Ukiachana na ranks, kwa score bado mazingira ya habari ni magumu

Ukiachana na ranks, kwa score bado mazingira ya habari ni magumu

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Mei 3, watu wengi walifurahi kuona Tanzania imepanda kwa nafasi 40 kwenye uhuru wa habari duniani. Yaani mwaka 2023 ilikuwa ya 143, lakini mwaka 2024 imekuwa ya 97. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Reporters without Borders.

Hata hivyo, ripoti ile inaweka score kwa kila nchi na kila score ina maana yake kwa kadiri walivyoeleza. Bofya HAPA angalia wenyewe wameeleza namna score zinamaanisha. Nenda utaona hii map kwa chini. Kwa mwaka 2023 na 2024, nchi ikiscore chini ya 55 ambapo inakuwa na rangi ya chungwa, ni "Difficult", yaani uhuru wa habari una hali ngumu.


Screenshot 2024-05-16 101012.png

Tanzania imescore 54.8, na imewekwa rangi ya Orange, means bado uhuru wa habari nchini ni magumu. Tulichokifanya mwaka huu ni sawa na kufurahia mtoto kuwa wa kwanza kwenye shule ya kijijini kwa kudhani mwanao ni mkali, kumbe sio mkali kwa ukweli bali ni mbumbumbu tu. Yaani mtu anapata 30% ila anaongoza darasa halafu mzazi unafurahia, akifeli kwenye NECTA unasema karogwa.


Angalia score za Tanzania hapa
Screenshot 2024-05-16 101119.png
Screenshot 2024-05-16 100931.png
 
Habari kwa tz hutolewa pale mtoa habari anapotaka kutoa na Wala hakuna namna analazimishwa hata ikiwa ni kwa maslahi ya uma
Huwa naangalia wasemaji wa vilabu vyetu na wasemaji wa taasisi wanavyowanyanyasa waandishi (kwa maneno) hadi nasema wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana
 
Back
Top Bottom