Ukiagiza bidhaa au gari na ukakwama ushuru ni vyema baada ya gari kufika ukapeleka Bonded Warehouse.

Unavyoandika kama vile hauna ubongo!! Hivi unaishi wapi?
 
Usalama unakuaje?? Hawachelewi kukubadirishia spare parts
Usalama ni mkubwa sana, moja ya masharti ya kufungua Bonded Warehous e inabidi eneo liwe limewekewa fence, CCTV camera. Na endapo itatokea wizi ukapeleka malalamiko kwa mhusika akagoma kuwajibika ukienda kuripoti Tasac/TRA hiyo Bonded Warehouse inafungiwa na mmiliki anafunguliwa Kesi ya uhujumu uchumi maana wizi umefanyika kwa bidhaa ambayo ilikuwa chini ya uangalizi.

Pia hakuna mmiliki anayelea wizi kwenye Bonded Warehouse maana kawekeza pesa ndefu( moja ya sharti la kupewa leseni lazima uwe na mtaji usiopungua 500million) na sheria kali zinambana akifanya kosa anaingia kwenye uhujumu uchumi.

Pitia link hii ya TRA usome vigezo vya kuanzisha Custom Bonded Warehouse
 
Unajua kitu kinaitwa Uplifting ?!!! Unaweza ukaja na mzigo wako unamenunua bei ya kishikaji huko nje jamaa wakapinga invoice yako na wakaingia kwenye vitabu vyao na kuja na bei zao Yaani unashangaa mzigo umekuwa na gharama (Kodi zaidi ya mara Kumi) bei uliyonunulia..., Nadhani wewe ni mgeni nchini.... Anyway hii ya bonded warehouse ni kutibu symptoms badala ya kutibu tatizo... Na tatizo ni Kodi za Ajabu Ajabu...

 
Dah!! Umetisha mkuu!! TRA wanapaswa kukulipa posho kwani hii ni elimu kwa wateja wao.
 
Asante sana kwa andiko zuri na la kuelimisha; je mzigo unaweza kuwekwa kwenye bonded warehouse kwa muda gani. Kuna time limit?
 
Kuagiza gari na hauna hela ya kulipa hizo expenses hizo ndo tunaita harakati za pimbi
 
Kuna bonded warehouse moja mitaa ya Akachube, ina gari zipo pale nahisi zaidi ya miaka 4 huoni hata zikisogezwa wala kufutwa vumbi...

Zile hata zikipigwa mnada si ajabu zikauzwa bei kubwa sana kufidia deni...
 
Sio kila kitu ni kukurupuka mzee, au wewe hujawahi kukumbwa na dharura?? Sio poa kabisa unaweza kulala masikini ukaamka tajiri au the vice versa

Jana ulikuwa na milioni 100 ya kucheba after days ukajikuta hauna hata 10 na deni la negative 30+ huko

Dharura inaweza kukuchachafya ukaona dunia chungu ilhali kila siku ulikuwa unapanda juu ya meza na kurusha maburungutu kwa kadamnasi
 
Sawa,
Ila Sasa unakuta mpaka TRA wakuruhusu hilo lazima uwe uneeakatia kadhaa. Kila mtu pale anakula Kwa urefu wa kamba yake kama alivyoruhusu Maza.
 
Sawa,
Ila Sasa unakuta mpaka TRA wakuruhusu hilo lazima uwe uneeakatia kadhaa. Kila mtu pale anakula Kwa urefu wa kamba yake kama alivyoruhusu Maza.
TRA hawasumbui mkuu, ni wepesi wa wakala wako wa forodha (Clearing Agent) kujaza fomu na kuomba nafasi kwenye Bonded Warehouse unayotaka
 
TRA hawasumbui mkuu, ni wepesi wa wakala wako wa forodha (Clearing Agent) kujaza fomu na kuomba nafasi kwenye Bonded Warehouse unayotaka
Aisee,
Na huko Bonded maximum inaweza kukaa muda gani?
Je kwenye kuomba TRA naweza kukataliwa pia?
 
Huyo jamaa uliyemnukuu ni kiazi sana, yaani ameandika tu utafikiri Hana kichwa...

Bandiko lake limejikita kuwalaumu vijana ambao ni wahanga wa mfumo mbovu wa Kodi pasipo hata kuangalia chanzo Cha wao kuonekana kama wamekurupuka.

SI ajabu huyo utakuta ni Mmoja ya wafanyakazi wanaohusika na mambo ya forodha huko bandarini na ni mnufaika WA mfumo kandamizi WA Kodi.
 
Aisee,
Na huko Bonded maximum inaweza kukaa muda gani?
Je kwenye kuomba TRA naweza kukataliwa pia?
Hakuna limit ya kukaa, kukataliwa hakupo labda uwe ujakamilisha vitu au mzigo ukawa na mashaka. Mzigo ukiwa Bonded bado unakuwa upo chini ya TRA kwaiyo hapo kinachofanyika ni kubadili eneo la kutunza mizigo kutoka Bandarini kwenda Bonded Warehouse ambapo gharama za kutunza mizigo (storage charges) zipo chini.

Kwenye kila Bonded Warehouse kuna ofisi rasmi za TRA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…