PreGE2025 Ukibisha wewe ni mfanya fujo!: Kupitia 4R za Mama, Matunda yanaonekana!

PreGE2025 Ukibisha wewe ni mfanya fujo!: Kupitia 4R za Mama, Matunda yanaonekana!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

The Dictator

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
4,475
Reaction score
12,281
Tuishi humo!

1745322279212.jpg

Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali, Amedeus Shayo amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwa kielelezo kizuri cha haki nchini kutokana na juhudi kubwa anazozifanya ili kuhakikisha Watanzania wanafikiwa na huduma za kisheria pamoja na kupata haki zao kwa wakati.

Ameeleza kuwa kupitia falsafa yake ya 4R pamoja na kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, matunda yanaonekana katika utoaji haki kwa wananchi, akieleza kuwa wanasheria wa Serikali wamekuwa wakishiriki moja kwa moja katika utoaji haki na msaada wa kisheria kwa wananchi kupitia kamati za kisheria za wilaya na mikoa na sasa masuala ya utoaji haki sio changamoto tena.

Shayo ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma leo Aprili 15,2025.

Ameongeza kuwa juhudi hizo za Rais Samia Suluhu Hassan zimesaidia kusogeza huduma za kisheria karibu na wananchi.
 
Kwa kuwanyima CCM nafasi ya kutoa hata fomu moja (1) ya kugombea ama kutia nia ya Urais kwakweli 4R zinafanya kazi vizuri sana.
 
Back
Top Bottom