Ukiachana na tabia za kimtandao wewe ni mtu wa aina gani?

Ukiachana na tabia za kimtandao wewe ni mtu wa aina gani?

yuzazifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2018
Posts
5,108
Reaction score
9,436
Natumai hamjambo wanabodi,

Wakuu sio siri mitandao ya kijamii imetupatia tabia mpya ambazo katika uhalisia hatuna, tabia hizi za kimtandao zimetufanya tuwe na mbwembwe, show off, chai na mizaha mingi kupitia post na comment zetu.

Tabia za kimtandao mara nyingi hutumiwa na wahusika katika kuitafuta furaha na faraja ambayo inakosekana katika maisha halisi, tabia hii ya kimtandao inamadhara pia coz kuna baadhi huichukulia kua ndo tabia yako halisi, mfano kuna watu huku wanaweza tukana na kutoa maneno ya shombo bt katika maisha ya halisi hawawezi fanya hivo hata wakiudhiwa.

Mfano kuna huyu mwamba ZERO IQ post zake nyingi huzungumzia uchakataji wa papuchi bt unaeza kuta papuchi hizo hua anazichakata hapa mtandaoni kwa maandishi na katika maisha yake halisi ni mtu wa tofauti sana.

Binafsi ukiachana na tabia za kimtandao ni mtu mpole, mkarimu, sina maneno mengi, inshort katika maisha halisi mi ni mtu wa watu.

Je, kwa upande wako ukiachana na tabia za kimtandao we ni mtu wa aina gani?
 
Mimi ninavyoishi mitandaoni na uhalisia ndio sawa sawa.
sawa bt bado kuna tabia za kimtandao ambazo huna katika maisha halisi, mfano mtu anaeza kuomba ushauri hapa ndani bt robo3 ya wachangiaji wakamkejeli na kuleta mzaha kitu ambacho katika maisha halisi huwez fanya mtu akikutaka ushauri.
 
Back
Top Bottom