Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Utamuuliza swali gani mama yetu?Hongera mama , chonde chonde ! Endeleza kazi ya marehemu JPM ,kaza uzi ule ule .
Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Utamuuliza swali gani mama yetu?Nitamwambia, "ww mama utairudisha nchi hii kwenye ubadhirifu wa utawala wa JK, jitetee"!
Safi sana mkuu...Nitamuuliza maswali Tisa yafuatayo
1. Ni lini na kwa nini mpaka sasa hakuna uchunguzi wowote serikali iliyoufanya wa kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda na tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu na Je serikali yake lini itafungua jalada la uchunguzi huo?
2. Suala la katiba mpya tusubiri, tusubiri mpaka lini?
3. Kwa nini waliiba uchaguzi mkuu wa mwaka wa serikali za nitaa 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020 na hatimaye kutuwekea viongozi wasiotokana na sisi wananchi, Je ana mpango gani ili bungeni waingie wabunge halali wenye ridhaa ya wananchi?.
4. Yeye kama sehemu mojawapo ya bunge, anachukua hatua gani kulinda katiba baada ya uwepo wa wabunge 19 ndani ya bunge ambao ni kinyume cha katiba?
5. Kwa kuwa hatuna uwezo wa kunufaika na madini yetu ipasavyo kwa nini kwa yale madini ambayo hatujaingia mkataba, asiyaache chini mpaka tutakapopata uwezo wa kuyachimba sisi wenyewe?
6. Kwa kuwa Masheikh wa uamsho wako ndani sasa mwaka wa nane kinyume cha sheria za Zanzibar walipokamatiwa kwa nini asiwarudishe Wakashitakiwe Zanzibar au kumuagiza DPP afute kesi yao kwa kukosa ushahidi?
7. Kwa kuwa zuio la vyama vya siasa lilifanyika kinyume cha sheria na katiba, ni kwa nini serikali yako inaonekana kuendeleza ukandamizaji huo wakati uliapa kulinda na kutetea katiba?
8. Kwa kuwa serikali yako imejinasibu kuwa ni serikali ya Utu, inaonaje kiubinadamu ikatoa chochote kitu kwa watumishi wa umma waliolitumikia taifa hili kwa muda mrefu na kwa uadilifu licha ya kuwa na vyeti visivyo halali? - Ikumbukwe zoezi lile la uhakiki lilifanyika kwa ubaguzi maana wanasiasa na vyombo vya usalama hawakuguswa!
9. Kutokana na serikali kuwavunjia watu nyumba zao kimara-mbezi icha ya uwepo wa zuio la mahakama, na kwa kuwa nchi hii ni yetu sote serikali kwa nini in humanitarian ground isiwape chochote kitu waliovunjiwa nyumba hizo hasa ukuzingatia zoezi la uvunjaji wa nyumba zao lilifanyika kiubaguzi, kwa mfano wale wa mwanza hawakuvunjiwa kwa sababu za kisiasa ila wale wa kimara mbezi walivunjiwa eti kwa sababu za kisheria?
Mzigo huu wa maswali umeshiba. Asante sana mzee baba.Nitamuuliza maswali Tisa yafuatayo

Utaendekezaje - Bila shaka ulikuwa unamaanisha "utaendelezaje"
Duh!1. Tarehe ipi Jiwe lilikufa (Ya Ukweli)? 2. Wakati Jiwe anakata roho alikuwa anaweweseka maneno gani?
Hii ndio JF mkuu, kila mmoja anaandika atakaloDuh!
Sio kazi pekee ya Rais ila ni moja kati ya majukumu yake ya msingi...Kwani kazi ya Raisi ni kuulizwa tu Maswali?
Huu sio uzi wa maoni, huu ni uzi wa maswali mkuuMwambieni atekeleze tu Majukumu yake ipasavyo na asimamie haki ikiwemo ya Masheikh wa Uhamisho... na aunde tume ya kuchunguza watu walipotea au kupotelewa na ndugu zao bila kufahamika
Kulikuwa na umuhimu gani wa kutumia lugha ya matusi/kejeli?Kwani kazi ya Raisi ni kuulizwa tu Maswali? acheni uzwazwa...
Sawa mkuuNitamuuliza
1. Kwanini Benk ya Kilimo isitumike pia kuwekeza kwa vijana wanaomaliza vyuo kuwekeza katika miradi maalum itakayosimamiwa kwa program maalum bila vikwazo vya dhamana ya mali?
2. Ikiwa fedha za mikopo zimejenga madaraja ya juu na watu wanapita bure, kwanini fedha za mikopo za daraja ya kigamboni wananchi tunalipia kwa kutozwa kila siku? Kwanini serikali isilipie hizi pesa kama inavyofanya katika miradi mingine?