Ukiachana na bei za Saruji, bei ya kupata Kibali cha ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu huko Halmashauri ya Kigamboni ni Tshs 250,000

Mbona hiyo table umeisoma vibaya, kwa eneo la ukubwa uisozidi 200 sq M gharama haifiki 200000 Tsh. Pia nauliza, kwani hzo gharama zinatofautina halmashauri moja na nyingine au zipo uniform?
 
Mbona hiyo table umeisoma vibaya, kwa eneo la ukubwa uisozidi 200 sq M gharama haifiki 200000 Tsh. Pia nauliza, kwani hzo gharama zinatofautina halmashauri moja na nyingine au zipo uniform?
Soma Tena utaelewa, 156 inaangukia kwenye kundi gani hapo,? Pia katika huyo bei ongeza elfu kama ada ya file kuweza kukaliwa yaani ada ya maombi(application fee)
 
Njoo Chanika, kibali ni kiwanja chako tu
 
Gharama ni kubwa sana !

Halafu huo urasimu katika kuomba hata kukipata hicho kibali utachoka mwenyewe!

Yani upitie serikali ya mtaa uende Halmashauri, umchukue afisa mipango miji akachukue coordinates na umlipe posho, akishachukua cordinates usubiri hadithi na nenda rudi danadana na wewe, ikifika wizara ya ardhi ndiyo kabisaaaa kukatishwa tamaa kwisha na mwananchi kuanza kugairi kuanza kujenga eneo husika!
 
Ni kama wamewatafutia watu chanzo cha madeal ya kula za wananchi.
 
Je vibali hivyo ni kwa maeneo yaliyopimwa tu au hata ambayo bado hayajapimwa?
 
Hizi ni za nini?

Serikali inachukua mapato kila sehemu.

1 manunuzi ya kiwanja.
2 kibali
3 mchoro
4 material
5 kodi (kwa watumishi)PAYE
6 kodi ya jengo kila mwaka.

Hii ndo serikali ya wanyonge au wanyongwa?
 
Hizi ni za nini?

Serikali inachukua mapato kila sehemu.

1 manunuzi ya kiwanja.
2 kibali
3 mchoro
4 material
5 kodi (kwa watumishi)PAYE
6 kodi ya jengo kila mwaka.

Hii ndo serikali ya wanyonge au wanyongwa?
Ebu waza nyumba ndogo kama ya vyumba vitatu wanataka pesa nyingi hivi za nini?
 
Kuanzia lini?
 
Duh! Wacha nikakiuze tuu changu nikajenge huko kilwa
 
Mbona kibali ni laki moja huku halmashauri tatzo mko kwenye majiji
 
Mimi wakati nafuatilia kibali cha ujenzi nilicheka sana. Nilipigwa danadana mpaka nikaona bora nihonge tu yaishe maana la sivyo ningemaliza hela yote ya ujenzi kabla kibali hakijatoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…