Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

You done everything my friend
 
Kumbe Chanika nako kumekucha, mimi nilifikiri kumedolola kiaina.
 
Hapo kama ni fursa ya kuchagua japo viwanja viwili basi nitachagua kwanza kibaha alafu cha pili kitakuwa cha bagamoyo.

Huko chanika na vikindu yake kuna wafaa waswahili kama kina kingwendu nk.
Hapo tuseme jibu lako limeegemea zaidi Kibaha, maana mfano ni kiwanja kimoja tu.
 
Hapo tuseme jibu lako limeegemea zaidi Kibaha, maana mfano ni kiwanja kimoja tu.
Nakushauri tena.

Njoo haraka sana Bagamoyo.

Ntarudi hapa mwezi wa kumi na mbili mwaka huu kukukumbusha kwanini unapaswa uje Bagamoyo.

Wenye pua za kunusa fursa wote wanaamia Bagamoyo.

Hata hao madon wa kibaha sasa wananunua mashamba na viwanja kwa fujo sana Bagamoyo.
 
Hongera uko vizuri sana.
 
Kalibu sana CHANIKA kuko njema kumbuka hata makamo wa Samia kwake ni CHANIKA brother
 
Hata mimi kura yangu naipeleka Kibaha,sababu ni miundo mbinu iliyopo na itakayokuwepo,Bandari kavu ya Kwala na muunganiko utakaokuwepo na Bandari ya Bagamoyo bila kusahau uanzishwaji wa viwanda vingi ndani ya Kibaha na Bagamoyo kwa ujumla
 
Vikindu ipo kilometa 23.6 kutoka katikati ya jiji Kariakoo na sio kilometa 45 ulizosema na ushahidi wa Google map ikionesha umbali toka Vikindu hadi Kariakoo nimekuwekea hapo, Ila kwa hapo 1.Chanika na 2.Kibaha ndizo sehemu nzuri
Nimetumia neno takribani maana yake ni makadilio.

Halafu sijui kama unafahamu unaweza toka vikindu mpaka kariakoo kwa njia tofauti, je umbali wa njia zote tatu ni 23.6km mpaka kariakoo?

Mandela road to kariakoo via Nyerere road.
Kilwa road to kariakoo
Same distance?
 
Chanika inakua kwa kasi sana.

Huko kwengine bado bushi.
 
Asante mkuu, acha niutafakari ushauri wako na kuufanyia kazi haraka iwezekanavyo.
 
Kalibu sana CHANIKA kuko njema kumbuka hata makamo wa Samia kwake ni CHANIKA brother
Ya hilo nalifahamu mkuu. Kabla ya kuchukua uamuzi nataka kwanza nifunge safari nije mimi mwenyewe kupaona. Wanasema kusadiki kwa toma ni kujionea.

Nina binam yangu amejenga na kuhamia huko, japo mimi binafsi sijawahi kuja kumtembelea kutokana hatuna mazoea kwa sana. But nitajitahidi siku 1 nimtembelee ili nijionee mwenyewe kile ulichoandika hapa. Asante sana
 
Hata mimi kura yangu naipeleka Kibaha,sababu ni miundo mbinu iliyopo na itakayokuwepo,Bandari kavu ya Kwala na muunganiko utakaokuwepo na Bandari ya Bagamoyo bila kusahau uanzishwaji wa viwanda vingi ndani ya Kibaha na Bagamoyo kwa ujumla
Wengi wame prefer kwa Kibaha, japo Bagamoyo na Chanika nayo si haba, zina watu wengi wanaozikubali.
 
wengi hawawez kuliona hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…