iNine9
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 4,412
- 8,198
Kuna kitu kinaitwa Tarrif nafikiri wengi hamkijui na ndo maana watu wengi mnalalamika kwanini unanunua umeme wa 5000/= afu unapata Units 14! Hapo ujie unatumia umeme wako ukiwa katika mfumo wa Tarrif One huu ni mfumo wa umeme wa viwandani na kama hujaenda kujaza form kubadilishiwa kwenda Tarrif Zero ambao ndo mfumo wa umeme wa majumbani ndo utapata hiyo TZS 100 kwa units 1 lakini chini ya Units 70 mpaka 70! Watanzania wengi hiki kitu huwa hawakijui kabisa na Tanesco hawakwambii wanapokufungia umeme kwa mara ya kwanza kwamba unakua kwenye default system ya Tarrif One (Matumizi ya umeme wa viwandani) mpaka pale utakapoenda jaza form ya kuamishwa kutoka huo mfumo! Sharti lake ukibadilishiwa huo mfumo sasa ni kwamba unatakiwa matumizi yako ya umeme yasizidi 10,000/= kwa mwezi, yakizidi kwa zaidi ya mara 3 automatically unarudishwa kwenye mfumo wa umeme wa viwandani sabu utaonekana una matumizi makubwa! Hapo inakubidi kusubili mwaka mzima tena ndo ukaombe tena! Binafsi nilkuja kupata uelewa huu 2014 nikafatilia na kubadilishiwa ndani ya siku 3 tu huko kijijini kwa bibi angu..! Toka huo mwaka nanunua units 8 kwa 1000 tu.. Kwa wastani natumia TZS 4000-5000 (Units 32-40) tu kwa ajili ya umeme mwezi mzima! Na matumizi yake ni TV,Taa ziko 9, Friji saa 24 inafanya kazi, pasi ya umeme japokua kwa nadra sana, brenda mara chache matumizi ya computers kuna wajukuu wanazo kule kwa bi mdashi wanatumia..