhusu msimamo wa BLW ni kiashirio kizuri.
Lakini pia, kuna watu wanaunga mkono kwa chini chini.
Rais wa zamani Karume ana ushawishi miongoni mwa wajumbe wa BLW na yupo upande wa S3.

Kama ulivyomuona Mansour Himid, ndivyo walivyo wajumbe wengine kichini chini.

Kimantiki kura ya wazi kwa CCM iliwekwa mahususi kuzuia 2/3 kupatikana kwa kutumia zanzibar.

Kikwazo kikubwa, ni BMLK baada ya hapo kura za maoni hazitakuwa na tatizo.
Kwakuelewa hilo CCM hawakubali kuvuka BMK.

Wanajua rasimu ya Warioba ikienda kwa wananchi kuizuia ni taabu sana.
Kumbuka wazanzibar walitaka mkataba, alternative yake ni S3

Hata kwa bara 2/3 inawezekana kabisa. Tatizo wabunge wa CCM wamesokomezwa matambara mdoni. Wapo kifungoni
Ni ngumu kuelewa wanasimamia nini wakiwa 'gerezani' lakini upo ushahidi wengi hawakubalini na mfumo uliopo.

Kama unafutilia, angalia waliobaki kuutetea mfumo huuni wangapi.
Wengi wamejitoa kwa kuelewa kuwa mwakani watasimama wenyewe mbele ya mahakama ya wananchi.

Disadvantage ya wabunge wa CCM ni kusema 'mimi nina msimamo ABC' kulingana na wananchi.
Hapo watakuwa na wakati mgumu kwenda kinyume na msimamo wa chama, wakati huo wakitakiwa kuwafariji wapiga kura.

Kwa upinzani, hilo litakuwa ni agenda ya vyama vyao. Watasema sisi, kwasababu imo katika ilani yao.
Hawatajitetea kama individuals

Kwa kuangalia hilo, wabunge wa CCM wamesoma hisia za wananchi wao. Ingekuwa mambo yamenyooka 2/3 ingepatikana.
Hapana.

Conclusions zangu zimetokana na matokeo ya kamati za Baraza la katiba,akidi, ulegevu na uishiwa nguvu wa UKAWA (It doesn't resonate to people as it used to, it's bogus),na hoja za wajumbe wa bunge la katiba kutoka zanzibar (CCM wanaonyesha kuwa na hoja zaidi ... na-base kwenye mdahalo wa ZIRP uliosimamiwa na Polepole na mdahalo wa Rose Mwakitwange Serena uliowahusisha Haji Duni na Ali Vuai).

CUF bado wanayumba sana kwenye kuelezea gharama, bado wana msimamo wa muungano wa mkataba na bado wana hoja ya kunyonywa na watanganyika wakati ukweli ni kuwa Tanganyika is the one being heavily exploited internally and externally.
Nitakupa mifano miwili kwanini CUF hawana hoja na wananchi wengi wameanza kugundua. Haji Duni alisema pale Serena kuwa, Tanzania tangu ianze kuvuna gesi, zanzibar haikufaidika lolote na gesi hiyo. Ukweli ni kuwa gesi ya Songosongo inatumika kuzalisha umeme ambao Zanzibar inakopa at a subsidized rate. Umeme wanaouziwa Zanzibar unakuwa subsidized na Treasury na bado hawawezi kuulipa.

Zaidi ya hapo, Polepole alishaambiwa na mwenyekiti wa PAC ya Baraza la wawakilishi kuwa Zanzibar haiwezi kuchangia hata 100bn out of the 2.1 trillion budget ya muungano (as cooked by Warioba's commission) na jinsi walivyojibu ilikuwa ni aibu tupu. Hata Awadh alijikanyaga siku ile. (I'm talking about ZIRP's debate).

Independents wengi wa Tanzania wanaanza kuona carelessness ya Tume ya Warioba with all due respect to the man. Ile tume imeleta draft moja ambayo haijatulia kabisa I can even dissect it easily kifungu by kifungu and I'm not even that educated.

