Katika Afrika,Tanzania inashika nafasi ya 9 kwa kuwa na watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri. Ushuhuda wa hilo ni haya ya SIMBA NA YANGA,CCM,MANDONGA na mengine ya hivyo. Kuna watu wazima wanaamka asubuhi breki ya kwanza ni kwenye kibanda cha magazeti na kuanza ubishi wa Azizi Ki,Mayele,na Chama mpaka saa 7 mchana na hao ni watu wana familia. Mpira umeleta ujinga ambao sijapata kuona,mtu anafunga duka kwenda kuangalia Yanga huyohuyo baadaye anashindwa kupeleka marejesho ya mkopo na anakimbia familia. Ukimuuliza anakwambia karogwa. Nashukuru mleta huzi kwa kuliona jambo hilo.