Usalama ni mkubwa sana, moja ya masharti ya kufungua Bonded Warehous e inabidi eneo liwe limewekewa fence, CCTV camera. Na endapo itatokea wizi ukapeleka malalamiko kwa mhusika akagoma kuwajibika ukienda kuripoti Tasac/TRA hiyo Bonded Warehouse inafungiwa na mmiliki anafunguliwa Kesi ya uhujumu uchumi maana wizi umefanyika kwa bidhaa ambayo ilikuwa chini ya uangalizi.
Pia hakuna mmiliki anayelea wizi kwenye Bonded Warehouse maana kawekeza pesa ndefu( moja ya sharti la kupewa leseni lazima uwe na mtaji usiopungua 500million) na sheria kali zinambana akifanya kosa anaingia kwenye uhujumu uchumi.
Pitia link hii ya TRA usome vigezo vya kuanzisha Custom Bonded Warehouse
www.tra.go.tz