Ukichelewa kuoa au kuolewa ni ngumu kumpata mwenza mnayeendana

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Ukichelewa kuoa au kuolewa ni NGUMU SANA kumpata mwenza mnayeendana.

Huu ni mtazamo tu wakuu japo najua kila mtu anaweza kuwa na namna yake ya kutazama mambo lakini mimi naona kama ni ngumu sana kwa wengi ya senior bachelors kupata wenza sahihi maana wale waliopaswa kuwa nao wanakuwa tayari wameoa au kuolewa kitambo na sasa wana maisha yao.

Nje ya hapo senior bachelor inabidi apate mwenza aliyeishi kwenye ndoa halafu akaacha au kuachika na hawa wengine aliowazidi umri pakubwa ambao nao wana changamoto zao sio za kitoto.
 
Somo
====
Kama wewe ni mtu mwenye dhamira ya kuishi katika ndoa hakikisha unaoa au kuolewa mapema
 
Mwanaume Chelewa kuoa lakini uwe na pesa, utaoa yeyote unae mtaka
Ni sawa. sio kama ukichelewa kuoa aunkuolewa basi utakosa mtu wa kuoa au kuolewa naye, la hasha. ishu ni je utapata mtu sahihi wa kukufaa kwa umri wako?

Fikiria umepishana na mwenza wako kwa miaka 20 au 30 hapo mpo tofauti kwa vizazi viwili au hata vitatu, fikra na mitazamo ya maisha zipo tofauti sana. ndio ishu inayozungumziwa hapa. styms hata kutazama tv pamoja inakuwa changamoto.
 
Kuoa ama kuolewa ni lazima ? Mbona mnakariri maisha ? Kila mtu ajiamulie kadri atakavyoona inamfaa
Haulazimishwi mkuu ila sisi kama jamii tunategemea kuwa umeoa au kuolewa kama uko sawa na hauna vipingamizi mfano mapadre na masista wa baadhi ya imani wanaokatazwa kuoa au kuolewa kulingana na imani yao.
 
Kuoa sio lazima unaweza ukaishi mwenyewe Kwa raha BIla stress na mtu yeyote.Unatumia kibunda chako mwenyewe unajitibu mwenyewe,Uhuru wako mwenyewe,kusali mwenyewe.Usiangalie mitazamo ya jamii inayolazimisha lazima uoe.
 
Hakikaaa kabisaaaa watu wanakua na Iman potofu kuhusu ndoa kwamba lazima watu waoane
 
Somo
====
Kama wewe ni mtu mwenye dhamira ya kuishi katika ndoa hakikisha unaoa au kuolewa mapema
Mapema ni muda gani?
Kwa mtu atayeishi duniani miaka 98 mapema inaweza kua ni miaka 42,ila mwengine ataishi duniani miaka 46 miaka 28 kwake itakua michache sana
 
Kuoa sio lazima unaweza ukaishi mwenyewe Kwa raha BIla stress na mtu yeyote.Unatumia kibunda chako mwenyewe unajitibu mwenyewe,Uhuru wako mwenyewe,kusali mwenyewe.Usiangalie mitazamo ya jamii inayolazimisha lazima uoe.
kuoa na kuolewa itabaki kuwa ni dhana na mtazamo wa kijamii kama ulivyosema lakini ukweli unabaki kuwa ndio njia pekee ya kufanya binadamu tuongezeke hapa duniani. jaribu tu kufikiri dunia bila kuzaana Soft Guy tungempata wapi?
 
Ukichelewa kuoa au kuolewa ni NGUMU SANA kumpata mwenza mnayeendana.

Huu ni mtazamo tu wakuu japo najua kila mtu anaweza kuwa na namna yake ya kutazama mambo lakini mimi naona kama ni ngumu sana kwa wengi ya senior bachelors kupata wenza sahihi maana wale waliopaswa kuwa nao wanakuwa tayari wameoa au kuolewa kitambo na sasa wana maisha yao.

Nje ya hapo senior bachelor inabidi apate mwenza aliyeishi kwenye ndoa halafu akaacha au kuachika na hawa wengine aliowazidi umri pakubwa ambao nao wana changamoto zao sio za kitoto.
Kikubwa libeneke,. Kikubwa mapenzi
 
Kuchelewa/kuwahi ni umri gani kwani??
maisha ya mtz ni miaka 50-60 maana yake ukioa au kuolewa kwenye miaka 45 una kati ya miaka 5 hadi 15 ya kumlea huyo mtoto uliemzaa. maana yake unavyochelewa zaidi kuzaa kuna uwezekano ukafa kabla hata haujamwezesha dogo kuanza class one.
 
Ukichelewa kuoa au kuolewa ni NGUMU SANA kumpata mwenza mnayeendana.

Huu ni mtazamo tu wakuu japo najua kila mtu anaweza kuwa na namna yake ya kutazama mambo lakini mimi naona kama ni ngumu sana kwa wengi ya senior bachelors kupata wenza sahihi maana wale waliopaswa kuwa nao wanakuwa tayari wameoa au kuolewa kitambo na sasa wana maisha yao.

Nje ya hapo senior bachelor inabidi apate mwenza aliyeishi kwenye ndoa halafu akaacha au kuachika na hawa wengine aliowazidi umri pakubwa ambao nao wana changamoto zao sio za kitoto.
Ndoa hazina formula
 
Kulala wawili raha bana inapunguza hata stress, siwaelewi mnaokataa ndoa.
 
Oa by 30 kwa mwanaume, Zaa watoto wa 2 huku ubatafuta pesa kwa bidii, by 40 mwanamke akizingua toka kwenye ndoa, tumia pesa zako kwa Vitoto hata vya 25, usipende sana; vitakutesa; kaa kisanii
 
Kuoa ama kuolewa ni lazima ? Mbona mnakariri maisha ? Kila mtu ajiamulie kadri atakavyoona inamfaa
Kama huoi au kuolewa basi zaa . Wengine hawazai hivyo kupelekea wasiwasi kwa wazazi ndugu na jamaa.
 
Itakuwa hauna Hela tu.mwanaume ukiwa na Hela unaweza kuoa wa miaka ishirini wakati wewe ukiwa na miaka hamsini
 
Back
Top Bottom