Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Mangi, huwezi kukimbia uswahili ukitaka kujenga miji ya waswahili. Sehemu yoyote iwe Pwani au Dar uswahili upo. Kila jamii Ina tabia zake uhwezi kuzkwepa. All in all sehemu yoyote Ile ndani ya Pwani au Ina thamani kuliko kishumun#du
Sijasema ukimbie maeneo ya waswahili, mimi nimesema maeneo yenye ngome za kiswahili sio za kukimbilia ovyo ovyo kwenda kujenga ili kuishi. Kwanini? Miji yenye ngome za kiswahili ina tabia ya kudumaa, kuzubaa na kubakia hivyo hivyo bila kubadilika.

Unajua maana ya ngome za waswahili?
Hayo ni maeneo yenye kuwatambulisha waswahili, kuloea, kufia, kuzikwa vizazi vyao. Haijarishi maisha yatabadilika vipi kuwazunguka au kuwakaribia, mswahili akiwa kwenye ngome yake atataka kukomaa hivyo hivyo na ukale wake, uvivu, majungu nk.
 
Vikindu ipo kilometa 23.6 kutoka katikati ya jiji Kariakoo na sio kilometa 45 ulizosema na ushahidi wa Google map ikionesha umbali toka Vikindu hadi Kariakoo nimekuwekea hapo, Ila kwa hapo 1.Chanika na 2.Kibaha ndizo sehemu nzuri
Inamaana Vikindu ni Klmr chache tu namna hii kutoka K'koo. Basi hii ilistahili kuwa ndani ya Dar es salaam kuliko Chanika.
 
Kwahiyo mkuu unaona Kibaha haikupaswa kulinganishwa na hayo maeneo mengi, inamaana hata Bagamoyo hauikubali mkuu?
makao makuu ya mkoa halaf unafananisha na vitongoj vyake kwel wametumia akili hao ? Vikindu na Bagamoyo zote zipo mkoa wa pwan ambazo zote makao makuu ni kibaha
 
Ulichoandika kama kina ukweli fulani. Maana angalia Mw/nyamala, Mburahati, Kigogo, Buguruni nk hayo ni maeneo ya waswahili. Pamoja na kwamba maeneo hayo yapo katikati ya mji ambapo mtu unaweza kutembea kwa mguu kwenda K'koo, Posta nk, pia muingiliano wa watu mbali mbali kutoka maeneo tofauti ya nchi lakini maeneo yao yapo vilevile miaka nenda miaka rudi.
 
Mkuu yaani vikindu ni mbali kuliko kibaha? Ukitokea kati kati ya Jiji , hebu nenda kafanye calculations upya aisee , unegesemea miundombinu sawa lakini c umbali mkuu
 
Nani huyo anayegawa viwanjwa vya Bure ? Tupeane fursa hiyo mkuu
 
Je waweza fafanua zaidi, sababu ni nini hasa?
1. Bei ya viwanja ipo chini sana.

2. Gharama za ujenzi ni ndogo.

3. Mazingira ya kuishi na watu wa ina ile ile waliokuwa wanaishi nao Manzese, Mburahati, Kigogo nk wanasema ndege wafananao huruka pamoja.

Wengi ni wafanya biashara ndogo ndogo kama vile samaki, machungwa nk, hivyo watu wa maeneo hayo ndo wataweza kuzimudu bei za biashara zao nk.
 
Du kumbe katika sehemu nilizotaja kuna maeneo uswahili ni wa kiwango cha juu namna hii.

Acha mtu asikilizie Kibaha kwanza.
 
Kibaha
 
Naiona Kibaha ikienda kuwa na maendeleo makubwa siku za usoni. Nimefuatilia kwa makini na kuliona hili kupitia wingi wa comment na sifa inazopewa wilaya hiyo ya mkoa wa Pwani.
Kibaha panafaa sana kwa makazi na kibiashara pameshakuwa na watu wengi sana siku hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…