Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #301
Mwalimu , JK aliwakwepa UKAWA kwa trick.Mkuu Nguruvi3
Hivi JK alikutana na UKAWA kwa mwamvuli wa TCD au ni kinyume chake? Kwa mtazamo wangu sioni kama alikutana na UKAWA. Japo wana-UKAWA walihudhuria mkutano ule lakini walihudhuria kwa kofia TCD na si vinginevyo. Makubaliano yoyote yale yaliofikiwa mule ndani ni baina ya JK na TCD sio UKAWA....
Labda wangeweza kususia kikao kile waiache TCD ya kina Cheyo na Mrema ndio waonane na JK peke yao ingawa bado najiuliza kama hatua hiyo ingeleta athari zipi...
Hakuwa amepanga kukutana na wapinzani, lakini pia hakuwa tayari kukutana na UKAWA kwasababu alitaka mahali pa kutokea.
Ndipo njia ya udanganyifu ikifanyika kutumia kituo cha Demokrasia ambacho mwenyekiti ni Cheyo.
Cheyo, Hamad Rashid, Mrema, Mapalala, Dovutwa n.k. wapo bungeni hna hivyo hakukuwa na issue ya kuzungumza na JK
Alichokifanya JK ni kuwaweka hao vibaraka ili watumike kama mpini.
Tuliwaonya UKAWA hapa jamvini, tukiwauliza ushirika na hao walioko bungeni umeanzaje?
Kama kawaida ya UKAWA, walidhani JK ni mwema kwao bila kujua anachezea akili zao kila siku.
Wamekwenda, vibaraka wakatumika kuwavuruga UKAWA na issue ikatoka kwa JK na kuwa ugomvi miongoni mwa TCD
Hata tangazo na debe la mazungumzo anayelisimamia ni Cheyo.
UKAWA tuliwaambia kabla ya mazungumzo hapa jamvini.
1. Hao wapinzani walioko bungeni wanakwenda kuonana na JK kwa sababu zipi?
2.Lini JK amekuwa mwema kwa UKAWA zaidi ya chama chake?
3. Kwanini bunge halisitishwi kupishamajadiliano?
4. Lini UKAWA wamefanya majadiliano na JK wakafanikiwa?
5. JK alipowavuruga wazee wa tume, lipi UKAWA walitegemea tofauti?
6. Wamejifunza nini kutokana na majadiliano ya siku za nyuma?
Maswali haya walipewa ili kuwafungua vichwa. Inashangaza wakaingia kichwa kichwa wakijua kabisa JK na serikali yake hawana nia wala kusudio la katiba mpya.
Leo Cheyo amepewa rungu anawaponda UKAWA, JK na CCM wakiwa wamejifungua kitanzi.
Hawa viongozi wa UKAWA kuna nyakati huwa najiuliza kama kweli wanajua michezo ya kisiasa.
Wamechezewa sana JK na wala hawaonekani kujifunza.
Huo ndio hasa mwanzo wa nyuzi hii inayohusu Juisi ya maembe. Wamekwenda wamekunya na nadhani walilewa.
Last edited by a moderator: