Ukiambiwa unanuka kikwapa utafanyaje? Utakasirika?

Ukiambiwa unanuka kikwapa utafanyaje? Utakasirika?

Pape

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2008
Posts
5,487
Reaction score
83
Fikiria kwamba wewe ni mfanyakazi wa kampuni fulani! Unamtokea mdada/mkaka ambaye unampenda sana na ni mfanyakazi mwenzako. Kwa maringo huyo mdada/mkaka anakujibu kwamba hakutaki kwasababu unanuka kikwapa! Je, hali kama hii ikikukuta utachukua uamuzi gani? Utamtukana? Utampotezea? Utaendelea kupiga nae story au utakata mawasiliano kabisa?
 
nitaendelea kupiga nae story halafu kesho yake nitaoga vizuri na kutia deodorant then namfuata kumuuliza kama bado nanuka
 
nitaendelea kupiga nae story halafu kesho yake nitaoga vizuri na kutia deodorant then namfuata kumuuliza kama bado nanuka
hahahahahaha, duh hii ndiyo tunaita ung'ang'anizi!
 
mtu anapokuambia udhaifu wako unapaswa kumshukuru maana utaufanyia kazi
kuliko yule anayekwenda kukusema kwa watu bora huyo anayekwambia laivu kakusaidia
 
ha ha ha itabidi umuulize ni hilo tu ama kuna lingine!! maana unaweza weka 'deodorant' thena akaja na ishu nyingine kama "sipendi mavazi yako' ukisoma btn the lines" inadepend na jamaa alivyo mtokea huyo demu maana hii nayo shughuli!!
 
kwa kweli nitajisikia vibaya alafu ata ule ujasiri wakumtokea tane unapotea so nitafanyia kazi kile alichoniambia nitajisopusopu nitanunua kaperfumu nitatafuta mwingine
 
kwa kweli nitajisikia vibaya alafu ata ule ujasiri wakumtokea tane unapotea so nitafanyia kazi kile alichoniambia nitajisopusopu nitanunua kaperfumu nitatafuta mwingine
It sound good!
 
Daima mtu anayekwambia ukweli na kama ni kweli kile anachokuambia basi huyo anaonyesha kwamba anakupenda sana kwa maana anakusaidia wewe kujirekebisha. Wewe kama unanuka kaonge na kesho yake endelea kupiga naye story ukiwa safi. Haiwezekani mtu asikuambie ukweli halafu mwishowe atapike bure kwa sababu ya maharufu yako kisa eti hutaki akwambie ukweil. UKWELI UNAUMA LAKINI.
 
kama unanuka ingebidi hata kama hakutaki akwambie kwa njia ya kistaarabu lkn sio kukwambia kimaringo maana lazima utajisikia vibaya na ingekuwa mie nisingeweza kuendeleza story maana nitajistukia labda anahisi na mdomo wangu unanuka!
 
its nice to hear from you dada cheusi mangala!
 
Nitamshukuru aliyeniambia kwa kuniambia ukweli
kisha nitamuuliza nifanyeje ili kuepukana na hali hiyo
nitumie deorant ipi, niogee sabuni gani, ushauri mwingine
kama akisema hajui nitamshukuru tu na kwenda zangu bafuni kuonga
 
nitafurahi sana kwani nitakuwa na uhakika wa kumpata 100%.............. kwani kwa uzoefu w\angu, huyu ndiye rahisi zaidi kumpata............ hahaha................ wanosema watajisikia vibaya mna tatizo inferiority complex...............
 
Mimi nitajinusa nione kama kweli nanuka au la! Sikubali kirahisirahisi tu...
 
fikiria kwamba wewe ni mfanyakazi wa kampuni fulani! Unamtokea mdada/mkaka ambaye unampenda sana na ni mfanyakazi mwenzako. Kwa maringo huyo mdada/mkaka anakujibu kwamba hakutaki kwasababu unanuka kikwapa! Je, hali kama hii ikikukuta utachukua uamuzi gani? Utamtukana? Utampotezea? Utaendelea kupiga nae story au utakata mawasiliano kabisa?

ntamwambia sinuki kikwapa ila harufu anayoisikia inatokea kwenye soksi zake.
 
nitaendelea kupiga nae story halafu kesho yake nitaoga vizuri na kutia deodorant then namfuata kumuuliza kama bado nanuka
jamani mnavunja mbavu zangu nyie vijana!sasa akisema bado unanuka je!hahaa lol!
 
Akisema bado nanuka kama ni mimi nitamwomba akaniogeshe!
huyo mwenye maringo si atakuogesha na mpira wa maji huku yeye kasimamia kule mbali akiwa kaziba pua!
au unadhani ndio utakuwa umepata fursa ya kuwa karibu na kimwana bafuni!lol
 
huyo mwenye maringo si atakuogesha na mpira wa maji huku yeye kasimamia kule mbali akiwa kaziba pua!
au unadhani ndio utakuwa umepata fursa ya kuwa karibu na kimwana bafuni!lol
hahahahahaha simba mkali na anazaa! sembuse binadamu!
 
Back
Top Bottom