Nguvu ya Serikali ya muungano, hoja ambayo nimekuwa nikibweka mara nyingi, inawasumbua moderates wengi wa Tanzania. Serikali imelegea na imekaaa kimkwara. Haina authority YA iNTERNATIONAL TRADE (REALLY?),Haina uwezo wa ku-create na ku-enforce National policies kwa sababu haina vyanzo vya fedha na haina kampuni ya maana unless STAMICO na TPDC ziwe za serikali ya muungano, at least we can have our own Gazprom. The media is not owned by the union government and our Ocean front will belong to the so-called nchi washirika.

The semi and well educated mass of Tanzanians wanaanza kuichambua hii draft na matokeo yake sidhani kama yatakuwa palatable kwa UKAWA. HATA CCM SASA WANAANZA KUJA KWENYE MIJADALA, and we all (me and you at least) know thats not the last card, the spade is still in the back pocket if you know what I mean.

Mwisho kabisa,sababu inayonifanya nione kuwa Zanzibar hakuna 67% ni CHADEMA. Samahani sana mkuu ila CUF kutogundua irrelevance ya CHADEMA kuna expose king yao easily. CHADEMA na CUF ni washirika wa kinafiki. Hii siyo siri kwa sababu kuna mengi yameshasemwa na kufanywa kati yao. Wazanzibari wanaanza kuona umuhimu wa kukaa na CCM kuliko CDM. Hiki ni chama pekee ambacho katika mchakato huu wa katiba, mpaka sasa ndicho kilichopigwa chini live na wananchi bila chenga kwa kukataliwa hoja yao ya majimbo (synonym to the dilution of the unity within Tanganyikans). Kama majimbo ndani ya Tanganyika yanawapa wananchi hisia ya kuzorotesha unity, will this be reflected in the proposed federal union as proposed by Warioba's commission? You can argue, but trust me, a big chunk of Tanzanians believe so.

To make things worse, wakati rasimu inaopolewa, CDM hiyohiyo ilipigwa chini kwenye chaguzi ndogo za local governments. Signalling their deteriorating grip in the political arena. CDM, as people are now observing, is not a good partner kwenye zoezi hili, matter of fact wangekaa tu pembeni kwa sasa hivi.

hayo ndiyo mambo yaliyonifanya nione kuwa itakuwa kazi sana kwa chama chochote kupata 67% Zanzibar as days go. Siku zinavyoenda ndiyo UKAWA wanavyopoteza. Je , wewe ni vitu gani vilivyokufanya uje na conclussions zako? Apart from umbeya kuwa kuna makundi na ugomvi na kusutana ndani ya CCM. Au , apart from Karume na Mansoor ambao sidhani kama hata kura watapiga?
 
Kobello
Ingalikuwa vema kama ungetenga hoja zako baina ya UKAWA na CDM. Hatudhani kuwa udhaifu wa UKAWA unaweza kuwa solely udhaifu wa CDM. Unless unajenga hoja kwa lengo la kushambulia, nadhani hapo hujatendea uchambuzi haki.

Katika mdahalo wa Serena, ukiatazama kwa umakini Vuai hakuwa anajibu maswali.
Nitakupa mfano, aliulizwa, wazanzibar kuanzia enzi za jumbe walitaka serikali 3,leo kimebadilika nini wanataka 2?
Vuai hakujibu kabisa. Alichosema ni kuwa rasimu ina tatizo la msingi kabisa bla bla bla.

Mdahalo ule, Pole pole na Awad walijibu vizuri sana hoja zilizokuwa na utata.
Ukirudi upande wa Duni Haji, alichokionyesha ni udhaifu wa baadhi ya viongozi kwa kuongozwa na jazba na ushabiki

Tatizo la Duni aliongelea Uzanzibar zaidi kuliko muungano.
Nakubaliana nawe kuwa suala la gesi alitia kinyaa. Mbali ya sababu ulizoeleza, Duni hakueleza kuwa muungano unaendeshwa na Tanganyika na gesi ni moja ta michango hiyo. Hakunasababu za mapato kupewa znz kwasababu tayari imebembea katika muungano.

