Ukiachana na bei za Saruji, bei ya kupata Kibali cha ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu huko Halmashauri ya Kigamboni ni Tshs 250,000

Ukiachana na bei za Saruji, bei ya kupata Kibali cha ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu huko Halmashauri ya Kigamboni ni Tshs 250,000

Mimi wakati nafuatilia kibali cha ujenzi nilicheka sana. Nilipigwa danadana mpaka nikaona bora nihonge tu yaishe maana la sivyo ningemaliza hela yote ya ujenzi kabla kibali hakijatoka.
Kabisa mkuu
 
Gharama ni kubwa sana !

Halafu huo urasimu katika kuomba hata kukipata hicho kibali utachoka mwenyewe!

Yani upitie serikali ya mtaa uende Halmashauri, umchukue afisa mipango miji akachukue coordinates na umlipe posho, akishachukua cordinates usubiri hadithi na nenda rudi danadana na wewe, ikifika wizara ya ardhi ndiyo kabisaaaa kukatishwa tamaa kwisha na mwananchi kuanza kugairi kuanza kujenga eneo husika!
Kila hatua ni pesa
 
Wakati tukiendelea kumtafta mchawi aliyepandisha Cement!

Tutafakari gharama za kibari cha ujenzi huko halmashauri ya Kigamboni zilivyokubwa zilizo tiwa baraka na ofisi ya Mkurugenzi kwa ajili ya kutunisha mfuko wa manispaa!

Bei ya kibali cha ujenzi wa nyumba ndogo kabisa ya vyumba vitatu na sebule kwenye kiwanja cha upana (12m kwa 13m) ambapo ni sawa mita za mraba 156 ni TSh 200,000 (laki mbili) na ada ya maombi ni Tsh 50,000 JUMLA NI 250,000/=

Ikumbukwe hapo hujajumlisha gharama za michoro ya ujenzi na Nauli za saveyi ambapo ukiongeza na huyo 250k zaweka fikia laki Saba jumla!

250,000 ni sawa na mifuko 17 ya cement inatosha kabisa kujenga msingi!

Kwanza kwanini msitoze Square mita moja hata tsh 200? Ili watu wengi watamani kuja kuomba kibali?

View attachment 1631309
Ulaya mambo yapo hivi
 
Kihere here chako kimekuponza.. Kwa nini uombe kibali? We anza kujenga mpaka uandikiwe kwenye nyumba yako 'Simamisha ushenzi' ndipo uwatafute.

Zamani tulikuwa tunaambiwa, soma mpaka ukute kibao kimeandikwa, 'there is no school for you' ndipo uache.
Mkuu
 
Back
Top Bottom