Ukiacha ya juzi haya aliyoyakoroga kwa kuropoka hovyo, Lisu is smart! The smartest Tanzanian Ever

Ukiacha ya juzi haya aliyoyakoroga kwa kuropoka hovyo, Lisu is smart! The smartest Tanzanian Ever

Unakuaje smart halafu unaropoka?

Kama huyu ndiye smartest Tanzanian sisi wengine ni meng'enyu meng'enyu kama hivyo
 
Lissu kaingia mtego wa influence peddling kwa Samia na Abdul kupata pasipoti yake na mafao.

The smartest Tanzanian would not do that.
We unadhani yeye hajui anachokifanya na matokeo yake?
 
We unadhani yeye hajui anachokifanya na matokeo yake?
Anajua kuwa Watanzania wengi standards zao ziko chini sana kuweza kuona hili kuwa ni tatizo.

Rushwa ya fadhila haieleweki Tanzania. Watanzania washaizoea. Wameshaifanya kuwa ni sehemu ya maisha yao.

Majibu ya watu wengi kwenye uzi huu tu ni kielelezo kwamba rushwa ya fadhila ama haieleweki, ama hata ikieleweka, haionekani kuwa ni tatizo.

Kila mtu anataka kuwa na "mtu wake" wa kumrahisihia mambo katika kila ofisi muhimu.

Wengine utawasikia kabisa kabla ya kwenda ofisi fulani wasiyomjua mtu wanauliza "Nani anamjua mtu wa ofisi fulani?" ili wapate upendeleo kupata huduma. Watu hawana imani na mifumo, mifumo imewaangusha, hawataki kutengeneza mifumo, wanataka shortcuts za kufanya mambo kwa kujuana. Tundu Lissu naye kaangukia humo.

Watu hawafikirii kutatua tatizo la kimfumo kila mtu apate huduma kwa haki bila kuhitaji upendeleo wa mtu wake kwenye hizi ofisi.

Pengine hata Tundu Lissu anaijua na kuikataa rushwa ya fadhila kinadharia, lakini kiutamaduni kama Mtanzania ameikubali na anaona kukikataa ni vigumu sana.

Watanzania wamekuwa kama samaki anayeishi kwenye maji maisha yake yote, ameshayazoea maji mpaka hajui kuwa anaishi kwenye maji.

Rushwa ya fadhila kwa Watanzania imekuwa kama maji kwa huyo samaki.

Ndiyo maana hata katika uzi huu, kuielezea rushwa ya fadhila inakuwa vigumu.

Namfafanulia mtu kuwa kupewa fadhila ili kupata haki yako ni rushwa.

Halafu mtu anauliza, lakini si anapata haki yake, rushwa iko wapi hapo?

Ile fadhila anayopewa mtu ili kupata haki yake haitambuliki kuwa ni rushwa.

Samaki kazoea maji mpaka hayatambui kuwa haya ni maji.
 
Back
Top Bottom