Lakini Duni ameficha ukweli mkubwa sana, kwamba yeye akiwa kinara na Mansour ndio waliondoa gesi katika mambo ya muungano. Hivyo kama hawajaanza kuvuna gesi yao hawana sababu ya kulilia ya Tanganyika.

Huu ndio upuuzi ambao lazima Watanganyika waukatae. Zanzibar haiwezi kujificha na kutaka mafao kwa jina.

Kwa mtazamo huo, uwepo wa Tanganyika utasaidia sana kutenga shughuli hizi bila kulaumiana.
Kwa mfano, Tanganyika iwe na gesi yake na znz yake. Halafu tuangalie tunachangia vipi hili dude linaloitwa muungano.

Kuhusu mjadala wa ZIRRP, Salimin Awadhi wa CCM alisema hivi,'' kuwa na S3 znz itapoteza.
Hata kama ikiambiwa ichangie Bilioni 100 itakuwa imepoteza. Kwasasa haichangii, hivyo bilioni 100 ni nyingi na haitaweza''

Kobello, alichosema Salimin ni kuwa sasa hivi hawalipii hivyo likija suala la kulipia ni hasara kwao.
Nadhani hatuwatendei haki Watanganyika. Kwa sasa tunabeba mzigo wote wenyewe.
Je, Kobello hilo ni nafuu kuliko kuwaambia wachangie hata bilioni 50?

Kwa vile hawachangii muungano hiyo imekuwa haki yao na sasa wanatumia mwanya huo kuomba haki wasiyo na uchungu nayo. Tumeona tume ya Warioba tukibeba wenyewe, muungano wenyewe, wabunge wao tunawalipia n.k.
Nadhani S3 zitapunguza sana utegemezi na kuongeza uwajibikaji.

Kwa mfano, hatuna sababu za kulipia wabunge wa znz. Hatuna sababu za kulipia mishahara yao, hatuna sababu za kus subsidize bajeti yao na wala hatuna sababu ya kuwapa 4.5 ya pato letu kwa jina la muungano.

Uwepo wa Tanganyika una maana moja, zile gharama zisizotuhusu ziende kwao.
Hata kama watachangia bilioni 20, kuondoa gharama zisizotuhusu ni msaada sana kwetu.

Hapa hoja ya S3 inakuwa na nguvu zaidi labda unithibitishie vinginevyo

Katika mjadala wa Star TV, Shamsa Vua aliulizwa kama znz inaonewa. Alichokisema ni kuwa inanyimwa misaada. Akapendekeza kama barabara zinajengwa Muleba basi JMT itoe 4.5 iende zanzibar.
Hapa unaona jinsi wznz wanavyoongozwa na jazaba badala ya maarifa na weledi. Ni yale yale ya Duni haji

Shamsa Vua hajui kua ndani ya JMT wao hawana mchango na kwamba misaada inapokuja kuna madeni ya mikopo.
Mbona wznz hawaulizi wanachangia nini katika madeni ya taifa?

Bajeti yao haina mahali inaonyesha deni linalipwaj liwe la ndani ua nje.
Hivyo wanapodai misaada ije, tunauliza hivi Sumbawanga nao wadai nini maana mchango wao katika pato la taifa ambalo znz inachota 4.5 ni mkubwa kuliko wazanzibar ambao ni sifuri.

Hapa napo unaona haja ya kutenga hizi shughuli. Kinachotakiwa znz ipewe mamlaka ya kukopa na misaada na ilipe kwa kutumia njia zake. Tutaondokana na lawama zisizo na maana kwasababu hatunufaiki na chochote zaidi ya kuumiza wananchi wa Tanganyika.

Nimalizie kwa kusema, hata kama hoja zipo tatizo la wznz ni umimi na wanshindwa kuzijenga kwa weledi.
Wangeliangalia muungano kama ushirika wana hoja. Tatizo ni hilo la jazaba zaidi ya maarifa.

Umeona umuhimu wa kuzinduka kwa Tanganyika?

Nitaendelea kujibu hoja
 
Back
Top Bottom