Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Ukiambiwa kuna viwanja vya bure uchague tu sehemu ya kujenga na kuishi kati ya Vikindu, Kibaha, Chanika na Bagamoyo, utachagua kujenga wapi?

Wengi wanaosapoti Kibaha wanapaangalia pale Maili Moja, Kwa Mfipa, Kwa Mathias hadi Kongowe tena barabarani. Hivi mmewahi kuingia huko ndani ndani kwenye viwanja vinakouzwa? Ni uzaramoni haswaaaaa, ni uswahili sana.

As for Bagamoyo, ule mji mimi hapana. Haujawahi kunivutia.
Labda maeneo kama Zinga huku nyuma kabla hujafika Bagamoyo kwenyewe. Bagamoyo ni mji usioendelea kwa miaka mingi.

Chanika, sehemu nzuri mwisho pale Taliani. Huko mbele sijui Zingiziwa, kwa Mpango sjui wapi huko ni mateso tu. Na uswahilini sana.

Vikindu, ubaya wa Vikindu ina jamii mchanganyiko lakini wamekaa vikundi vikundi. Unaweza kwenda sehemu wamejaa Wapare watupu mtaa mzima viwanja vyote wanamiliki wao. Kuna sehemu unaenda wamejaa Wamakonde watupu, ipo sehemu ina Wandengereko tupu. Hawa wengi ni zao la machinga wa Mbagala na waliouza nyumba za urithi au zao wenyewe Tandika na Mbagala/Magomeni wamekimbilia huko.

Ceteris Paribus, Kibaha is promising. Ile barabara kutoka pale Maili Moja wanataka iwe njia 4 hadi Chalinze so kutakuwa magoli sana. Maroli hayatakuja mjini kwa sababu Kwala wanajenga bandari kavu.

Kumbuka mkoa wa Pwani ndio mkoa pekee Tz usiokuwa na Manispaa.
Hata mkoa wa songwe, njombe,katavi nazo pia hazina manispaa
 
Kibaha and Bogamoyo...

Cc: Mahondaw
Kifupi huko ndo kunafaa, maana watu wengi wameyachagua hayo maeneo.

Inaonekana maeneo mengine hasa pande za kusini mwa mkoa wa Dar es salaam bado yana safari ndefu ya kupata watu wa maana wa kwenda kuishi kule.
 
Mimi bagamoyo na ukanda wake naona kama kumekaa kushoto hivi, yaani ni kama sehemu ya wachawi wachawi hivi! Kibaha nako kumekaa kimkoani mkoani hivi!
Chanika nayo imekaa kiswahili Swahili hivi, kwa ufupi mbagara ya baadae.

Walau Vikindu naweza kuweka boma langu!
🤣🤣🤣🤣🤣🤣vikindu over bagamoyo?🤣
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣vikindu over bagamoyo?🤣
Mdau anashangaza sana. Kwamba hajui kuwa Bagamoyo ndio Mbweni, Masaki, Salasala, Mikocheni, Goba na Mbezi beach ijayo 😄😃😂
 
Mdau anashangaza sana. Kwamba hajui kuwa Bagamoyo ndio Mbweni, Masaki, Salasala, Mikocheni, Goba na Mbezi beach ijayo 😄😃😂
Sema wewe tena kwa sauti kubwa aisee🙌 Bagamoyo ni uzunguni hakuna mfano. Yani kuna mitaa saizi ni ulaya hasa opposite na eneo
Lote na bandari
 
Sema wewe tena kwa sauti kubwa aisee🙌 Bagamoyo ni uzunguni hakuna mfano. Yani kuna mitaa saizi ni ulaya hasa opposite na eneo
Lote na bandari
Huenda ni mkazi wa huko huko Vikindu, ndomaana amekimbilia kupatetea. Lakin pia inaonekana hajawahi kufika au hata kuisikia Bagamoyo vizuri, ndomana kaandika alichoandika.
 
Niaje waungwana,

Kama swali linavojieleza hapo juu, ukiambiwa uchague sehemu moja tu ya kujenga kwa ajili ya makazi kati ya Chanika, Kibaha, Vikindu na Bagamoyo ila kiwanja unapewa bure.

Ndugu muungwana hebu tuambie utachagua kujenga na kuishi wapi? Na kwanini?
Inategemea ,
Mfano kama wewe chimbuko ni kusini chagua vikindu,
Kama mzaramo chagua chanika, kama mikoa ya kati na bara chagua kibaha, kama ukanda wa kaskaz chagua Bagamoyo .
Regardless of all preferably nimechagua Bagamoyo.

Sisi tuliozaliwa Dar lakin hatuna asili ya Pwani wala kusini huwa tunachagua popote.

Kwangu mimi ukiacha Dar, sehem nyingin ambayo naweza kununua nikajenga ni Kibaha na Bagamoyo tu.
 
Sisi tuliozaliwa Dar lakin hatuna asili ya Pwani wala kusini huwa tunachagua popote.

Kwangu mimi ukiacha Dar, sehem nyingin ambayo naweza kununua nikajenga ni Kibaha na Bagamoyo tu.

Ni kweli,
Kama ni machaguo mawili na mimi ningechagua kama wewe,
Lakini kama ni Chaguo moja ningechagua Bagamoyo .
 
Back
Top Bottom